Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

Mmmh! Askari Tena afisa mwenye nyota Mbili anapotea mpaka ndugu wanagundua ZAIDI ya wiki 3 wenzie hawajui?!!!! Basi uchunguzi uanzie hapo kwenye kituo chake Cha kazi kituo Cha kati dodoma.
Itakuwa alikuwa likizo, tofauti na hivyo si rahisi taarifa kutokuwa wazi......
 
Mimi siyo msemaji wa familia ya afwandre riinsipekita naona umekosea kuni quote jaribu siku nyingine nikiwa full wanzuki nitakujibu
Mkuu kwa vyovyote wewe ni pumbavu to the highest level,huna Cha kuchangia ZAIDI ya chuki pimbi!!!
 
Umasikini ndio laana kubwa,wekeza nguvu huko kuuondoa.

Mungu alivyo wa ajabu,mwanao wa kike ataolewa na polisi,na ndiye pekee atakuwa anakutunza.
Hata YEYE anaweza kuolewa na polisi.
 
Huyo ni undercover agent wa CIA alipewa kazi sasa ile job description ame ignore ,kinachofuata huwa kama Dr shika vile alipoponea chupuchupu ,na ukipona lazima uwe mafia to the highest and topest
Story za vijiwe vya kahawa
 
Mungu amsaidie huko aliko sijui kakumbana na dhahma gani..lakin naona kuna maajabu hapo simu iwe hewan kwa siku zaid ya kumi tena hadi wasap? Au kuna alikua na hiyo simu alikua anasikilizia? Hiyo simu haikua na paswd? Kuna ujumbe wowote unaonyesha alichat kwa hizo siku?
Mkuu mala ya mwisho simu kuwa hewani ilikuwa juni26 tangu juni27 simu yake haikupatikana mpaka walipokuja ndugu zake julai20 na kukuta simu ipo ndani ya chumba chake ikiwa na line zake zote pamoja na pochi ikiwa na fedha kadi ya benki na vitambulisho vyake vyote kwahiyo simu yake ilikuwa imezima yaani haina chaji lol.
 
Mh rais nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupa Afya njema na kuweza kutekeleza vyema majukumu yako ya kitaifa,mh rais Nina ombi maalum kwako kama mwananchi wako ambaye nimeguswa Sana na tukio la kupotea kwa askari polisi Emmanuelle Govella wa kituo kidogo cha mtumba mji wa kiserikali hapa Dodoma.

Mimi ni jirani hapa Nkuhungu Dodoma na Nyumba ambayo polisi huyu alikuwa amepanga siku ambayo ndugu wa huyo polisi walifika na polisi wa kituo Cha kati dodoma kuvunja mlango ili kujua kwanini askari huyo hapatikani muda mrefu nilikuwepo karibu.

Ilikuwa kati ya tarehe 19| 20 mwezi huu wa saba baada ya kuingia ndani walikuta simu ikiwa na laini zake zote Mbili lakini pia walikuta wallet yake ikiwa na vitambulisho vyake vyote mpaka kadi ya benki pamoja na fedha tasrimu sikujua kiasi gani, namba yake 0768243998 inaonyesha alikuwa hewani mala mwisho ni tarehe 26june hata ukiangalia WhatsApp inaonyesha hivyo mpaka siku wanabomoa kwake zilisha pita siku 24 Sasa Kuna maswali najiuliza ni kweli kwamba askari anapotea ZAIDI ya wiki 3 bila wenzake kujua?

Ombi langu kwako MH RAIS uunde kikosi maalum kichunguze upoteaji wa askari huyu Emmanuel govella Mpaka Leo hii nakutumia maombi haya ni takribani mwezi mmoja na siku 5 askari huyu hajaonekana ,nakutakia majukumu mema na Mwenyezi Mungu akutangulie.
Kuna MTT amepotea hapa Napo iunde time ichunguze why upotevu wa mtt.
 
Mkuu mala ya mwisho simu kuwa hewani ilikuwa juni26 tangu juni27 simu yake haikupatikana mpaka walipokuja ndugu zake julai20 na kukuta simu ipo ndani ya chumba chake ikiwa na line zake zote pamoja na pochi ikiwa na fedha kadi ya benki na vitambulisho vyake vyote kwahiyo simu yake ilikuwa imezima yaani haina chaji lol.
Ooh!! Sawa nimeelewa! Any update? Polis wamesema lolote? Ndugu kuna dalili za kumpata?
 
Kwahiyo inawezekana alitekwa ghafla, kwanini aache simu, pesa na vitambulisho? Waangalie simu yake mara ya mwisho aliwasilina na nani..
 
