Mamlaka ya usafirishaji nchi kavu (LATRA) iruhusu daladala za bei ya juu/first class ama business class

Kipindi cha nyuma pale Mwenge kulikuwa na daladala za mbezi ila unalipa 1000. Sijui kama sasa yapo.

Full AC, level seat na hakuna kusimama hovyo njiani labda kama unashuka.

Wengi waliyakimbilia kwasababu yalikuwa yanapita njia ya chuo.
Wangeweka izo daladala zenye AC ingekuwa poa sana
 
Tulia wewe! Kipaumbele chetu ni :-

Mji wa Serikali​

Eneo: Jiji la Dodoma imetenga eneo la mji wa Serikali ambao upo katika Kata ya Ihumwa kilomita 17 kutoka katikati ya Mji. Eneo hili lina ukubwa wa Hekta 617.15 sawa na Ekari 1,542.88.

Mipaka: Mji wa Serikali kwa upande wa mangaribi unapakana na kambi ya Jeshi ya Ihumwa, Kaskazini-Mashariki unapakana na kata ya Mtumba na upande wa Kusini unapakana na barabara kuu iendayo Dar es salaam.

Mgawanyo: Mji wa Serikali umegawanyika katika maeneo tofauti kama ifuatavyo:-

  • Wizara za Serikali,
  • Ofisi za Mabalozi,
  • Nyumba za Serikali,
  • Huduma za Jamii,
  • Maeneo ya biashara,
  • Bunge,
  • Mahakama,
  • Maegesho ya magari,
  • Eneo la majitaka
Mifumo ya Maji: Mji wa Serikali utakuwa unatumia maji lita za ujazo 3,016.7 kwa siku. Mfumo wa majitaka utakuwa umeunganishwa na mtambo wa kisasa utakaofanya kazi ya kupokea majitaka na kuyachakata kuwa maji safi tena kwa ajili ya matumizi mengine.

Majitaka%20-%20Mtambo.jpg

Gharama: Gharama za Utekelezaji ujenzi wa Mji wa Serikali: Makadirio ya gharama za kukamilisha Mji wa Serikali ni Dola za Kimarekani 4,788,749,111 sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 10,709,176,758,503. Gharama hizi zinategemewa kutoka katika vyanzo mbalimbali vifuatavyo:-

  • Fedha za Serikali,
  • Wafadhiri,
  • Mashirika ya Umma,
  • Taasisi binafsi na za serikali, na
  • Mashirika binafsi.
Majengo1.jpg
Majengo2.jpg
Mitaa.jpg

TANBIHI: usitupangie cha kufanya, ka' umechoka kuishi Dar hama!

By utawala.
Hii ni kweli mkuu?
 
Hizo dala dala za kifahari zikruhusiwa mwendokasi (BRT) iendelee kuwepo kwani watu wanatofautiana kipato. Ndio maana leo tuna boda boda, bajaji, taxi za kawaida, ubber na bolt uchaguzi unabaki kwa abiria atumie usafiri gani kwa wakati gani. Na hili mamlaka zinazohusika zikishirikiana na wawekezaji wa usafiri wanaweza kufanya majaribio haraka kwa kuruhusu idadi fulani ya magari kwenye ruti mojawapo (mfano Posta - Mbezi, Posta - Gonngolamboto au Posta - Mbagala) kwa muda kama wa mwezi mmoja. Hiyo itwasaidia serikali na wawekezaji kujua changamoto na mafanikio kabla ya kuruhusu kwenye ruti zote.
 
Kabisa mkuu. Mwendokasi bado ibaki na iendelee kufanya kazi. Naamini si watu wote watakaokuwa na uwezo wa kupanda bus hizo.
 
Back
Top Bottom