Mamlaka ya maji mkoa wa Morogoro (MORUWASA)-jipu sugu

nyembeason

Member
May 4, 2009
44
21
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye mito isiyopungua 100 isiyokauka kipindi chote cha mwaka. Lakini cha ajabu mji wa Morogoro, chini ya MORUWASA, unakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa maji, maji ya matumizi ya nyumbani. Kuna mitaa mingi sana, mathalani Bigwa, ambayo hukaa kwa muda wa miezi mpaka mitatu bila maji. MORUWASA, bila aibu, kila mwisho wa mwezi hupita na kusoma mita za maji na kuwapa wenye mita bili za majipwalipe-service chaji na gharama za maji-hewa. Hapa nazungumzia mitaa yenye uafadhali, ukiachilia mitaa kama Kihonda ambayo kwao maji ni almasi-hununua kwenye magari, uhaba huu yaelekea hauna jawabu.Ndoo MOJA ya maji, ya lita 20, huuzwa shilingi mia tano za kitanzania.

Huwezi kuwa nchi ya viwanda ikiwa maji yasiyohiyaji akili HAYAPATIKANI-just laying pipes na kusambaza kwa umma/watu!

Nionavyo mimi Shida kubwa kwa taasisi nyingi za umma, ikiwemo MORUWASA, ni: Kuwa na watumishi wengi wasio na uwezo,mizigo, wapiga dili na wanaofanya kazi kwa mazoea na pengine wenye maslahi na uhaba wa huduma za umma (mathalani wana magari ya kuuza maji, wana visima, au huduma fulani zikiwepo kwenye idara za umma wanakosa dili). WENGI PIA HAKUNA UBUNIFU, SOGA TU OFISINI NA kufanya kazi kwa mazoea-BUSINESS AS USUAL, ili mradi mwisho wa mwezi ufike waende kwenye ATM-kula kodi zetu-FOR NOTHING IN TURN

Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paulo Makonda aliwahi kusema kuwa SERIKALI ina wafanyakazi wengi sana wasio na KAZI, MIZIGO. Nafikiri ni wakati muafaka kwa serikali kupitisha fagio la chuma, kubakisha watumishi wenye ueledi, tija na wabunifu, WENYE KUFANYA KAZI, SI KUPOKEA SALARI TU. Kuna mizigo mingi sana kwenye UTUMISHI wa umma. Magu pitia huku-watumishi waliopo, ambao si hewa, lakini hawana tija, mizigo, WAPOKEA SALARI TU BILA KUREJESHA HUDUMA ZENYE TIJA, WELEDI NA ZA WAKATI kwa jamii inayowalipa.
 
Jipu tena limeshaiva, chanzo cha mindu na kibwe toka enzi za mbaraka mwinshee na Salum Abdallah. Siyo wabunifu kbs, naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom