3 Angels message
JF-Expert Member
- Aug 3, 2017
- 4,877
- 13,555
Wasalaam wakuu,
Kwa sisi wafugaji hasa wa kuku hivi karibuni tulipata afuheni ya chanjo mara baada ya kuingia sokoni kwa chanjo ya kuku ya tatu moja ambayo kwa maelezo inatoa kinga kwa magonjwa matatu Newcastle, mafua na ndui ambayo hapo awali ilihitajika uingie gharama kununua chanjo hizo tofauti tofauti.
Lakini sasa pamekuwa na malalamiko kadhaa kuwa hii chanjo haipo vizuri kwenye kukinga hayo magonjwa maana kuna baadhi waliochanja kuku wao ila Newcastle ilipowakumba iliwafagia kuku wote na hata mafua kinyume na matarajio na hivyo kuingia hasara kubwa.
Na baadhi ya madaktari wa mifugo wanadai hii chanjo haina nguvu hiyo inayosemwa na wanapendekeza bora utumie chanjo ya Newcastle yenyewe halafu uichanganye na hiyo tatu moja.
Ili kuondoa huu mkanganyiko ni vyema mamlaka husika watusaidie hii chanjo ya 3 moja imefanyiwa utafiti kweli na inafaa au laa ili kutuondolea hasara na huu mkanganyiko uliopo sasa juu ya uimara wake kukabiliana na hayo magonjwa.