Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) yakanusha kubaini vyeti 'feki' JWTZ na Polisi

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA,kupitia mkurugenzi wake,wamekanusha kubaini vyeti feki ktk JWTZ na Polisi,katika tamko hilo NIDA wamesisitiza kuwa wao hawana uwezo wala mamlaka ya kubaini vyeti feki...na hivyo taarifa zilizotelewa na kunukuliwa ktk vyombo vya habari ni upotoshaji!

Mkurugenzi ndugu Maimu,amesisitiza kuwa sintofahamu ya JWTZ na Polisi si ktk vyeti tu,bali ktk nyaraka nyingine zaidi ya vyeti vya kitaaluma..

Maana upatikanaji wa vitambulisho unahusisha cheti cha kuzaliwa, Personal Record Form,barua toka kwa Mtendaji wa Mtaa,Uthibitisho wa barua ya kuitwa kazini n.k!!hivyo ktk hayo uwenda ni kipengele cha Personal Record Form ndo hakikuwa sahihi na si pengine vyeti vya kughushi..hivyo NIDA inaziachia Mamlaka(Necta? UWT?) husika kuthibitisha kama JWTZ na Polisi wana vyeti feki

Kama kweli tunaweza kuwa wakweli tunaweza kukubaliana kuwa kuna vitendo vingi vya kugushi na kuna watu kweye nyadhifa kubwa wana phd za ajabu, wengine wanazo za kuokota au za kupewa sioni ajabu, kama polisi na jeshi watakuwa nazo nyingi, sio haki watu wa juu waweze kufanya hivyo na wa chini wasifanye hivyo.
 
Kama ni kweli Mkurugenzi alinukuliwa vibaya, kwanini umchukue takriban week nzima kukanusha hiyo taarifa? Wamefungwa midomo tayari? Increadible!

FJM hata mimi naamini huyo mkurugenzi atakuwa ametishwa na kutakiwa akanushe taarifa yake aliyoitoa kwa wananchi.
Nchi hii inaongozwa na watu wajanja wajanja, shule zao za mashaka mashaka.
Nadhani wameona wakubwa wenye scandal ya kutumia vteti visivyo vya kwao wakaamua kuwanusuru kwa kumtisha ndg. Maimu.
 
Last edited by a moderator:
Unajua swala la vyeti feki lazima NIDA wafunike kombe kwani Watoto wa wakubwa wengi wanavyeti feki

MMESAHAU KASFA YA WAFANYAKAZI WA B.O.T WENGI KUBAINIKA KUFOJI VYETI WAKATI JK ANAINGIA KWA KASI MPYA KWELIKWELI
 
Binafsi nimeshiriki ktk zoezi lka NIDA nimejaza fomu,
Sasa katika kujaza academic details, unapaswa ujaze shule uliyosoma, mwaka uliomaliza, na pia namba ya cheti,
Sasa unakuta majina matatu ya watu tofauti yanafanana yakiwa yanafanana namba za cheti, mwaka wa kumaliza elimu hiyo, shule waliosoma waajiriwa hao, sasa unajiuliza inakuwaje watu hawa wafanane majina, namba ya cheti, shule waliohitimu, na mwaka wa kumaliza?

Idadi ya waliobainika itaongezeka kadiri ziezi hili litakavyoendelea kwa kukusanya taarifa kwa waajiriwa wa kada, na taasisi nyingine,
Utakuta jina na cheti kimoja linajitokeza kwa mwajiriwa kutoka jeshi la polisi, mtu huyo huyo tena unamkuta kaajiriwa ktk idara ya afya, halafu NIDA tena wanapoenda kuchukua taarifa za waajiriwa wa TAKUKURU jina hilo hilo tena na namba zile zile za cheti wanazikuta huko,

Tusubiri tuone
 
Hii ndo Tanzania bwana!! Upuuzi kila kukicha! Waendelee na kazi, hao wanaobainika wameiba vyeti wapigwe chini mara moja. Vijana kibao wapo mtaani wenye taaluma za ukweli, hawapati kazi kumbe kazi zimekamatiwa na majambazi!! Hii itakuwa njia nzuri ya kubadilisha mfumo wa kulindana uliotamalaki hapa nchini. Nashauri zoezi lisonge mbele, hao wezi wa vyeti hatuwezi kuwaogopa kiasi hicho. Vitambulisho ni kwa maslahi ya Taifa, wao wanalinda matumbo yao...
 
