Mamlaka husika fanyieni utafiti haya malori aina ya FUSO

Yaan hili tatizo vijana wa kaskazini sijui watasaidiwaje. Huwa wakikaa bar wanasifianaga kbs bwana jama unatembea sana wewe hufai. Basi wanaona sifaaaa... yaani hizo filimbiii daah. Hata bure sithubutu kupanda lift. Halaf ukikuta dereva ameshaiva kvant ama nyagi anaona kama hatembei hv. Na ingine aweke kwenye kichupa cha maji sikilizia filimbi zake. Na usimombe gari haina mzigo.
Ndo maana Bus za kichina kazkazn n chache bado zipo zle lori zenye body ya bus ya kuchonga huku ina engine ya scania machalii wanapenda mlio wa scania balaa wakiuskia hadi wanaisindikiza kwa miluzi
Sahiv had pikpik zinaharibiwa exhaust na zinapigwa Moshi tatu ili ilie kama scania
 
Sidhani kama umemuelewa mtoa mada. Ukweli kwamba fuso la tani 5 kubeba tani 15 unajifanya hujui? Bodi zinafanyiwa modification na kuweza kubeba mzigo mkubwa kwa madai kwamba engine za hizi gari zina nguvu, bila kuzingatia uwiano wa uzito na bodi ya gari katika ile Centroid( centre of mass) na vitu kama hivyo.
Modification ya bodi sawa sijajua kuhusu kadi ya gari wanafanyaje kubadili uzito kwenye kadi ili iweze kupita mzani
 
Fuso ya tani 4 umeitoa wapi mkuu? Au unaongea tu jamaangu

Naongea kutokana na uzoefu wa zaidi ya miaka 10 kuendesha Fuso (zote namanisha single,tipper na tandam) na uzoefu wa miaka 7 ya kumiliki Fuso zaidi ya 10

Usiongee vitu usivyovijua.

Nitakubaliana na wewe kuhusu ishu ya MADEREVA tu kuwa hao ni pasua kichwa ila sijuI kama wanatumia hivyo vitu umeorodhesha.

Ajali za Tanzania hii sababu kuu ni 3
1: Elimu ya MADEREVA
2: Barabara vimeo
3: Spea vimeo

Usisingizie FUSO mkuu. Achana nayo kabisa
Mtu mwenye IST halafu asafiri usiku utamjua tu, achananae anaongea kimitandao hana anachokijua kuhusu anachokizungumzia, wakati mwingine unamuacha afurahishe genge.
 
Acha upuuzi unataka kutuambia Wajapani waliotengeneza hii gari hawakufanya research, mje mtake kufanya nyie Mapopoma ambao hamjawahi hata kutengeneza baiskeli ya kwenu?
Japan ndio wansozijenga hizo bodi!?? Umesoma na kuelewa !?? Au ndio ila hadithi ya nyuki na yule mdudu anaebiringisha kinyesi!?? Nafikiri ulimpa shida sana mwalimu wako!!! Kama bandiko dogo hiv huelewi vipi importance of studying physics!?? Utaelewa kweli!?
 
6D15T,6D16T 3T,6D17,6M6OT,6M61...fuso ni gari kali sana...kadiri muda unavyokwenda maboresho yanafanyiaka. Ajali nyingi za mafuso chanzo ni USINGIZI. Huku field tunawaita wakukesha, usiombe ukutane nao iyovi wana wahi mabibo.
 
Nadhani shida sio kupakia Bali baadhi ya Madereva ni shida kuna Moja nilikimbizana nayo Kutoka Tanga kuja Dar Gari inakimbia utadhani haina mzigo ni balaa ukute Turbo yake bado ipo unaweza kusema haijapakia!!..Zile Kona za Wami jamaa ana lala nayo tu nilivyofika Kibaha nikamwambia utakufa wewe!!.. imagine Niko na crown lakini Fuso ilinitoa Jasho
Ha ha ha ha wana balaaa.. nakuakbia juzi kati wakato tunateremka usiku kuna hiyo fuso apaa ndengaa. Bila shala alikua na ndizi. Siyo kutembea kule ni kupaa. Nawasifu madereva wanaoendesha usiku. Yaan naogopa balaa. Wanawezaje?
 
Ndo maana Bus za kichina kazkazn n chache bado zipo zle lori zenye body ya bus ya kuchonga huku ina engine ya scania machalii wanapenda mlio wa scania balaa wakiuskia hadi wanaisindikiza kwa miluzi
Sahiv had pikpik zinaharibiwa exhaust na zinapigwa Moshi tatu ili ilie kama scania
Ha ha ha kiufupi hata mimi napenda scania. Na napendaga hizo makitu. Mchina unanikera sana. Napendaga jinsj engene zinavyolalamikaga. Halaf wanavyipenda ligi sasa nachekaga sana ligi za mchina na msweden aisee. Ila wanakuambia mwili hauna roho tembea dere iende irudi arifuuu
 
Neno utafiti limetumika vibaya. Yaan Japan wasifanye utafiti mje kufanya utafiti Wamatumbi?
Mbona yuko sawa kutumia neno 'utafuti'. Ana maana utafiti ufanyike hapa kwetu, kutambua nini chanzo cha ajali nyingi zinazohusisha malori ya Fuso hapa kwetu Tanzania. Ili ijulikane tatizo au chanzo cha ajali. Kama ni madereva wetu, au ni mifumo mibovu ya gari lenyewe au ni miundo mbinu yetu kama Taifa nk na nk.
 
Back
Top Bottom