Mamlaka ya nchi na kauli ya Mh. Rais Kikwete mkoani Dodoma

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Kuna habari hizi kuwa wakati mwenyekiti wa chama tawala akikaribia kumtangaza mgombea mwenza huko Dodoma 11 Julai 2010 aliongea masuala ya kitaifa na alikazia hotuba kwa kusisitiza kuwa yeye rais akisema hapana hakuna wa kubadilisha hata Mahakama. Habari hiyo pia imenukuliwa humu JF.

Kauli hiyo inayosemekana aliitoa rais Kikwete inazua maswali mengi kuliko majibu. Hivi rais Kikwete na serikali wanafahamu kuwa wananchi ndio msingi wa mamlaka yote? Je rais anafahamu kuwa Serikali inapata madaraka yote kutoka kwa wananchi kwa msingi wa Katiba? Rais wetu Kikwete akisoma ibara ya 8 kipengele cha 1a anaelewa nini? Kulingana na Katiba yetu hakuna aliye juu ya sheria. Na rais anaongoza nchi kutokana na Katiba inayotoa mamlaka sehemu mbalimbali ikiwemo Mahakama. Ni kwa vipi basi Rais aseme hata mahakama haiwezi kubadilisha alichosema yeye hapana? Inawezekanaje Rais atoe kauli ya kunyakua uhuru wa Mahakama ambao unaelezwa kwenye katiba ya nchi? Watanzania tuna haki na wajibu wa kumkumbusha rais kuwa msingi wa mamlaka ya nchi, rais na serikali ni wananchi na rais na serikali wanawajibika kwa wananchi. Rais hawezi kuwa juu ya Katiba ambayo inatamka mamlaka yake kuwa yanatoka kwa Wananchi. Wananchi ndiyo waajiri wa rais na Serikali. Rais na Serikali wako chini ya mamlaka ya wananchi na siyo kinyume chake. Rais wetu Kikwete anaelewa na kutekeleza hili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom