Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) yakanusha kubaini vyeti 'feki' JWTZ na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) yakanusha kubaini vyeti 'feki' JWTZ na Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngaliba Dume, May 18, 2012.

 1. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA,kupitia mkurugenzi wake,wamekanusha kubaini vyeti feki ktk JWTZ na Polisi,katika tamko hilo NIDA wamesisitiza kuwa wao hawana uwezo wala mamlaka ya kubaini vyeti feki...na hivyo taarifa zilizotelewa na kunukuliwa ktk vyombo vya habari ni upotoshaji!

  Mkurugenzi ndugu Maimu,amesisitiza kuwa sintofahamu ya JWTZ na Polisi si ktk vyeti tu,bali ktk nyaraka nyingine zaidi ya vyeti vya kitaaluma..

  Maana upatikanaji wa vitambulisho unahusisha cheti cha kuzaliwa, Personal Record Form,barua toka kwa Mtendaji wa Mtaa,Uthibitisho wa barua ya kuitwa kazini n.k!!hivyo ktk hayo uwenda ni kipengele cha Personal Record Form ndo hakikuwa sahihi na si pengine vyeti vya kughushi..hivyo NIDA inaziachia Mamlaka(Necta? UWT?) husika kuthibitisha kama JWTZ na Polisi wana vyeti feki
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli Mkurugenzi alinukuliwa vibaya, kwanini umchukue takriban week nzima kukanusha hiyo taarifa? Wamefungwa midomo tayari? Increadible!
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamaa keshapigwa bit hii ngoma inawahusu wakubwa!
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,874
  Trophy Points: 280
  Hawakusema kuwa wamebaini vyeti feki bali walisema wamegundua kuwa ktk jwtz na polisi kuna watu wametumia vyeti ambavyo si vyao na vimetumika kwa zaidi ya mtu moja ktk maeneo mbali mbali, hili bado ni kosa kubwa.
   
 5. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Hivi kiongozi anaweza kunukuliwa/kuelewekavibaya kweli? au waandishi Wa habari hawajui kiswahili!!Hii Serikali ya kulindana tutafikishana pabaya.Sasa sie wananchi tumwamini nani?Nida walitoa taarifa wenye makosa wachunguzwe ikibainika hatua Kali zichukuliwe,Kama hatutafanya hivi ktk Serikali hii hakuna kitakachosonga mbele.Na kwa nini wachukue muda mrefu kukanusha?,usaniii mwingine tena Serikalini
   
 6. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mesage sent kwa wananchi hata Kama NIDA wangesema hawakuwahi kusema chochote juu ya vitambulisho.
   
 7. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nchi hii ina mambo! yani week imeisha ndo anakuja kukanusha, hakika hii ndo Tanzania! Tunajua viongozi wengi wamefoji vyeti! Hakika nchi yangu haina kiongozi tuna janga la Taifa!
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  WAIT!

  Labda humu ndani wapo ambao tayari wameshapitia huo utaratibu wa kupatiwa vitambulisho vya uraia. Ina maana jamaa wanahitaji mtu kwenda na academic certificates?! Kama sio, then inawezekana kabisa kwamba palikuwa na upotoshaji au ku-sum up information.

  Labda NIDA waligundua majina yanayofana kwa 100% kwa mtumishi zaidi ya mmoja! Bila shaka haya si yale majina Issa Mohamed Mussa; la hasha! Hivi ukutane na watu wawili tofauti na wote wanaitwa Jakaya Mrisho Kikwete au Zitto Zuberi Kabwe!!

  Bila shaka hapo taarifa itakayotolewa ni kugundulika kwa watu wenye majina yanayofanana ambao probably wametumia cheti kimoja!
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  tunasubiria part III
   
 10. M

  Manyovu Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Nafikiri ni suala tu la tafsri (interpretation) ya hiki unachokisema ambacho na mimi ndicho ninachofikiri.

  Sidhani kama NIDA wanaomba academic certificates ila wanachofanya ni kukupa fomu/kujaza fomu ambayo itakuwa na maelezo yako binafsi ya kuanzia kuzaliwa, kusoma na makazi. Sasa baada ya kuingiza majina yote kwenye mtandao ya watu wa Dar Es Salaam then ukakutana na watu wawili wenye majina ya John Masumbuko Lamwai wote wakionyesha walizaliwa mwaka 1970 wamesoma shule moja ya Sekondari, shule moja ya A level lakini wanafanya kazi ofisi mbili tofauti lazima ikupe conclusion kuwa mmoja wao atakuwa alitumia cheti cha mwingine kupata kazi.

  Na hiki ndicho nafikiri NIDA watakuwa walikiona na kukisemea kwani inachanganya sasa nani apewe kitambulisho kati ya watu hao wawili. Wanaweza kuwa walitumia vyeti ambavyo ni halali vya shule lakini mmoja wao amedanganya kusoma shule ambayo hakusomea kwani ametumia/alitumia cheti cha mwingine.

