Mamlaka ya Jeshi la Polisi juu ya vyombo vya habari kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari (2016)

Mamlaka mbalimbali zimepewa madaraka kubwa katika kudhibiti maudhui na shughuli za kila siku za vyombo vya habari. Nguvu hizo, hasa kwa vyombo binafsi vya habari, zinaingilia uhuru wao wa uhariri na hivyo kuathiri kwa upana uhuru wa vyombo vya habari, kutoa maoni na kujieleza.

Mamlaka ya Polisi

Jeshi la Polisi limepewa mamlaka pana ya kufanya upekuzi kwenye chombo cha habari na kukamata kifaa chochote kilichoanzishwa, kuwekwa, au kuendeshwa kwa kukiuka matakwa ya Sheria hii. [Kifungu cha 60]

Vifaa vinavyotumika kuchapisha,kuzalisha au kuandaa habari havitoshikiliwa hadi tu pale ambapo askari anaona kuwa kuendelea kufanya kazi kwa kifaa husika kutazuia au kuharibu mchakato wa upelelezi

Upekuzi na ukamataji huo utazingaia Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai au sheria nyingine zinazosimamia masuala ya upekuzi na ukamataji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom