Nimatumaini yangu kwamba wanajukwaa mnaendelea vizuri.
Wiki iliyopita iliripotiwa jukwaani kwamba makatibu wa TSC Tanga na Mkinga wamekua wakifanya udanganyifu kwa kila mmoja kumsainia mwenzie kwenye halmashauri yake ili watoe hela.
Jambo la ajabu zaidi nikwamba wamekuja maafisa kutoka TSC makao makuu. Maofisa hao watatu wamewahoji watumishi hapo Tanga lakini hawagusi kiini cha tatizo jambo ambalo linaonesha kulindana na harufu ya rushwa.
Kilichoripotiwa mtandaoni ni matumizi mabaya ya ofisi kwamaana ya udanganyifu au wizi wa mali ya umma. Maafisa wa TSC kutoka Dodoma wanawauliza watumishi kwamba
1: Ninani aliyetoa taarifa hizo mtandaoni. Kwani kutoa taarifa ni tatizo? Hapo tatizo ni ujanjaujanja kwenye mali ya umma. TSC makao makuu acheni kutoka nje ya reli
2: Je ofisi inamgogoro gani hadi taarifa ziripotiwe mtandaoni?Hapo mgogoro upo wapi? Kwani kuusema ukweli ndio inamaanisha mgogoro?
Mamlaka husika eleweni kwamba tatizo hapo sio kutoa taarifa hiyo,maafisa hao walitakiwa kujua kwamba kilichosemwa kina ukweli gani? Mpango huo wa kumlinda katibu huyo wa TSC Tanga hauna afya katika kada ya ualimu. Hao maafisa watatu kutoka makao makuu hawajaitisha nyaraka kujua ukweli bali wanauliza nani ametoa taarifa hizo.Watumishi hao ndani ya ofisi wamesema hamna mgogoro wowote ofisini jambo ambalo wamelikubali kwa woga na unafiki. Wamekua wanafiki kwani kama hakuna shida ofisini mbona hawashirikishwi katika maamuzi ikiwemo kutoa hela na matumizi ya hela hizo.
TSC makao makuu badilikeni acheni kulinda wizi huo uliofanyika muda mrefu na matumizi mabaya ya ofisi kwa watu wenu mlio waweka. Mkiendelea kuwalinda mtakua sehemu ya uozo huo
Katibu mkuu mpya wa TSC angalia sana watendaji wako hao watakuharibia na wanafanya kazi kwa mazoea na undugu