Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

Mkuu siku nilipocomment hapa uliniona nakutoa kwenye mada:- haya ndo maelezo ya polisi Kwa niaba ya gazeti la mwananchi:- soma Kwa makini ujifunze kitu.
By Waandishi Wetu
More by this Author

Dodoma. Siku moja baada ya Gazeti la Mwananchi kuripoti kutoweka kwa ofisa wa Polisi aliyekuwa mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mji wa Kiserikali Mtumba, Emmanuel Govela, Jeshi la Polisi limesema linamtafuta ofisa huyo, huku mama yake mzazi akisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na jeshi hilo.

Govela (39) tangu apoteze mawasiliano na ndugu zake Juni 26, 2021, bado hajulikani aliko, licha ya jitihada za kumtafuta za ndugu zake na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, mama mzazi wa Govela, Monica Maluli alisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na polisi kumtafuta mwanawe kutokana na kauli alizoambiwa.

Monica, anayeishi Kijiji cha Mtera alisema wadogo zake na ofisa huyo (Govela) walikwenda polisi ikiwa ni siku ya 29 tangu walipokosa mawasiliano naye, wakaambiwa hata wao walikuwa wanamtafuta.

Alisema baada ya mjadala waliangalia simu ya mwanawe na kukuta ilifanya mawasiliano ya mwisho na polisi (anataja jina), lakini anashangaa kwa nini mhusika haulizwi.

Soma zaidi hapa: Ndugu walia askari polisi kutoweka siku 41

ADVERTISEMENT

“Mwanangu sijamuona, lakini mambo mawili yananiumiza sipati majibu, moja wadogo zake walikuta sare alizozitumia wakati anavishwa nyota ya pili. Hajatumikia cheo hicho. Lakini, hadi wanangu wanawasha simu kuna polisi alimpigia Emma mwezi wa sita tarehe 26 jioni ndio ikawa mwisho,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Monica alisema ana mambo mengi moyoni, lakini ni ngumu kuyasema mapema. Alidai kauli ya mwisho waliambiwa na polisi (anamtaja jina) kwamba wamemtafuta wameshindwa, hivyo ndugu nao wasaidie.

Polisi wazungumza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema taarifa rasmi itatolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini.

Mwananchi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ambaye alijibu kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Mkaguzi (Govela) ambaye imedaiwa haonekani na wala hakuna anayejua alipo na haijulikani nini kilichomsibu hadi sasa, Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi. Taarifa zimesambazwa mikoa mbalimbali kama ilivyo taratibu za kumtafuta mtu aliyetoweka/potea bila taarifa zozote,” alisema Misime.

Misime alisema taratibu za kiuchunguzi nazo zinaendelea na Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu mwenye taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa mkaguzi huyo, asisite kuwasiliana na kituo chochote cha polisi au kiongozi yeyote.

Tangazo latolewa kanisani

Mwananchi liliwasiliana pia na diwani wa Mtera jana, eneo ambalo ni nyumbani kwao Govela aliyesema tangazo la kutoweka kwa polisi huyo lilitangazwa kanisani.

Diwani huyo, Zawadi Maulya alisema akiwa kanisani kwenye ibada alisikia tangazo la kupotea kwa askari polisi huyo na baadaye alielezwa mkasa mzima. “Leo (jana) ndiyo nimepata ukweli, watu walizungumzia jambo hilo baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari (Mwananchi), kuwa ni mtoto wa mama Yuda ambaye namfahamu vizuri,” alisema Maulya.

Alisema anaifahamu familia ya askari huyo na hasa mama yake mzazi kuwa ni mcha Mungu, ingawa tabia na mienendo ya askari hawezi kuifahamu kwa kuwa ni muda mrefu tangu atoke kijijini
Mkuu Bado nasimamia nilichokueleza jambo ambalo pengine linaweza kufanywa na baadhi ya askari wachache haliwezi kuwa ni mpango wa jeshi.
 
Mpuuzi wa kiwango cha lami wewe unataka unataka nikuambie alipo wakati ndg zake wapo? Umerusha mada humu Jf members tumtafute? Polisi wenzie hawajui alipo kwanza naomba kujua jinsia yako maana inawezekana ni hawara yako kakukopa nenda chukua gwanda zake vaa kaweke barrier pale Maria de mathias uvune, acha shobo
Mkuu kwa vyovyote wewe ni pumbavu to the highest level,huna Cha kuchangia ZAIDI ya chuki pimbi!!!
 
Haieleweki ndugu yangu kwanza Sisi majirani tuliowengi miezi yote hatukuweza kujua kama jamaa ni askari mpaka ulipovunjwa mlango wake na kukuta uniform Tena alikuwa na nyota Mbili wenzake walisema alikuwa mkuu wa kituo cha mtumba mji wa kiserikali nafkiri hakutaka watu wamjue kama ni askari.
Askari kupotea/ kufa sawa tu. Wale ni binadamu washenzi na wapuuzi sana
 
Mpuuzi wa kiwango cha lami wewe unataka unataka nikuambie alipo wakati ndg zake wapo? Umerusha mada humu Jf members tumtafute? Polisi wenzie hawajui alipo kwanza naomba kujua jinsia yako maana inawezekana ni hawara yako kakukopa nenda chukua gwanda zake vaa kaweke barrier pale Maria de mathias uvune, acha shobo
Jinga kweli aliyekuomba umtafute nani?
 
