Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,411
- 7,306
Miaka ya 2011 au 2012 mimi binafsi bila kuhadithiwa nilishuhudia askari mmoja wa jeshi la Magereza kijana mdogo asie na cheo (rank yake inaitwa Warder) akihangaika kumuulizia mitaani pale Mpwapwa mjini mfungwa alie mtoroka.
Askari yule akiwa peke yake alikuwa akiliswaga na kulilinda kundi la wafungwa kama 10 hivi akipita na lile kundi la wafungwa mitaa ya Mpwapwa mjini karibu na Gereza lake ambalo ni gereza la wilaya ya Mpwapwa na wafungwa wale wakiwa wameshika viboko wakimfuatilia yule mfungwa alietoroka.
Hii ni jinsi gani askari wa hilo Jeshi walivyo na mazingira magumu ya kazi , nilimshuhudia askari yule akitembea kwa miguu huku akiwa ana silaha/bunduki inayobeba risasi 10 tu Bunduki aina ya S.A.R huku akiliswaga kundi hilo kubwa la wafungwa peke yake na niliwashudia pia wale wafungwa baadhi yao wakimkashifu kwa kuwa nyuma.
Jeshi la Magereza wana mazingira magumu ya kazi ,hawana magari ya kutosha wanatembeaga kwa miguu wafungwa kwa askari , sijawahi kuona jeshi hilo likimiliki wanyama aina ya farasi au ndege aina ya Helikopta kama mojawapo ya vitendea kazi.
Askari huyo nina uhakika kama taratibu za jeshi hilo zinavuokuwa kwa askari anaepoteza mfungwa alikuja kuzuiwa kupanda cheo kwa miaka kadhaa na hivyo kubaki chini na rank ya Warder.
Naisihi mamlaka itengue maamuzi yake ya kulinyima jeshi la Magereza kibali cha kuajiri ,kwani kwa hakika maamuzi haya yanawaumiza zaidi askari ambao hawana vyeo na wenye cheo cha chini cha koplo kwani hao ndio hushika silaha kushinda na wafungwa (waliowahi kuwa majeshini wanajua uhalisia wa majeshi askari wa ngazi mbili za mwisho chini huwa ndio wanapitia msoto/mzigo mkubwa wa majukumu ya jeshi).
Askari hawa wa vyeo vya chini wataendelea kupata kazi changamoto ya kuswaga na kulinda makundi makubwa ya wafungwa maporini na vichakani na kuendelea kuadhibiwa pindi wanapotorokewa.
Na pia wanapata changamoto kwa kuwa wachache, waliofikisha wakati wa kustaafu wakistaafu na ilhali magereza mengi kama sio yote yamejaza watu kuliko uwezo wake , na mazingira ya kazi ni magumu.
Mamlaka na sisi wananchi kiujumla tungetambua kwamba askari magereza kiujumla ni watumishi wazalendo,wachapakazi na wakakamavu kwelikweli hivyo tunakuwa na deni la kiungwana la kuwathamini na kuwajali.
Nimalizie kwa wito kwa Mheshimiwa kutafakari upya mtazamo wake na pia atafakari pia na kuwasaidia jeshi hilo kwa kuwanunulia vitendea kazi kama farasi na magari na pia bila kusahau kujenga zaidi magereza mengine sababu taifa letu idadi ya wanachi inaongezeka kwa kasi na idadi ya wafungwa na mahabusu nayo inaendelea na itaendelea kuongezeka.