Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Sabaya amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa ujambazi wa kutumia silaha. Katika kujitetea, mara nyingi amesema kwamba alikuwa anatekeleza maagizo ya mamlaka iliyomteua.
Kwa maoni yangu, hata bila utetezi wake huo, kitendo cha mamlaka ya uteuzi kunyamazia vitendo vyake vya ujambazi, ni kuhusika moja kwa moja. Angalau tunaweza kumwondolea uhusika Rais Samia, kwa kuwa aliamua kuchukua hatua.
Najua kwamba Sabaya ni mbuzi wa kafara tu. Magufuli na idadi kubwa ya wateule wake, sio tu wamehusika na ujambazi, wizi, uporaji wa mali na hata binadamu, na wizi wa kura, lakini wamehusika pia na utekaji, utesaji na mauaji ya wanasiasa ambao walikuwa na msimamo tofauti na Magufuli.
Hata kama Magufuli hayupo hai, ipo haja ya kufungua kesi dhidi yake, na dhidi ya wateule wengine, kutumia ushahidi na hukumu dhidi ya Sabaya, ili angalau haki itendeke kwa wengine kama Ben Saanane, Alfons Mawazo, Tundu Lissu, Azory Gwanda, na maelfu ya waliovunjiwa nyumba zao, nk.