Kwahiyo inawezekana alitekwa ghafla, kwanini aache simu, pesa na vitambulisho? Waangalie simu yake mara ya mwisho aliwasilina na nani..
Mdogo wake alisema walipoiwasha simu yake ilionyesha siku ya mwisho hiyo tar 26 Juni aliongea na mtu mmoja tu askari mwenzake hakuna simu nyingine iliyoingia Wala kutoka,hii habari inatembea gazeti la mwananchi
 
Mdogo wake alisema walipoiwasha simu yake ilionyesha siku ya mwisho hiyo tar 26 Juni aliongea na mtu mmoja tu askari mwenzake hakuna simu nyingine iliyoingia Wala kutoka,hii habari inatembea gazeti la mwananchi
Si mchezo! Kwasiku aliongea na mtu mmoja tu? Inamaana hata hata mpenzi?
 
Usitutoe kwenye njia hakuna system inayofanya kazi kienyeji kwa kiwango hicho mkuu.
Mkuu siku nilipocomment hapa uliniona nakutoa kwenye mada:- haya ndo maelezo ya polisi Kwa niaba ya gazeti la mwananchi:- soma Kwa makini ujifunze kitu.
By Waandishi Wetu
More by this Author

Dodoma. Siku moja baada ya Gazeti la Mwananchi kuripoti kutoweka kwa ofisa wa Polisi aliyekuwa mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mji wa Kiserikali Mtumba, Emmanuel Govela, Jeshi la Polisi limesema linamtafuta ofisa huyo, huku mama yake mzazi akisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na jeshi hilo.

Govela (39) tangu apoteze mawasiliano na ndugu zake Juni 26, 2021, bado hajulikani aliko, licha ya jitihada za kumtafuta za ndugu zake na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, mama mzazi wa Govela, Monica Maluli alisema amepoteza tumaini la kusaidiwa na polisi kumtafuta mwanawe kutokana na kauli alizoambiwa.

Monica, anayeishi Kijiji cha Mtera alisema wadogo zake na ofisa huyo (Govela) walikwenda polisi ikiwa ni siku ya 29 tangu walipokosa mawasiliano naye, wakaambiwa hata wao walikuwa wanamtafuta.

Alisema baada ya mjadala waliangalia simu ya mwanawe na kukuta ilifanya mawasiliano ya mwisho na polisi (anataja jina), lakini anashangaa kwa nini mhusika haulizwi.

Soma zaidi hapa: Ndugu walia askari polisi kutoweka siku 41

ADVERTISEMENT

“Mwanangu sijamuona, lakini mambo mawili yananiumiza sipati majibu, moja wadogo zake walikuta sare alizozitumia wakati anavishwa nyota ya pili. Hajatumikia cheo hicho. Lakini, hadi wanangu wanawasha simu kuna polisi alimpigia Emma mwezi wa sita tarehe 26 jioni ndio ikawa mwisho,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Monica alisema ana mambo mengi moyoni, lakini ni ngumu kuyasema mapema. Alidai kauli ya mwisho waliambiwa na polisi (anamtaja jina) kwamba wamemtafuta wameshindwa, hivyo ndugu nao wasaidie.

Polisi wazungumza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema taarifa rasmi itatolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini.

Mwananchi lilimtafuta Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ambaye alijibu kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Mkaguzi (Govela) ambaye imedaiwa haonekani na wala hakuna anayejua alipo na haijulikani nini kilichomsibu hadi sasa, Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi. Taarifa zimesambazwa mikoa mbalimbali kama ilivyo taratibu za kumtafuta mtu aliyetoweka/potea bila taarifa zozote,” alisema Misime.

Misime alisema taratibu za kiuchunguzi nazo zinaendelea na Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu mwenye taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa mkaguzi huyo, asisite kuwasiliana na kituo chochote cha polisi au kiongozi yeyote.

Tangazo latolewa kanisani

Mwananchi liliwasiliana pia na diwani wa Mtera jana, eneo ambalo ni nyumbani kwao Govela aliyesema tangazo la kutoweka kwa polisi huyo lilitangazwa kanisani.

Diwani huyo, Zawadi Maulya alisema akiwa kanisani kwenye ibada alisikia tangazo la kupotea kwa askari polisi huyo na baadaye alielezwa mkasa mzima. “Leo (jana) ndiyo nimepata ukweli, watu walizungumzia jambo hilo baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari (Mwananchi), kuwa ni mtoto wa mama Yuda ambaye namfahamu vizuri,” alisema Maulya.

Alisema anaifahamu familia ya askari huyo na hasa mama yake mzazi kuwa ni mcha Mungu, ingawa tabia na mienendo ya askari hawezi kuifahamu kwa kuwa ni muda mrefu tangu atoke kijijini
 
Back
Top Bottom