Nyanje
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 494
- 375
- Thread starter
- #141
Mkuu Bado nasimamia nilichokueleza jambo ambalo pengine linaweza kufanywa na baadhi ya askari wachache haliwezi kuwa ni mpango wa jeshi.Mkuu siku nilipocomment hapa uliniona nakutoa kwenye mada:- haya ndo maelezo ya polisi Kwa niaba ya gazeti la mwananchi:- soma Kwa makini ujifunze kitu.
By Waandishi Wetu
More by this Author
Dodoma. Siku moja baada ya Gazeti la Mwananchi kuripoti kutoweka kwa ofisa wa Polisi aliyekuwa mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mji wa Kiserikali Mtumba, Emmanuel Govela, Jeshi la Polisi limesema linamtafuta ofisa huyo, huku mama yake mzazi akisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na jeshi hilo.
Govela (39) tangu apoteze mawasiliano na ndugu zake Juni 26, 2021, bado hajulikani aliko, licha ya jitihada za kumtafuta za ndugu zake na Jeshi la Polisi.
Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, mama mzazi wa Govela, Monica Maluli alisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na polisi kumtafuta mwanawe kutokana na kauli alizoambiwa.
Monica, anayeishi Kijiji cha Mtera alisema wadogo zake na ofisa huyo (Govela) walikwenda polisi ikiwa ni siku ya 29 tangu walipokosa mawasiliano naye, wakaambiwa hata wao walikuwa wanamtafuta.
Alisema baada ya mjadala waliangalia simu ya mwanawe na kukuta ilifanya mawasiliano ya mwisho na polisi (anataja jina), lakini anashangaa kwa nini mhusika haulizwi.
Soma zaidi hapa: Ndugu walia askari polisi kutoweka siku 41
ADVERTISEMENT
“Mwanangu sijamuona, lakini mambo mawili yananiumiza sipati majibu, moja wadogo zake walikuta sare alizozitumia wakati anavishwa nyota ya pili. Hajatumikia cheo hicho. Lakini, hadi wanangu wanawasha simu kuna polisi alimpigia Emma mwezi wa sita tarehe 26 jioni ndio ikawa mwisho,” alisema mama huyo kwa uchungu.
Monica alisema ana mambo mengi moyoni, lakini ni ngumu kuyasema mapema. Alidai kauli ya mwisho waliambiwa na polisi (anamtaja jina) kwamba wamemtafuta wameshindwa, hivyo ndugu nao wasaidie.
Polisi wazungumza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema taarifa rasmi itatolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini.
Mwananchi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ambaye alijibu kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
“Mkaguzi (Govela) ambaye imedaiwa haonekani na wala hakuna anayejua alipo na haijulikani nini kilichomsibu hadi sasa, Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi. Taarifa zimesambazwa mikoa mbalimbali kama ilivyo taratibu za kumtafuta mtu aliyetoweka/potea bila taarifa zozote,” alisema Misime.
Misime alisema taratibu za kiuchunguzi nazo zinaendelea na Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu mwenye taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa mkaguzi huyo, asisite kuwasiliana na kituo chochote cha polisi au kiongozi yeyote.
Tangazo latolewa kanisani
Mwananchi liliwasiliana pia na diwani wa Mtera jana, eneo ambalo ni nyumbani kwao Govela aliyesema tangazo la kutoweka kwa polisi huyo lilitangazwa kanisani.
Diwani huyo, Zawadi Maulya alisema akiwa kanisani kwenye ibada alisikia tangazo la kupotea kwa askari polisi huyo na baadaye alielezwa mkasa mzima. “Leo (jana) ndiyo nimepata ukweli, watu walizungumzia jambo hilo baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari (Mwananchi), kuwa ni mtoto wa mama Yuda ambaye namfahamu vizuri,” alisema Maulya.
Alisema anaifahamu familia ya askari huyo na hasa mama yake mzazi kuwa ni mcha Mungu, ingawa tabia na mienendo ya askari hawezi kuifahamu kwa kuwa ni muda mrefu tangu atoke kijijini