Mamlaka Ya Hali Ya Hewa nchini na utabiri wa kubahatisha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka Ya Hali Ya Hewa nchini na utabiri wa kubahatisha.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikivembu, Mar 25, 2011.

 1. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Rais Jakaya Kikwete leo katika ziara yake ya kutembelea wizara mbalimbali,alitembelea wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi.Wizara hii ina sector nyeti kama viwanja vya ndege,Reli,Mamlaka ya Usafiri wa Anga na Mamlaka ya hali ya hali ya hewa.Leo amemwagiza Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa kuwa ampelekee mahitaji muhimu ili isitoe utabiri wa kubahatisha.Mawazo yangu ni hapa,ina maana hajui kama mamlaka hiyo ina upungufu mkubwa wa vitendea kazi?Huhitaji kuenda ndani zaid ya hapo kwani ukitazama tu utabiri wao katika televisheni utagundua upo tofaut na ule wa nchi zingine tunaouona katika televisheni kubwa kama CNN na BBC.Utabiri wa hapa nchini unafanyika kwa saa 24 tu kitu ambacho kinaleta tatizo kubwa la kuaminika katika utabiri wao.Wanarekodi toka saa tisa mchana na kutangazwa saa tatu usiku.Kuna walakini hapo.

  Matukio yote ya hapa katikati huwezi kuyapata.Hata ukifungua katika website yao utaona jinsi wanavyobahatisha taarifa zao.Huwezi kuapata utabiri uliokamilika.Mfano utakuta wanakutangazia kiwango cha mvua kilichonyesha katika mkoa fulani labada ni 23mm.Lakini uhalisia wa mvua iliyonyesha mahali hapo ni tofauti.Wao wanadai eti ni lazima mvua hiyo ipimwe kwenye eneo waliloweka rain gauge yao,kama mvua haikufika eneo hilo hata kama itanyesha ya mafuriko basi wao hawataripoti.Hapa sasa kuna udhaifu.

  Kumbe hawa jamaa wanahitaji kuwa na rain gauge nyingi katika distance ndogo na si kama wanavyofanya sasa mvua kupimwa zaid ya kilometa 300,toka ilipo rain gauge moja.Wasaidie.Lakini pili hata elimu yao nayo ina utata.Hebu tazama chuo wanachosoma kule Kigoma hata hakijasajiriwa toka mwaka 1983.wafanyakazi wao hawapimwa kwa madaraja.Mwisho wa siku wanaambiwa tu umefaulu.Kwa kiwango gani huhitaji kujua.Imarisha na chuo hicho basi ndugu Kikwete.
   
Loading...