Mamlaka za maji safi na maji taka hazitakiwi kukatia wateja huduma za maji

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
59,043
2,000
Unaambiwa kwenye sheria za Tanzania, hairuhusiwi Mwananchi yeyote kukatiwa maji pale anaposhindwa kulipia bili yake ya mwezi, hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Maji safi na Mazingira ya mwaka 2019.

“Mtu yeyote anaetumia maji ambayo yanatoka kwenye Mamlaka ya Maji Tanzania anatakiwa kisheria kulipia bili yake ya maji baada ya matumizi lakini ikitokea akapata changamoto za kifedha akashindwa kulipa kwa wakati basi Mamlaka haipaswi kumkatia maji Mtu huyu”

“Sheria kwenye kifungu cha 72 inasema ikitokea Mtu ameshindwa kulipia anatakiwa kupewa notisi ya siku 30 na akishindwa kulipia ndani ya hizo siku 30 basi Mamlaka itatakiwa kumshitaki Mtu huyo” - Wakili Hamza Jabir wa Avis Legal.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom