Mamia ya watoto watoweka jela nchini Syria

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mamia ya wavulana wametoweka kwenye Gereza la Kikurdi nchini Syria ambalo linawazuia wapiganaji wa Kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS na familia zao.

Hii ni baada ya wanajeshi wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani wakipigana na wanamgambo wa IS kwa siku kumi ili kuikomboa jela hiyo.

Ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limeyasema hayo leo ikiwa ni siku moja baada ya kiongozi mkuu wa IS, Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi, kuuawa katika operesheni ya Marekani kwenye makazi yake Kaskazini Magharibi mwa Syria.

Rais Joe Biden alisema al-Qurayshi alihusika na shambulizi kwenye jela hiyo ya Syria, pamoja na mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa jamii ya Yazidi nchini Iraq mnamo mwaka wa 2014.

Watoto hao ni kutoka jamii na uraia wa mchanganyiko. Waliwekwa gerezani kwa sababu serikali nyingi zimekataa kuwahamisha, huku mamlaka za Kikurdi zikielezea wasiwasi kuwa huenda wana tabia za itikadi kali.
 
Back
Top Bottom