Mamlaka za Marekani zakabidhiwa kanda mpya inayomuonesha R. Kelly akiwanyanyasa Wanawake kingono

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,986
2,000
_105970297_gettyimages-1134965039-594x594.jpg

Gary Dennis aliwaambia wanahabari kuwa alionelea ni ''wajibu wake'' wa kimaadili kuwafahamisha maafisa wa usalama.

Mtu mmoja nchini Marekani anadai kuwa amepata kanda ya video inayomuonesha mwanamuziki wa R. Kelly "akiwanyanyasa kingono wasichana wadogo wenye asili ya wamarekani weusi ."

Gary Dennis amewaambia wanahabari kuwa ameiwasilisha kanda hiyo kwa mamlaka za Marekani baada ya kuipata ndani ya nyumba yake.

R. Kelly alishitakiwa mwezi uliyopita na makosa kumi ya unyanyasaji wa kingono unaohusisha waathiriwa wanne watatu kati yao wasichana wadogo.

Msanii huyo wa muziki wa R&B amekanusha kuwa ndani ya video hiyo pamoja na tuhumu zote zinazomkabili

Akipatikana na hatia Kelly anakabiliwa na kifungo cha miaka saba kwa kila kosa..

Bwana Dennis,ambaye ni mhudumu wa makaazi ya watoto, amesema kuwa alipata kanda hiyo alipokuwa akipanga sanduku la video za zamani.

Aliamua kutazama moja ya video hiyo baada ya kuona imeandikwa jina "R. Kelly".

_105141349_gettyimages-922620958.jpg


Alitarajia kuona onyesho lake la zamani lakini badala yake ashangaa kuona picha za kingono anazodai zinamhuisisha msanii huyo.

Bila kuelezea kwa undani yaliyomo kwenye kanda hiyo, bwana Dennis anasema kuwa alimuon "[R. Kelly] akiwaambia wasichana hao kufanya alivyowaagiza kufanya na kuashiria kuwa ni yeye mwenyewe aliyekuwa akinasa video hiyo."

Anasema baada ya kugundua hilo alionelea ni ''wajibu wake'' wa kimaadili kuwafahamisha maafisa wa usalama.

Lakini kabla ya kufanya hivyo anasema kuwa aliwasiliana na wakili Gloria Allred,ambaye anawaakilisha wanawake wanaodai kudhulumiwa kingono na mwanamuziki R. Kelly.

Baada ya hapo kanda hiyo iliwasilishwa kwa waendesha mashtaka wa jiji la New York.

Bi Allred, amesema kuwa Dennis hakuwa na uhusiano wa kibinafsi na R. Kelly na kuongeza kuwa alipewa kanda hiyo na rafiki yake akifikiria maudhui yake ni ya matukio ya kitambo ya michezo.

Mapema mwezi huu nyota huyo wa miondoko ya R&B alionesha masikitiko makubwa kuhusiana na tuhuma dhidi yake katika kipindi kimoja cha asubuhi cha televisheni.

Kelly alikiri kufanya mambo mengi mabaya miaka ya nyuma lakini aliomba radhi kwa wanawake ambao alikuwa na mahusiano nao.

Kelly anaamini kuwa , ni rahisi sana kwa msanii kushutumiwa na madai mbalimbali, kitu ambacho watu wanafanya ni kupiga simu tu.

BBC
 

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
22,196
2,000
Huyo atakuwa aliomba pesa nyingi sana kwa R.Kelly ili atanze siri, aliponyimwa ndio anajidai eti alihisi ni wajibu wake, halafu hiyo video anasema R.kelly ndio kairekodi, hivyo haonekani bali ni sauti tu, sasa sauti zinafanana, haiwezi kuwa ushahidi hata siku moja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom