Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) yatahadharisha ujio wa mvua kubwa kwa siku tano kwa mikoa ya pwani

Huu ni msimu wa mvua Dar...mie natabiri wiki ijayo itanyesha mvua Alhamis au Ijumaa
 
Mimi huwa siwaamini mpaka nijionee mwenyewe. Hata hivyo mwaka huu mvua zimechelewa.
 
Kwa nini kila TMA wakitoa utabiri lazima uwe wa siku 5? Haujawahi kuwa siku 3 , 4,7,11 au 14 kwa nini? Hali ya hewa haiwezi kuwa so precise, kuna usanii hapa.
Kwahiyo unawafundisha kazi? Basi anza na wewe kutoa utabiri wa siku 3.
 
Angalao wamejaribu kuliko hata Wizara ya Afya ambayo imebatizwa Wizara ya Nyungu
 
Kwa nini kila TMA wakitoa utabiri lazima uwe wa siku 5? Haujawahi kuwa siku 3 , 4,7,11 au 14 kwa nini? Hali ya hewa haiwezi kuwa so precise, kuna usanii hapa.
Hahahaaa mkuu una lako jambo. Kiutaalamu na mara nyingi huwa inakuwa hivyo utabiri unagawanyika kwa msimu, siku kumi, siku tano na siku moja huku mkipewa taarifa za matukio ya kujiandaa kadri muda wa tukio unavyokaribia!
 
Na pia mvua zikishaanza ndio na utabiri unafata, utabiri huwa hauji kabla ya mvua.... maajabu mengine haya.
Kuna mtu aliwahi kufanya utafiti na akaja na majawabu ya maswali y majibu yake kwamba wanawake wapo katika uwezo mkubwa wa kupata mimba kuliko wanaume endapo watajihusisha na masuala ya ngono
 
Mvua.PNG

Hapo kwenye Athari zinazoweza kujitokea wamefumbafumba wanasema "ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji" wanaogopa kusema kutakuwa na mafuriko Jangwani Dar
 
Kuna movie moja inaitwa sometime in april,basi bwana inavyoanza kumbu kumbu kuwa ni matonye ya mvua.
Basi kila mwaka naona ni ukumbushi kila ukifika mwezi huu na mvua mvua hii.
 
Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) imetoa tahadhari ya matarajio ya hali mbaya ya hewa itakayoambatana na mvua kubwa kwa siku tano.

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Mtwara, Lindi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba mvua hiyo huenda ikaathiri shughuli za uvuvi na usafirishaji.

Huu utabiri wao unaanza kazi lini?
 
Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) imetoa tahadhari ya matarajio ya hali mbaya ya hewa itakayoambatana na mvua kubwa kwa siku tano.

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Mtwara, Lindi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba mvua hiyo huenda ikaathiri shughuli za uvuvi na usafirishaji.

Huyu Mungu wa mamlaka ya hali ya hewa ni Mungu wa ajabu, kila tukitangaziwa huwa ni siku tano! Tano! Tano! Na cha ajabu huwa ahadi haitimii!
 
Back
Top Bottom