Mamia ya waombolezaji wajitokeeza kuuaga mwili wa Mpoki Bukuku jijini Dar, kuzikwa leo Dodoma

Abu Haarith

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
314
165

Mamia ya wadau pamoja na wale wa Tasnia ya Habari wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa shule ya Tabata, Wilayani Ilala Jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa mpiga picha Mwandamizi wa Magazeti ya The Guardian Limited yanayochapisha magazeti ya Nipashe, The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku (44) aliyefariki dunia juzi baada ya kupata ajali ya gari.

Wadau mbalibali walipata kutoa salamu zao za rambirambi kwa familia ya marehemu ambapo pia Waziri mwenye dhamana, Mh. Nape Nnauye alipata kutoa salamu na kuungana na msiba huo.
Pia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mh. Freeman Mbowe nae alipata kutoa salamu huku akitaka wanahabari kuyaendeleza yale aliyoacha Marehemu.

Pia viongozi mbalimbali wamepata kutoa salamu zao wakiwakilisha tasnia ya habari, vyama vya wanahabari na maeneo mengine wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu.

Msemaji wa familia, ambaye ni kaka wa marehemu, Gwamaka Bukuku, aliwashukuru watu wote kwa kujitokeza ambapo amewaomba kuendeleza umoja wao kama walivyouonyesha kwa marehemu.

“Mwili wa marehemu baada ya kutoka hapa unapelekwa Dodoma kwa mazishi na huko ndipo utazikwa. baada ya taratibu hizi hapa mwili utasafirishwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake, Dodoma kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika leo Dodoma” amesema. Habari picha na Mob Blog

Mwili wa Mpoki Bukuku ukiwasili nyumbani kwake Tabata ukitokea Muhimbili

Mwili ukiwa ndani ya nyumba yake

Familia ya Mpoki Bukuku ikiwa na uzuni baada ya kuwasili kwa mwili wa mpendwa wao nyumbani

Mwili wa Mpoki Bukuku ukitoka nyumbani kwake kuelekea uwanja wa shule kwa ajili ya kuagwa

Mkurugenzi wa Redio One, Deo Rweyunga ( mwenye shati jeusi ) akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akisalimiana na aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini, Baraka Konisaga






















CHANZO : Mo dewji Blog
 
Raha ya milele umpe ee Bwana na Mwanga wa Milele umuangazie apumzike kwa amani. Amina
 
RIP mpoki Bukuku, hivi Bukuku ni watu wa dodoma?, sio mbeya?, au mleta mada amekosea?, naomba ufafanuzi tafadhali
 
RIP mpoki Bukuku, hivi Bukuku ni watu wa dodoma?, sio mbeya?, au mleta mada amekosea?, naomba ufafanuzi tafadhali
ninavyodhani wazazi itakuwa walikuwa watumishi wa serikali dodoma na kustaafia huko mpaka wakaamua kuendelea na maisha pale, just like wengi wanavyoamua kujenga na kuishi dar hata wakifia london wanaletwa kuzikiwa makaburi ya kinondoni

ni mtazamo tu
 
ninavyodhani wazazi itakuwa walikuwa watumishi wa serikali dodoma na kustaafia huko mpaka wakaamua kuendelea na maisha pale, just like wengi wanavyoamua kujenga na kuishi dar hata wakifia london wanaletwa kuzikiwa makaburi ya kinondoni

ni mtazamo tu
Nàshukuru kwa ufafanuzi mzuri
 
Ndio ni watu wa Mbeya, majina kama. Mpoki, Bukuku, Gwamaka,Ulimboka,Gwakisa, Ambakisye,Anyelwisye, Atu,Bupe, Bhumi, Mwakyoma,Mwafilombe,Lusekelo,aUswege,nk. asili yake ni Mbeya
 
Back
Top Bottom