Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

Wewe ni ndugu yake?
Isije kuwa amelowea kwa pisi kali?
Mtu mzima hapotei..!
Nimeeleza vzr hapo juu,hata ingekuwa wewe umepotea ndugu jamaa na majirani wangekutafuta hata kama roho yako mbaya mazingira yanaonyesha wazi amepotea hata wenzake walistuka siku hiyo walipokuja kwake.
 
Hapa ndipo mnapokosea nyie watu wasiasa sio kila jambo lakuleta mizaha ya ccm na chadema,,..
Wengne hivyo vyama tunaviona f*** kbsa vyote sbbu ya ujinga ujinga ka huo,,..
Tujadili suala la mtu huyu kupotea,,..
Anzisha thread ya ndugu azory tutakuja kuchangia pia
Acheni double standard kujiona nyie bora kuliko binadamu wengine kisa watumishi wa umma huo ni upuuzi na ubinafsi,mkuki kwa nguruwe
 
Inawezekana ikawa ni sehemu ya kazi yake! Yupo kazini kama hakuwa akivaa mavazi ya kiaskari na ni askari akaiwa mazingira ya uraiani huenda yupo katika kutimiza majukumu yake ya kikazi, kazi hizo ni ngumu kuliko tunavyofhani. Na kama ametoweka kwa muda wa mwezi mzima bila ya kuwepo na taarifa yoyote hata kutangazwa katika vyombo vya habari, basi vyombo husika vitakuwa vikilifuatilia suala hilo kwa utaratibu uliowekwa mpaka hapo watakapoona umuhimu wa kulitangaza ama kinyume chake! Duniani apa kuna mengi ya kujifunza kuliko kujua kila kitu..
 
possible alimbambikia mtu kesi, hivyo na yeye kwa vile anaisha uswazi akambambikwaa !!!!
 
Huyo ni undercover agent wa CIA alipewa kazi sasa ile job description ame ignore ,kinachofuata huwa kama Dr shika vile alipoponea chupuchupu ,na ukipona lazima uwe mafia to the highest and topest
 
Inawezekana ikawa ni sehemu ya kazi yake! Yupo kazini kama hakuwa akivaa mavazi ya kiaskari na ni askari akaiwa mazingira ya uraiani huenda yupo katika kutimiza majukumu yake ya kikazi, kazi hizo ni ngumu kuliko tunavyofhani. Na kama ametoweka kwa muda wa mwezi mzima bila ya kuwepo na taarifa yoyote hata kutangazwa katika vyombo vya habari, basi vyombo husika vitakuwa vikilifuatilia suala hilo kwa utaratibu uliowekwa mpaka hapo watakapoona umuhimu wa kulitangaza ama kinyume chake! Duniani apa kuna mengi ya kujifunza kuliko kujua kila kitu..
YaMungu mengi.
 
Nimeiona Leo tar 5 august hii habari gazeti la mwananchi ukurasa wa mbele hii nchi ilipofika hakuna mtu anaejua kesho yake
Nami pia nimeiona mwananchi wameichambua vizuri Sana nafkiri Sasa jamii kwa eneo kubwa itajua uwenda akawa miji mingine kapata tatizo hata la ufahamu wakamtambua na kutoa taarifa.
 
Mh rais nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupa Afya njema na kuweza kutekeleza vyema majukumu yako ya kitaifa,mh rais Nina ombi maalum kwako kama mwananchi wako ambaye nimeguswa Sana na tukio la kupotea kwa askari polisi Emmanuelle Govella wa kituo kidogo cha mtumba mji wa kiserikali hapa Dodoma.

Mimi ni jirani hapa Nkuhungu Dodoma na Nyumba ambayo polisi huyu alikuwa amepanga siku ambayo ndugu wa huyo polisi walifika na polisi wa kituo Cha kati dodoma kuvunja mlango ili kujua kwanini askari huyo hapatikani muda mrefu nilikuwepo karibu.

Ilikuwa kati ya tarehe 19| 20 mwezi huu wa saba baada ya kuingia ndani walikuta simu ikiwa na laini zake zote Mbili lakini pia walikuta wallet yake ikiwa na vitambulisho vyake vyote mpaka kadi ya benki pamoja na fedha tasrimu sikujua kiasi gani, namba yake 0768243998 inaonyesha alikuwa hewani mala mwisho ni tarehe 26june hata ukiangalia WhatsApp inaonyesha hivyo mpaka siku wanabomoa kwake zilisha pita siku 24 Sasa Kuna maswali najiuliza ni kweli kwamba askari anapotea ZAIDI ya wiki 3 bila wenzake kujua?

Ombi langu kwako MH RAIS uunde kikosi maalum kichunguze upoteaji wa askari huyu Emmanuel govella Mpaka Leo hii nakutumia maombi haya ni takribani mwezi mmoja na siku 5 askari huyu hajaonekana ,nakutakia majukumu mema na Mwenyezi Mungu akutangulie.
Ina staajabisha
 
Askari amepotea?
Amepotelea wapi?
ITV yu wapi hatujasikia
Au amepotezwa na wasiojulikana
Kwanini tukio hilo lipo kimya
Siri ya jeshi baada ya u hunguzi ndio habaro mnajua vitu vingine ni aibu ya jeshi hivyo sio rahisi kutangaza tuu
 
Haya wameanza kutekana wenyewe kwa wenyewe sasa what goes around comes around
 
Kama aliingia kwenye anga za watu wakala kichwa utajuaje maaskari wa Tanzania wanajifanyaga sometimes miungu watu sasa ukikutana na watu wa Kanda Maalum wanakuua na wanakulawiti vilevile , dhuluma na dhambi zao ndio zinawatafuna hawatakaa salama, Babu yangu alishawahi kusema ukiona umekosa kazi ukawa sijui polisi sijui mkamata nini ujue basi tena huna maana kwenye jamii
 
Unajitoa mwenyewe, unadhani Askari officer WA nyota mbili anawezaje kupotea kienyeji hivo, zingatia maelezo hapo juu alikuwa mkuu wa Kituo fulani,alikuwa hapendelei kuvaa uniform akienda kazini badala yake alikuwa akibeba begi jeusi mgongoni, jiulize Kwa nini alikuwa anaficha identity? Defenitly was an agent undercover, jiulize Askari wa level officer commanding station anawezaje kupotea polisi wasitoe tamko mpaka ndg zake ndo wamtafute? Anzia hapo kujiuliza kama alivuruga mission huyo ndo umsahau, formula ni moja tu kwamba if the law doesn't work, Eliminate.
Kama nakuelewa hivi
 
Back
Top Bottom