Mamlaka ya Usafirishaji Baharini YafungiaBoti Tatu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya Usafirishaji Baharini YafungiaBoti Tatu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 26, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  [​IMG]


  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
  Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo.


  Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.


  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.


  Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo.


  Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao.


  Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.


  Kufuatia sheria hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili kinyume na maeneo ya Zanzibar.


  Akizungumzia Meli ya Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50 hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo ilivyo.


  Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  walikuwa wapi siku zote?
  mpaka watu wafe ndo washtuke?
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nyambafu...ndio wameamka eeh?? i think they're 20 years too late...shenzyyy taipu:nimekataa wataweza kuturudishia ndugu zetu tuliowapoteza...
   
 4. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna somo linaitwa "Consequence Management"Mlipaswa kujifunza kabla ya tukio.Nyie mpaka watu wafe ndio mnajifunza ilhali mmeishapoteza maisha ya watu wasio na hatia.Ajali za barabarani ,kila siku zinaua,na sabbau ni zilezile,barabara nyembamba ikiunganishwa na mwendo kasi, huku traffic wao wakichukua kitukidogo.
   
 5. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Too late
   
 6. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wamepata nguvu ya kuwakazia macho vigogo wenye boti - mradi isiwe changa la macho
   
 7. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa wanatangaza kuja kwa meli kubwa ya Azam, kwani hii kampuni ni ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar?
  Huu mkondo unaojaa mabaki ya meli zilizozama kuna siku hautapitika. Chukueni neno hili liwafae mbeleni.
   
 8. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mbuzi hawezi kuingia baharini...
   
 9. M

  Msajili Senior Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  makali ya Waziri mpya, isiwe nguvu ya 7 juu..
   
Loading...