Hivi kiongozi anaweza kunukuliwa/kuelewekavibaya kweli? au waandishi Wa habari hawajui kiswahili!!Hii Serikali ya kulindana tutafikishana pabaya.Sasa sie wananchi tumwamini nani?Nida walitoa taarifa wenye makosa wachunguzwe ikibainika hatua Kali zichukuliwe,Kama hatutafanya hivi ktk Serikali hii hakuna kitakachosonga mbele.Na kwa nini wachukue muda mrefu kukanusha?,usaniii mwingine tena Serikalini
ndugu, yakubidi uungane na rais wetu mpendwa Jk asiyefahamu kwa nini Tanzania ni masikini.

Kwa sababu inawezekana walioiagiza NIDA 'ifute kauli' ndio hao hao iliowasema, sasa kama watakuwa na nguvu kubwa hivyo ya ku-destruct (kuzuia ukweli usijulikane) na hayo maamuzi mengine wanaamuaje huko waliko na 'vyeti vyao' hivyo!?

Ni masikitiko makubwa kwa sehemu hii ya sayari ya dunia!

 
Mara nyingi hawa watu wanakujaga baadae wanasema"nilinukuliwa vbaya na vyombo vya habari" wanataka kusema waandishi wetu ni makanjanja namna hiyo? Wako wapi waandishi wajitokeze sasa wapinge hili la kusukumiwa lawama kila saa
 
NIDA wametoa ufafanuzi si kukanusha. Wanachosema ni kwamba kulikuwa na mapungufu yakiwamo ya vyeti, majina kufanana na mtu mmoja kujaza fomu mbili na mtu kujithibitishia fomu yake.
 
Binafsi nimeshiriki ktk zoezi lka NIDA nimejaza fomu,
Sasa katika kujaza academic details, unapaswa ujaze shule uliyosoma, mwaka uliomaliza, na pia namba ya cheti,
Sasa unakuta majina matatu ya watu tofauti yanafanana yakiwa yanafanana namba za cheti, mwaka wa kumaliza elimu hiyo, shule waliosoma waajiriwa hao, sasa unajiuliza inakuwaje watu hawa wafanane majina, namba ya cheti, shule waliohitimu, na mwaka wa kumaliza?

Idadi ya waliobainika itaongezeka kadiri ziezi hili litakavyoendelea kwa kukusanya taarifa kwa waajiriwa wa kada, na taasisi nyingine,
Utakuta jina na cheti kimoja linajitokeza kwa mwajiriwa kutoka jeshi la polisi, mtu huyo huyo tena unamkuta kaajiriwa ktk idara ya afya, halafu NIDA tena wanapoenda kuchukua taarifa za waajiriwa wa TAKUKURU jina hilo hilo tena na namba zile zile za cheti wanazikuta huko,

Tusubiri tuone

nayaamini uliyoyaandika kama ni kweli ulishiriki kwenye hili zoezi vinginevyo wabadili details au info zinazohitajika kwenye hivyo vitambulisho ila suala la kughushi au cheti kimoja cha elimu/taaluma kutumiwa na mtu za ya mmoja lipo na si suala la kukanusha au kutoa ufanunuzi tatizo ni nani wa kumfunga paka kengele na naamini huu ndo utakuwa mwanzo
 
NCHI YA MFALME JUHA!
HIVI WATU WAMEKUSHUHUDIA UMEDONDOKA CHINI TENA KWENYE TOPE,
THEN UNARUDI BAADAYE MBAYA ZAIDI KWA WATU WALEWALE WALIOKUSHUHUDIA
UNADONDOKA, NA KUSEMA.."HUJAWAI KUDONDOKA"??? kuna tatizo hapa...either mtoa mada
ameamua kuburudisha baraza la Ghaawa au Mkurugenzi anamatatizo fulani!

Watanzania na Viongozi wetu wafike sehemu wawe na uwezo wa kuthubutu
kuita kitu kwa majina halisi...call a spade a spade..hata kama kisu iko kwa shingo!
 
WAIT!

Labda humu ndani wapo ambao tayari wameshapitia huo utaratibu wa kupatiwa vitambulisho vya uraia. Ina maana jamaa wanahitaji mtu kwenda na academic certificates?! Kama sio, then inawezekana kabisa kwamba palikuwa na upotoshaji au ku-sum up information.

Labda NIDA waligundua majina yanayofana kwa 100% kwa mtumishi zaidi ya mmoja! Bila shaka haya si yale majina Issa Mohamed Mussa; la hasha! Hivi ukutane na watu wawili tofauti na wote wanaitwa Jakaya Mrisho Kikwete au Zitto Zuberi Kabwe!!

Bila shaka hapo taarifa itakayotolewa ni kugundulika kwa watu wenye majina yanayofanana ambao probably wametumia cheti kimoja!

