Mamlaka ya Hali ya Hewa yatahadharisha uwepo wa mvua kubwa ukanda wa Pwani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
WhatsApp Image 2017-04-27 at 17.54.46.jpeg
 
Mmh! Kwa jua hili la leo Dar. sijui ngoja tusubiri kesho, 28.04.2017
 
Mmh! Kwa jua hili la leo Dar. sijui ngoja tusubiri kesho, 29.04.2017
Ninachojua hawa jamaa huwa wanaendeshwa kwa matukio..Wakiona kamvua kameanza kunyesha huwa wanaanza kutabiri.
Wakitaka kunishawishi watabiri kama mwezi mmoja kabla na walichotabiri kitokee kweli, hapo tutaenda sawa
 
Mamlaka ya hali ya hewa wanatoa utabiri Wa Massa 24, utabiri Wa mwezi mmoja na utabiri Wa msimu. Jaribu kutumia taarifa zao kamwe hutajuta
 
MVUA.jpg

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari kwa umma kuhusu vipindi vya mvua kubwa vinavyoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa katika mwambao wa ukanda wa pwani.

Katika taarifa yake ya jana saa 11:15 jioni, TMA imetoa tahadhari kuwa, kuanzia leo hadi keshokutwa kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinavyoambatana na upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.

Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.

“Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika Bahari ya Hindi eneo la kisiwa cha Madagascar, hivyo kusababisha upepo mkali katika pwani ya Tanzania,” imesema taarifa hiyo.

TMA imewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki na kwamba, inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa mrejesho kila itakapobidi.
 
Ngoja nijitafutie kipozeo mapemaaaaaa, maaana hapa itakuja mvua na ubaridi, kulala peke itakuwa shida.
 
Haya ndugu zetu wa mabondeni ondokeni mapema serikali ndo imesha sema mchukue tahadhali mapema
 
Nawaombea Angalau wawe wamepatia Kwani hii aibu wataibeba na nani
Mpaka muda huu hujajua kuwa wamepatia? Mitaa yangu mvua imenyesha tangu saa saba usiku imepugua saa mbili asubuhi. Na kuna kila dalili itarudi tena.
 
Back
Top Bottom