Mamlaka za Barabarani Dar es Salaam naomba ziitazame barabara ya Kimara - Mbezi

Underwood

JF-Expert Member
Dec 25, 2020
1,909
3,104
Za asubuhi Wanajamvi,

Nadhani watumiaji wa barabara hiyo ni mashuhuda kuwa wakati inapotokea lane moja katika barabara hiyo kuwa katika matengenezo hasa nyakati za usiku, huwekewa mapipa yenye rangi nyekundu na nyeupe ili kuzuia magari na vyombo vingine kupita katika lane hiyo.

Changamoto ipo kwenye haya mapipa hasa nyakati za usiku ambapo madereva wa magari ambayo yana taa hafifu huishia kupata ajali kwa kwa kuparamia mapipa hayo kwa sababu huenda wakati wanapita mchana mapipa hayo hayakuwepo.

Jambo hili limefanya ajali za barabarani nyakati za usiku kuwa nyingi, watumiaji wa barabara hii nadhani watakuwa mashahidi namna wanavyo ona matokeo ya ajali hizo nyakati za asubuhi.

Naziomba mamlaka za barabara zinazohusika zitatue changamoto hii kwa kutumia vizuizi vyenye uwezo wa kuakisi mwanga (reflectors) ili hata madereva ambao vyombo vyao vina taa hafifu waweze kuona vizuizi hivyo.

Wenu katika ujenzi wa taifa.

Underwood
 
e87bf5ef-ab21-4e39-8800-61559fbd6336.jpg
 
Zimewekwa alama uendeshe 30kph. Kwa speed hiyo huwezi gonga hizo pipa hata gari isipokuwa na taa kabisa. Tatizo mnataka muende 80kph ndio maana saa hizi zile njia kuna traffic wanapiga torch kujipigia hela kutoka kwa wadwanzi kama wewe
 
Zimewekwa alama uendeshe 30kph. Kwa speed hiyo huwezi gonga hizo pipa hata gari isipokuwa na taa kabisa. Tatizo mnataka muende 80kph ndio maana saa hizi zile njia kuna traffic wanapiga torch kujipigia hela kutoka kwa wadwanzi kama wewe

Hizo alama hazipo
 
Back
Top Bottom