Mamilioni ya Watu kukimbia maeneo yao kutokana na athari za uchafuzi wa Hali ya Hewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Ripoti hiyo inaangazia athari zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile upungufu wa maji, upungufu wa uzalishaji chakula, ongezeko la maji baharini, masuala ambayo huenda yakasababisha uhamiaji wa mamilioni ya watu kufikia mwaka 2050.

Ripoti hiyo inasema takriban watu milioni 216 huenda wakalazimika kuhama makwao kwenye maeneo 6 ulimwenguni kutokana na uchafuzi wa hewa na ukosefu wa usawa wa kimaendeleo. Maeneo hayo ni pamoja na Latin Amerika, Afrika kaskazini, Mashariki mwa Ulaya na Asia ya kati, Asia kusini na Asia mashariki pamoja na eneo la Pacific.

Ripoti hiyo pia imeonya kwamba huenda kukajitokeza maeneo yenye misongamano mikubwa ya wahamiaji katika kipindi cha muongo mmoja, hali hiyo ikitabiriwa kudorora kufikia mwaka wa 2050.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom