Mamlaka ya Maji Dar es Salaam na tatizo sugu la kupasuka kwa mabomba ya maji

baba lulu

Member
Sep 12, 2015
8
0
Ni miaka sita sasa tangu nianze kuishi Dar es Salaam, wilaya na kata ya Ubungo mtaa wa msewe. Tangu nianze kuishi mtaa huu kila siku mabomba ya maji yanaharibiwa na kusababisha upotevu mkubwa wa maji. Na ha DAWASA wanapokuja kurekebisha kasoro hizo, mabomba hupasuka tena kabla hawajafika makwao.

Najiuliza, hivi tatizo ni kwamba mabomba wanayotumia kurekebisha ni mabovu ama hawana maarifa juu ya kazi ya mabomba ya maji?

Je, ni kweli huwa wanatengeneza kutibu matatizo ama hulipua kazi kwa maksudi ili na kesho warudi ili wapate posho?

Ukipita mtaani njia hazipitiki, zimejaa maji na matope yanayotiririka hovyo mtaani.
Nini kinapekekea hali hii?

Wahusika naomba muwe mnapita huku ili msolve tatizo.
 
Back
Top Bottom