Jinga kweli aliyekuomba umtafute nani?
Mimi Kuna sehemu nimezungumzia kumtafuta insp? Aliyeleta Uzi ww kumtafuta niwe Mimi? Umeshindwa kumtafuta Dom na viunga vyake kwa haraka unaleta Jf alafu unabwatuka kumbe ww zwazwa tu, huna vyanzo vya maana vya kumpata, acha vyombo vya uchunguzi vifanye yao
 
Kama huna la kuchangia si upige kimya umbwa wewe
 
Ukifuatilia kwa umakini stori hii eneo la kuanza kufuatilia kupotea kwa huyo askari ni Yale mawasiliano yake ya mwisho yaani tarehe 25 June na 26 haijalishi hata kama ni askari wenzie.
 
Kuna stori za vijiwe vya kahawa zinasema labda watumie mbwa maalumu kufuatilia harufu yake.
 
Ukifuatilia kwa umakini stori hii eneo la kuanza kufuatilia kupotea kwa huyo askari ni Yale mawasiliano yake ya mwisho yaani tarehe 25 June na 26 haijalishi hata kama ni askari wenzie.
Nilimuona tbc kamanda wa dodoma anasema wao watambua kama mtoro nikasema dodoma hawana kamanda.
 
Hakika huyu inspector hajapatikana mpaka leo huu ni mwezi wa tano anaelekea mwezi wa sita,nilimuona mama yake amalia muda wote anasema angalau hata waje waitupe maiti ya mwanae nje ya nyumba yake usiku amzike mwanae.dah maneno ya kukata tamaa!!
 
Mkuu siku nilipocomment hapa uliniona nakutoa kwenye mada:- haya ndo maelezo ya polisi Kwa niaba ya gazeti la mwananchi:- soma Kwa makini ujifunze kitu.
By Waandishi Wetu
More by this Author

Dodoma. Siku moja baada ya Gazeti la Mwananchi kuripoti kutoweka kwa ofisa wa Polisi aliyekuwa mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mji wa Kiserikali Mtumba, Emmanuel Govela, Jeshi la Polisi limesema linamtafuta ofisa huyo, huku mama yake mzazi akisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na jeshi hilo.

Govela (39) tangu apoteze mawasiliano na ndugu zake Juni 26, 2021, bado hajulikani aliko, licha ya jitihada za kumtafuta za ndugu zake na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, mama mzazi wa Govela, Monica Maluli alisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na polisi kumtafuta mwanawe kutokana na kauli alizoambiwa.

Monica, anayeishi Kijiji cha Mtera alisema wadogo zake na ofisa huyo (Govela) walikwenda polisi ikiwa ni siku ya 29 tangu walipokosa mawasiliano naye, wakaambiwa hata wao walikuwa wanamtafuta.

Alisema baada ya mjadala waliangalia simu ya mwanawe na kukuta ilifanya mawasiliano ya mwisho na polisi (anataja jina), lakini anashangaa kwa nini mhusika haulizwi.

Soma zaidi hapa: Ndugu walia askari polisi kutoweka siku 41

ADVERTISEMENT

“Mwanangu sijamuona, lakini mambo mawili yananiumiza sipati majibu, moja wadogo zake walikuta sare alizozitumia wakati anavishwa nyota ya pili. Hajatumikia cheo hicho. Lakini, hadi wanangu wanawasha simu kuna polisi alimpigia Emma mwezi wa sita tarehe 26 jioni ndio ikawa mwisho,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Monica alisema ana mambo mengi moyoni, lakini ni ngumu kuyasema mapema. Alidai kauli ya mwisho waliambiwa na polisi (anamtaja jina) kwamba wamemtafuta wameshindwa, hivyo ndugu nao wasaidie.

Polisi wazungumza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema taarifa rasmi itatolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini.

Mwananchi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ambaye alijibu kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Mkaguzi (Govela) ambaye imedaiwa haonekani na wala hakuna anayejua alipo na haijulikani nini kilichomsibu hadi sasa, Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi. Taarifa zimesambazwa mikoa mbalimbali kama ilivyo taratibu za kumtafuta mtu aliyetoweka/potea bila taarifa zozote,” alisema Misime.

Misime alisema taratibu za kiuchunguzi nazo zinaendelea na Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu mwenye taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa mkaguzi huyo, asisite kuwasiliana na kituo chochote cha polisi au kiongozi yeyote.

Tangazo latolewa kanisani

Mwananchi liliwasiliana pia na diwani wa Mtera jana, eneo ambalo ni nyumbani kwao Govela aliyesema tangazo la kutoweka kwa polisi huyo lilitangazwa kanisani.

Diwani huyo, Zawadi Maulya alisema akiwa kanisani kwenye ibada alisikia tangazo la kupotea kwa askari polisi huyo na baadaye alielezwa mkasa mzima. “Leo (jana) ndiyo nimepata ukweli, watu walizungumzia jambo hilo baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari (Mwananchi), kuwa ni mtoto wa mama Yuda ambaye namfahamu vizuri,” alisema Maulya.

Alisema anaifahamu familia ya askari huyo na hasa mama yake mzazi kuwa ni mcha Mungu, ingawa tabia na mienendo ya askari hawezi kuifahamu kwa kuwa ni muda mrefu tangu atoke kijijini
Huyo polisi aliyewasiliana nae mara ya mwisho, akiulizwa anajibu nini?
 
Back
Top Bottom