Mamlaka Ya Bandari Tuhumiwa Haina Utashi Kuwashughulikia Mawakala Inaowatuhumu

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Kufuatia tuhuma za wizi mkubwa unaohusisha kutafunwa malipo ya tozo za matumizi ya bandari kwa kipindi kirefu.Baada ya maagizo ya Waziri Mkuu yaliotokana na kuibuliwa kwa kashfa kubwa sana ya upotevu wa mapato lukuki ya umma,Mamlaka ya Bandari kupitia Meneja wa Bandari wamechukua hatua kadhaa kuhakiki na kujaribu kuokoa mapato yaliofujwa kiujanja kwa ushirikiano wa wafanyakazi wasio waaminifu wa Mamlaka ya Bandari,Benki na baadhi ya kampuni ya uwakala wa forodha.

Hatua ambazo zimekuwa zikichuliwa zikihusisha matumizi ya nguvu kubwa,vitisho ,ukiukwaji wa misingi ya haki,ubabe { kuwalazimisha mawakala kulipa kwa mara nyingine gharama walizokwisha lipia na kufanikiwa kutoa mizigo} n.k dhidi ya mawakala zinagubikwa na walakini kiuadirifu ,kimkakati ,kiutekelezaji na matokeo tarajiwa. sababu kubwa ikiwa ni ya utuhumiwa wa mamlaka husika {wafanyakazi waandamizi,mifumo ya mamlaka kiusimamizi wa mapato na udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka bandarini kwenda kwa wateja,ICD's,CFS...Hivyo Mamlaka kugeuka polisi,mahakama na magereza kwa inaowatuhumu.

Kimsingi mizigo ndani ya makasha {containers} inayotuhumiwa kuibwa haikuibwa bali ilitolewa kwa kufuata taratibu kwa kuhusisha wadau {TRA,Mawakala wa Meli} husika ktk mchakato yakinifu .Kimsingi mizigo ilitolewa katika bandari na mawakala kwa kufuata taratibu zote zinazopaswa kufuatwa likiwemo la malipo na uhakiki wa malipo ya husika kufanywa na idara za bandari .

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo wizi na ufujaji wa malipo uliratibiwa kwa ustadi mkubwa na maafisa waaminiwa wa bandari {Accounts,IT,Operations} kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Benki zenye kandarasi ya kukusanya makusanyo ya tozo ,Mathalani upo mfano wa wakala alielipa kwa hundi na mhamala wa fedha kuonyesha fedha imetoka kwenda Mamlaka ya Bandari lakini baadae kuonyesha walipiwa kuwa wateja wengine na si alietoa hundi husika.Pili,Upo ushahidi pia wa ankara moja kufanyiwa malipo zaidi ya mara moja kwa viwango tofauti na pesa kufujwa.

Leo kwa ajili ya kukwepa ghadhabu ya dola yenye nguvu mamlaka inalazimisha ilipwe tena gharama za tozo kwa kuwafungia baadhi ya mawakala na kutishia kuwafungia wengine wengi wakikaidi kulipa tena..Lakini pia mamlaka haitaki kufanya uhakiki shirikishi wa nyaraka zihusuzo ushahidi wa malipo ya tozo husika wakati wa utoaji wa mizigo husika kwa kusingizia kwamba nyaraka zinazowakirishwa na mawakala ni batili na za kugushi {swali:waliwezaje kuruhusu mizigo ya thamani kubwa ikatoka bandarini kwa kutumia nyaraka za kughushi?Je nyaraka mwambata za Mamlaka ya mapato pia za kughushi? Nini weredi wa wafanyakazi wa uhakiki ?}.
 
Kuna dalili kuwa bandarini na TRA kuna mambo makubwa kuliko yaliyoibuliwa mpaka sasa
 
Back
Top Bottom