Ni hivi ktk form ya maombi ya utambulisho kutoka NIDA Ktk kipengele f ambayo inahusu kumbukumbu binafsi unapaswa kujaza namba ya cheti cha form 4 & 6 na nyaraka zingine kama passport, leseni ya udereva na nk.na unapaswa kuambatanisha na nakala ya hizo nyaraka ulizoandika namba zake. Hivyo ni rahisi kuweza kukamata watu wawili au zaidi wanaotumia cheti kimoja, na kiuhalisia watu hao wapo wengi wanaotumia vyeti vya ndugu, jamaa na marafiki na kwa hilo Maimu hajakosea alisema kile alichokiona.
 
Mkwara huo umepigwa tayari. Nchi hii kwa kweli hatuwezi endelea. Pengeine ukiona hivyo ujue kati ya hao polisi 700 kova naye yupo.
 
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya VItambulisho vya Taifa- NIDA ,anatarajiwa kupigwaa chini wakati wowote kuanzia sasa....kwa kosa kubwa la kihaini la kuvunja sheria ya usalama wa Taifa,Taratibu za usalama wa Taifa zinakataza mtu ,taaisis au jumuia yeyote kutoa utambuzi wa Afisa au maafisa au watumishi wa idara za usalama ,na vyombo vyao...,Aidha ni marufuku kutoa taarifa yeyote itakayoonesha uwezo wa taasisi au chombo cha usalama .....ikiwemo majeshi.

Taarifa zilizotolewa na NIDA zimeonesha udhaifu mkubwa wa kiuweledi .....,wa kutoa taarifa za undani juu ya uwezo wa maafisa na askari wa majeshi yetu,katika Hali ya kawaida ....NDugu Mwaimu ...alikuwa na uwezo kabisa wa kuandika barua ya Siri kwenda kwa Amiri jeshi mkuu au mkuu wa majeshi kueleza juu ya kile alichokibaini.......ili aweze kujibiwa....na Kushauriwa cha kufanya......,Kiukweli hakuna anayekataa kazi Yake ila ni utaratibu mbovu alioutumia kutokea taarifa..hizo nyeti kana kwamba alikuwa amekagua .....sekta ya umma ...ie walimu, madaktari ,etc...

Katika Hali ya kawaida ya usalama inaelezwa kuwa Askari 250 wa jeshi la wananchi waliogundulika kuwa na majina mawili mawili...au yanayotofautiana na vyeti ....wengi wao wanatoka kitengo Nyeti cha Millitary Intelligence .....ambao karibu wote huwa na ...majina feki,,passport na VItambulisho zaidi ya kimoja...au hata passport za mataifa mengine....kadiri ya mikakati ya kijeshi.......Ni kosa la kihaini kutambua maaskari wa aina hii maana unaweza kuwasababishia Maafa na kuvuruga mipango Yao...,Pia imebainika kuwa ni maaskari wa kitengo hichi ambao wengine kwa sababu maalum ...wana VItambulisho vya idara Nyingine za kiraia ie ..TAnapa,wizara...na hata mashirika ya umma....au wizara ya nje.

Pia ndani ya jeshi la Polisi...Kati ya Hao askari polisi 700 ....wapo wa kitengo cha DCI...plain clothed police....,kitengo cha madawa ya kulevya...,Iterpol etc...ambao nao inaelezwa sio ajabu kukutana wanatumia majina tofauti na ya kwenye vyeti....kutokana na unyeti wa kazi Zao....

Haya ndio yanayofikia watu wa usalama kuona kuwa Ndugu Mwaim,hata Kama alikuwa na nia njema ....Kama Afisa wa serikali ...anayejuwa undani wake tayari amevunja sheria za usalama wa Taifa....kwa kushindwa kuwasiliana na vyombo husika katika Hali ya Usiri........stahili.
 
Huu ni uchochezi. Alichosema mkurugenzi wa NIDA siyo kile kinachoonekana katika yale yanayoonekana kwa wengine. Yeye alisema katika utendaji kazi wake alibaini vyeti vilivyokuwa na upungufu. Sehemu ya upungufu huo ni watu zaidi ya mmoja kutumia kutumia cheti chenye jina moja. Hilo halimaanishi kughushi. Ninaye mjomba wangu anaitwa Kassim Sabu Kassim, na bado nilisoma na mtu mmoja kuanza form 1 hadi 4 anayeitwa Kassim Sabu Kassim. Wote ni Waluguru wa Morogoro. Tofautisha kati ya kuwa na watu wawili walio na jina linalofanana na kughushi. Ni mambo mawili tofauti. Nadhani kama tunataka kuitendea mema nchi hii, tuache uchochezi.
 
Back
Top Bottom