Mamlaka zilizohusika na utoaji wa leseni za udereva bila vyeti vya mafunzo zichukuliwe hatua kali

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,551
Kiutaratibu, ni lazima mtu ahudhurie mafunzo ya udereva, ajaribiwe na mamlaka husika ( Traffic) ndipo apewe leseni ya udereva.


Sasa hapa naona tunshindwa kuelewa.

Ilikuwaje madereva wakapata leseni halali bila viambata ( vyeti vya mafunzo) vyovyote ? Nani aliidhinisha leseni zitolewe na nani alitoa leseni hizo ?

Isile upande mmoja.
 
Halafu watu wanaiita tanzania ni moja ya nchi changa. Kwani nchi iliyokomaa ina umri wa miaka mingapi tangu kupata uhuru?
CCM ndo imetufikisha hapa tulipo, badala ya kupiga hatua kusonga mbele tunarudi nyuma. Ngoja kwanza Zimbabwe watufundishe jinsi ya kuchagua watawala, nitakuja baadae.
 
Nchi ya vituko always itakuwa ya vituko;drivers licence zingebidi ziwe zinatolewa na traffic dept.baada ya kufaulu mitihani yao,kwanza ya kuandika kuhusu alama,sheria za barabarani na control then unafanya test ya pili driving kwa vitendo,ukifaulu then unapewa leseni yako,TRA they got nothing to do na leseni hizi;wapi umejifunza kuendesha sio tatizo kabisa maadam umefaulu mitihani itakayoendeshwa na traffic dept.
 
Kati ya matamko niliyotegemea yatasitisha kabla ya utekelezaji ni hili. Jana Muslimu kasema wametoa miezi 5 hadi Desemba madereva wote wawe na vyeti. Kwa maana nyingine wasio na elimu wameruhusiwa kufanya Kazi ya kitaalamu huku wakisoma Maskini Tanzania!!
 
Nijuavyo mimi, ilikuwa kama una askari unafahamiana nae ukimpa laki na 30 leseni unapata class D, ukiwa unafahamiana na Trafiki leseni utapata, ukiwa unafahamiana na mfanyakazi wa TRA leseni utaletewa nyumbani. Kilichopandwa ndicho kinachotoa matunda sasa, sioni cha ajabu hapo.
 
Nijuavyo mimi, ilikuwa kama una askari unafahamiana nae ukimpa laki na 30 leseni unapata class D, ukiwa unafahamiana na Trafiki leseni utapata, ukiwa unafahamiana na mfanyakazi wa TRA leseni utaletewa nyumbani. Kilichopandwa ndicho kinachotoa matunda sasa, sioni cha ajabu hapo.
Na wengi ndio tulizipata zetu namna hiyo miaka 18 iliyopita
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom