Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa vs Waziri : Ipi tofauti kati ya "Makambi ya RC Mtaka" na RC Geita kufukuza wanafunzi 11 na kuhamisha Walimu .

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,730
6,273
Mods uzi una maudhui tofauti na nyuzi zilizopita japo nimezitumia kama Mfano.
Nimeweka Link ya Mijadala hiyo Miwili ili kuweka kumbukumbu sawa.
Kuna mada imetrend sana kwenye jamvi letu kuhusu Kauli ya RC wa Dodoma Mh Mtaka akipinga maagizo ya Waziri wa elimu Prof Ndalichako ya kutaka kuondolewa kwa makambi ya ya jioni kwa wanafunzi wa Shule za msingi wanaofanya Mitihani ya taifa mwaka huu. Wengi wamekuwwa wakihoji nani ni Mwenye madaraka katika Ngazi ya mkoa. Imefika pahala inaonekana kama Waziri wa Elimu ni Bosi wa mkuu wa Mkoa. Kiuhalisia hapana, kwani Waziri wa Elimu ni mtu mwenye dhamana ya kutunza na kusimamia sera elimu na mengineyo kitaifa. Mkuu wa Mkoa hawajibiki kwa waziri wa elimu bali Ofisi yake ipo chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI. Hapa tunaweza kusema Administratively ofisi yake ipo chini ya Waziri wa tamisemi lakini KIUTAWALA Mkuu wa Mkoa ana mamlaka makubwa sana ktk Mkoa wake (Mwakilishi wa Rais hapo Mkoani). Ni ngumu sana kwa waziri kutengua agizo la Mkuu wa mkoa Narudia ni Ngumu sana. Fikiria hili neno MKUU WA MKOA yaani kidemokrasia tunashindwa kusema Mwenye Mkoa wake.

Kuthitisha hili tufuatilie tukio la kuungua shule Kwa Moto huko GEITA . Tumeona MKUU WA MKOA GEITA akifanya maamuzi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mkuu wa shule, kufukuza wanafunzi na kuhamisha waalimu pamoja na kutimua walinzi katika shule husika. Bado kuna haja ya kujadili hili?.. anayedahili wanafunzi si ni wizara ya elimu?, anayetengeneza kanuni na makosa ya kujifukuzisha shule si ni wizara ya elimu?. why RC katimua wote na kaagiza kuhamishwa walimu.

TUCHAMBUE MAAGIZO HAYO KWA KINA:

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule ameiagiza bodi ya shule hiyo kuwafukuza wanafunzi 11 waliobainika kuwa na makosa ya jinai.Amesema mbali na hao 11 wapo wengine 24 ambao bodi ya shule imetakiwa kuwapa adhabu ya kurudi nyumbani siku 30.. (Tujiulize Bodi ya shule inaripoti kwa nani?, mbona Mkuu wa mkoa naipa Maagizo magumu na inatekeleza?,Unafikiri waziri wa elimu anaweza kutengua hili? )

“Hawa wanafunzi 11 wamekutwa na makosa ya jinai walikuwa na visu, wana makosa ya kubaka na makosa mengine mengi ya kijinai wapo ambao walishajadiliwa na bodi na shule hawa washtakiwe kwa makosa ya jinai sio tu kufukuzwa shule, “ .. (Hili ni la kiusalama zaidi , so nadhani halitakuwa na mjadala)

Amemtaka katibu tawala wa mkoa kumchukulia hatua za kinidhamu
mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu 13 walioshindwa kuwajibika kwa mambo muhimu na kutaka kuwabadilisha kituo cha kazi ndani ya siku saba.. (Katibu tawala yupo ofisi ya Mkuu wa mkoa na ni katibu wa mkuu wa mkoa, Je Mamlaka za nidhamu za wakuu wa shule Hapo mkoani zipo Kwa mkuu wa Mkoa?, ukisema mkurugenzi wa hlmashauri bado tutarudi palepale TAMISEMI mpaka kwa RC. Je Mkuu wa Mkoa anaweza kubadilisha vituo wa elimu? Sidhani kama Waziri wa Elimu atatengua hili au anaweza kutengua hili.)

Katika hatua nyingine walinzi wa shule hiyo wamefukuzwa kazi kutokana na uchunguzi kubaini hawana mafunzo ya usalama na hawakupitia Jeshi la Akiba la Mgambo. (Hili halina Mjadala kwani ni la kiusalama zaidi, japo wameajiriwa na shule sasa inawezekanaje RC akatoa maagizo kama hana Mamlaka kwenye Shule)

TUNAOBEZA MAMLAKA YA WAKUU WA MIKOA, TUJIFUNZE HAPA KUWA MKUU WA MKOA NDANI YA MKOA WAKE YEYE NDO MWENYE MAMLAKA MAKUBWA YA KIUTAWALA KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE UKIONDOA WALE AMBAO WAMEMZIDI PROTOKALI ZA KIUTAWALA... NARUDIA "KIUTAWALA" NA NADHANI WAPO 4 TU. HAIWEZEKANI MTAWALA ASIWE NA MAMLAKA KULIKO MSIMAMIZI.
RC anaweza kuchukua maafisa na wakuu wa vitengo kwa amri kutoka taasisi yeyote ya wizara yeyote Si TRA, Polisi, Jeshi, TANESCO, Ewura akawaambia twendeni huku tukafanye zoezi hili na wakaenda. Lakini waziri wa elimu au wa mazingira hawezi.

Nyongeza ni mamlaka na nafasi zake zingine kisheria:
(i) Kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa (Katiba 1977, ib. 61(4))
(ii) Kuwa mwenyekiti wa RCC inayotoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali mkoani mwake (RAA No 19/1997).
(iii) Mhimili wa Halmashauri za wilaya (LG Finance Act No 9/1982)
(iv) Mhimili msaidizi wa Halmashauri za Miji iliyoko katika mkoa wake (LG (Urban Authorities) Act No 8/1982)
(v) Kumweka kizuizini kwa saa 48 mfululizo mtu anayehisiwa kuwa ni mhalifu au anayehatarisha hali ya utulivu naamani (Regional Admin Act No 19/1977)
(vi) Kuongoza Kamati ya Mkoa ya maombi ya leseni za magari (Motor Vehicles, Registrations, Acquisitions and Dispositions Act No 5/1972, ib 24(2))
(vii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa inayoshughulikia uteuzi wa vijana wanaojiunga na jeshi la kujenga taifa (National Service Act No 16/1964)
(viii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati yaMkoa inayochambua maombi ya watu wanaotaka kuuza madawa ya sumu (Pharmaceuticals and Poisons Act No 9/1978)
(ix) Kuongoza Kamati ya kusikiliza rufani za leseni za biashara mkoani (Business Licensing Authority Act No 25/1972, ib. 1)
(x) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya leseni za vileo (Intoxicating Liquours Act No 28/1968)
(xi) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya utoaji wa leseni za magari na uchukuzi (Transport Licensing Act No 1/1973)
(xii) Kuteua wakaguzi wa magereza (Prisons Act No 34/1967, ib. 100)
(xiii) Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani kwake ili kuhakikisha kuwa kuna ulinzi na usalama mkoani wakati wote na kuishauri serikali ipasavyo (National Defence Act No 24 1966)
(xiv) Kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi (Witchcraft Ordinance Cap 18)

I stand to be corrected!

huu uzi wako sijauelewa hata kidogo.yaaan hoja yako iko randaml
 
Mkuu wa Mkoa kumuagiza RAS kuhamisha mtumishi ni Sahihi kabisa. RAS ndiye anasimamia utumishi wa uma kimkoa
 
Kwenye masuala ya kisera hali ni tofauti, Waziri ndie mwenye mamlaka.

Mfano SERA ya Elimu ya Msingi inaitaja Tamisemi kama Mratibu, msimamizi na mtekelezaji wa mambo ya Kimitaala na nje ya mtaala. Kupitia TAMISEMI mkoa inawezekanaje Mkuu wa Mkoa asiwe na Mamlaka ilhali anaonekana kama ndo Mkuu wa Tamisemi mkoani
 
Maelezo mareeefu kujaribu kujustfy kauli za utovu wa nidhamu aliouonyesha bwana Mtaka. Kikubwa amepimwa nae ameonekana hafai na tayari ameandikwa Mene mene tekel na Peres
 
Back
Top Bottom