  Hatua ya pili sasa ni NIDA au chombo kingine kujiridhisha je aliyeko Jeshini/Polisi ndo mhusika halisi mwenye cheti au huyo mwingine aliyeko ofisi/taasisi nyingine ya serkali au ndani ya hayo hayo majeshi.
   
 11. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  NIDA, poleni blind and dumb we see nothing, hear nothing. Read between the lines please.
   
 12. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Alikurupuka bila kuwahusisha wahusika,

  we unasema wanajeshi 600 wamechakachua patakalika?

  Hili ni fundisho na wasirudie tena wasije kutuchafulia AMANI yetu.

  Hili ndio tatizo la taaluma kuingizwa na siasa, waandishi walitaka kujua kulikoni wamechelewesha zoezi, wakaona pa kutokea ni kuwatwisha mizigo walinda amani wetu.
   
 13. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  NIDA inafanya kazi vizuri tatizo ni MFUMO.Nyie mnafaham hata ikiundwa mamlaka kutoka mbinguni haiwezi kung'ata hadi hapo tutakapo badilisha mfumo kupitia katiba mpya.TUMPONGEZE MAIMU KWA KUTHUBUTU KUTUHABARISHA UKWELI.
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  mkuu kuna wakubwa wengi sana wanatumia majina ya ndugu zao kwenye kazi na wamepata vyeo. Hivyo kuwaumbua namna hii itahatarisha ajira zao na hadhi zao. Hili nililijua! Hivi vitambulisho haviji kukamilika milele. Sasa hivi wataanza mchakato upya. Huu ni upuuzi waliouanzisha wajanja wachache ili kupata ulaji. Hili shamba la bibi safi sana. Wanaolihudumia wanalala njaa,we unakuja unavuna na kuondoka.
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Be carefu
   
 16. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hii ndiyo maana nchi hii haukuna uongozi bali ujambazi na kwa namna hii hatuwezi kupata maendeleo hata kidogo, hiyo ilikuwa namna nzuri tu ya kuwaondoa watu wasiokuwa na sifa, lakini sasa mchakato huo unafunikwa kwa kuambiwa tena kanusha. Tanzania Jamani unapelekwa wapi usikokujua?
   
 17. Raiamwematz

  Raiamwematz Senior Member

  #17
  May 19, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hebu tupe chanzo cha hii habari........... kama ni kweli, basi huyo mkurugenzi ameshaambiwa anyamaze la sivyo hana kibarua..........
   
 18. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  ukilitizama kwa jicho la tatu MAIMU alifanya makosa kuyaongea hayo hadharani.at least angesisitiza kuwa postikodi na kufanya kazi pamoja na NEC ndio vimechelewesha kitambulisho kutoka.
   
 19. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  NIDA wanapokuwa ktk mchakato wa kukutengeneze kitambulisho cha Taifa, wanahitaji nyaraka zifuatazo... Cheti cha kuzaliwa au Affidavit, Passport ya kusafilia (kama unayo), cheti cha taalum (academic transicripts/certificates) cha elimu yako i.e Form IV, VI au chuo, Personal Record Form, form maalum kutoka NIDA itakayojazwa na kuthibitishwa na VEO au WEO (Ward Executive Officer) juu ya makazi yako, form nyingine maalumu toka NIDA yenye details mbalimbali kama mahali ulipozaliwa n.k!

  Hivyo kama kubaini udanganyifu huo, ni lazima NIDA walikuwa wakipata mkanganyiko ktk vyeti vya kitaaluma! Hali ni mbaya mana watu wengi sana wamefoji vyeti huko maofisini
   
 20. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kusoma kwenye gazeti mwaka jana, jamaa akilalamika kwamba kuna raia alijihunga na jeshi kwa kutumia jina lake baada ya kumuibia cheti chake. Hivi kumetokea nini mpaka huyu Mkurugenzi anakanusha taharifa kuhusu kughushi au tuseme cheti kimoja kutumiwa na watu zaidi ya mmoja, kwani NIDA hawana database filter ya kuweza kungamua utata huu! Hiyo wanayo sana, we sema tu sijuhi katishiwa nini?

  Nakwambia katika TAIFA letu hili ni watu wachache wenye ujasiri kama wa CAG (mkaguzi mkuu wa Serikali) wengi wetu tu woga kama nini sijuhi!!! Mimi huwa nasikitika sana nikiona mtu ambaye amesomea vizuri fani yake na kujuwa ethics zake, anakubali kuyumbishwa na wana siasa au watu wenye agenda zao - tukichezea zoezi hili la kuandikisha vitambulisho kwa kisingizio chochote kile, nchi hii itakwenda na maji.

  Huu ndio ungekuwa muda muhafaka wa kubaini ni watu gani wanawasilisha vyeti vya uongo au kutumia majina ambayo siyo yao hili watiwe msukosuko waeleze vyeti walivipata wapi na kama kweli ni Watanzania, lakini mambo yenyewe kama ndio haya tunayo shuhudia sasa hivi, basi mimi binafsi sitakuwa na imani na zoezi zima kusema ukweli!
   
Loading...