Mamlaka za Marekani zakabidhiwa kanda mpya inayomuonesha R. Kelly akiwanyanyasa Wanawake kingono

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,446
16,301
_105970297_gettyimages-1134965039-594x594.jpg

Gary Dennis aliwaambia wanahabari kuwa alionelea ni ''wajibu wake'' wa kimaadili kuwafahamisha maafisa wa usalama.

Mtu mmoja nchini Marekani anadai kuwa amepata kanda ya video inayomuonesha mwanamuziki wa R. Kelly "akiwanyanyasa kingono wasichana wadogo wenye asili ya wamarekani weusi ."

Gary Dennis amewaambia wanahabari kuwa ameiwasilisha kanda hiyo kwa mamlaka za Marekani baada ya kuipata ndani ya nyumba yake.

R. Kelly alishitakiwa mwezi uliyopita na makosa kumi ya unyanyasaji wa kingono unaohusisha waathiriwa wanne watatu kati yao wasichana wadogo.

Msanii huyo wa muziki wa R&B amekanusha kuwa ndani ya video hiyo pamoja na tuhumu zote zinazomkabili

Akipatikana na hatia Kelly anakabiliwa na kifungo cha miaka saba kwa kila kosa..

Bwana Dennis,ambaye ni mhudumu wa makaazi ya watoto, amesema kuwa alipata kanda hiyo alipokuwa akipanga sanduku la video za zamani.

Aliamua kutazama moja ya video hiyo baada ya kuona imeandikwa jina "R. Kelly".

_105141349_gettyimages-922620958.jpg


Alitarajia kuona onyesho lake la zamani lakini badala yake ashangaa kuona picha za kingono anazodai zinamhuisisha msanii huyo.

Bila kuelezea kwa undani yaliyomo kwenye kanda hiyo, bwana Dennis anasema kuwa alimuon "[R. Kelly] akiwaambia wasichana hao kufanya alivyowaagiza kufanya na kuashiria kuwa ni yeye mwenyewe aliyekuwa akinasa video hiyo."

Anasema baada ya kugundua hilo alionelea ni ''wajibu wake'' wa kimaadili kuwafahamisha maafisa wa usalama.

Lakini kabla ya kufanya hivyo anasema kuwa aliwasiliana na wakili Gloria Allred,ambaye anawaakilisha wanawake wanaodai kudhulumiwa kingono na mwanamuziki R. Kelly.

Baada ya hapo kanda hiyo iliwasilishwa kwa waendesha mashtaka wa jiji la New York.

Bi Allred, amesema kuwa Dennis hakuwa na uhusiano wa kibinafsi na R. Kelly na kuongeza kuwa alipewa kanda hiyo na rafiki yake akifikiria maudhui yake ni ya matukio ya kitambo ya michezo.

Mapema mwezi huu nyota huyo wa miondoko ya R&B alionesha masikitiko makubwa kuhusiana na tuhuma dhidi yake katika kipindi kimoja cha asubuhi cha televisheni.

Kelly alikiri kufanya mambo mengi mabaya miaka ya nyuma lakini aliomba radhi kwa wanawake ambao alikuwa na mahusiano nao.

Kelly anaamini kuwa , ni rahisi sana kwa msanii kushutumiwa na madai mbalimbali, kitu ambacho watu wanafanya ni kupiga simu tu.

BBC
 
Huyo atakuwa aliomba pesa nyingi sana kwa R.Kelly ili atanze siri, aliponyimwa ndio anajidai eti alihisi ni wajibu wake, halafu hiyo video anasema R.kelly ndio kairekodi, hivyo haonekani bali ni sauti tu, sasa sauti zinafanana, haiwezi kuwa ushahidi hata siku moja.
 
Wanakupa fame, watakuletea vimalaya uchwara huku wakikushoot clips, we hutaona hatari ya baadae kipindi hampo tena side moja…. Wakati ukifika ndio utajua hujui, Binadamu wabaya. If nobody is perfect why ain’t we all in jail?
 
Serikali imwekee ulinzi mkali huyu bwana.....R.Kelly apigwe hata maisha jela na iwe fundisho kwa wapumbafu wengine
 
Kelly alikiri kufanya mambo mengi mabaya miaka ya nyuma lakini aliomba radhi kwa wanawake ambao alikuwa na mahusiano nao

BBC Swahili ya akina Zuhura Yunus na Salim Kikeke hii, viwango vimekuwa vya Kiswahili. Mswahili ni mtu ambae toka utotoni hajafundishwa logic.

There is no way in hell R Kelly akakiri mabaya na kuomba radhi wakati ana face federal indictments kulia na kushoto na kuna shutuma za ma documentary zinamuanda za “Surviving R Kelly.”
Kwenye ile interview alikwenda kujisafisha na kujitetea, sio kuomba radhi. Never that!

Unatuambia R Kelly alikiri kafanya mabaya, na kwenye interview hiyo hiyo akalalamika kwamba watu maarufu hushutumiwa madai mbali mbali kwa kupiga tu simu. Mwandishi hakumuuliza “umekiri mwenyewe, kwani uongo”? Where is the logic there ?

Unafanya kazi BBC huelewi maelezo ya mtu anajitetetea saa mbili nzima anarudia yale yale mpaka anasimama analia machozi. Bado huelewi. Mbona utotoni tulikuwa tunaelewa movie za James Bond na John Rambo hata kwa lugha picha na lugha mwili, body language ?

BBC
 
Back
Top Bottom