Mamlaka za maji kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka za maji kulikoni?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Namnauka, Jan 23, 2010.

 1. N

  Namnauka Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau naomba tuliangalie suala hili la mamlaka za maji mikoani au wilayani kushindwa kusambaza maji ya kutosha kwa wananchi wake. Utakuta kuna vyanzo vya maji vingi tu lakini kubuni njia za kuyapata na kuyasambaza mpaka waje wachina watufanyie.

  Wakati mwingine unakuta maji yapo na mtandao wa mabomba upo ila hayasambazwi kwasababu tu wananchi wameshindwa kupata hela za kuunganishia maji.

  Wazo langu kwanini mamlaka zisiunganishe maji kwa wanaotaka kwa mkopo nafuu wa labda mtu alipe taratibu ndani ya mwaka mmoja au miwili ambapo kwa water connection fee ya Tshs.70,000.00 kwa mwezi itakuwa Tshs.5833.00 miezi kuni na mbili au nusu ya ke kwa miezi 24. Njia hii ilifanywa na NHC ambapo watu walikuwa wanalipa kidogo katika kodi za kila mwezi mpaka walimaliza madeni yao.

  Utaratibu huu sio tu utawahakikishia wananchi wengi zaidi kupata maji safi lakini pia kutakuwa na mapato yatokanayo na ulipiaji wa ankara za maji za kila mwezi kutokana na matumizi ya maji wakati huo huo connection fee nayo inalipwa kwa mwezi.
   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi ule mradi wa Wachina kusambaza maji umeishia wapi niliwaona Kibamba, Kimara, Kunduchi ila sasa ziii
   
Loading...