Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) hamuwatendei haki waonyeshaji/wafanyabiashara kwa kuchelewa kufungua mabanda

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,824
9,521
Tangu maonesho ya 2021 SabaSaba yaanze hapa Kilwa Road Dar es salaam hapa kwenye Banda la Karume wafanyakazi wa TANTRADE wanachelewa sana kufungua mabanda/Maholi makubwa wanafungua saa nne au saa tatu na dakika zilizozosonga sana.

MADHARA YA KUCHELEWA KUFUNGUA
  • Waonyeshaji wanakosa muda wa kutosha kuandaa mabanda yao
  • Ni usumbufu mkubwa kwa waonyeshaji ikizingatiwa kuwa waonyeshaji wengi wanafika kwenye mabanda mapema sana
  • Mamlaka inawapora waonyeshaji muda wao stahiki wa kuanza maonesho ikizingatiwa kuwa muda wenyewe ni mchache yaani saa 4 asubuhi hadi saa 12
MAPENDEKEZO
  • Kama issue ni usalama kwa ambao hawajafika tafuteni modality nzuri ya kuhakikisha angalau saa 3 asubuhi watu wanaingia kwenye mabanda yao ili kuanza kuonyesha
  • Imarisheni ulinzi ndani ya mabanda wakati wa asubuhi kulinda assets za wale ambao bado hawajafika. Kazi hii vijana wa Skauti mlio nao wanaweza kuifanya vizuri.
Ukweli ni kwamba waoneshaji wengi hasa wa Kimataifa wanalalamika sana kwa tabia hii ya wafanyakazi wenu kuchelewa kufungua mabanda makubwa ya pamoja. Ukweli ni kwamba INAUDHI na INAKERA. Jirekebisheni or else mnaathiri maonesho haya yaliyojijengea sifa.

PIA Rekebisheni miundombinu kwa kweli imechakaa sana kuanzia mabanda makubwa, toilets na hata walk ways...hivi ni kweli kwamba TANTRADE kwa kushirikiana na WIZARA hamuwezi kupiga Pavers kwenye Walkways zote za humu uwanjani? vumbi linachafua bidhaa za waoneshaji na kupunguza ubora...uwanja huu ni tunu katika kukuza BIASHARA hapa nchini...Tafadhali rekebisheni. TUNAONA.

20210707_095959.jpg
 
Pichani ni Wafanyabiashara waonyeshaji wakiwa wanasubiri Banda la Karume lifunguliwe leo siku ya SabaSaba 2021 Banda limefunguliwa saa Nne na Dakika Mbili asubuhi...Usafi ufanyike saa ngapi bidhaa zipangwe saa ngapi...TANTRADE mnapotezea muda wafanyabiashara jirekebisheniii
 
20210707_095959.jpg
Baada ya wafanyabiashara kusubiri kwa zaidi ya saa moja sasa huyu mzee na hao vijana wake wa skauti ndo wanakuja kufungua Holi saa Nne na dakika zake asubuhi...Watu wanaudhika sana...mimi kama mmoja wa waoneshaji nawaambia feeling ya exhibitors
 
Kwanini Banda la mali asili na utalii kwenda kuona wanyama wanatoa tozo ya 1,000/= (Wakubwa) na 500/=(watoto) wakati getini ushalipia?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom