kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,888
Mamia ya mashirika ya kigeni yashiriki maonyesho ya kibiashara Korea Kaskazini
Mei 23, 2019 08:08 UTC
Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vimeripoti kwamba mamia ya mashirika ya kigeni kutoka nchi tofauti yameshiriki maonyesho ya kimataifa ya kibiashara nchini humo licha ya vikwazo vya Marekani dhidi ya serikali ya Pyongyang.
Shirika la Habari la nchi hiyo KCNA limeripoti kwamba zaidi ya mashirika 450 kutoka nchi za China, Russia, Pakistan, Poland na nchi nyingine za dunia yalipeleka bidhaa zao katika maonyesho ya 22 ya kimataifa ya kibiashara yaliyofanyika mjini Pyongyang hivi karibuni. Shirika hilo la serikali, limeongeza kwamba maonyesho hayo yalifunguliwa na viongozi wa ngazi za juu wa sekta ya kiuchumi wa nchi hiyo. Chunguzi rasmi zilizofanywa kuanzia mwaka 2007 hadi 2019, zinaonyesha kwamba maonyesho ya kibiashara ya mwaka huu mjini Pyongyang ndio makubwa zaidi kutokana na ushiriki mkubwa wa mashirika ya kigeni. Hii ni katika hali ambayo katika maonyesho kama hayo ya mwaka jana mjini Pyongyang ni mashirika 260 pekee ndio yaliyohudhuria.
Maonyesho hayo makubwa ya kimataifa yamejiri huku Marekani ikiwa imeshadidisha vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini kwa lengo la kuifanya nchi hiyo ikubali kuipigia magoti. Wakati huo huo mwakilishi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi, ameionya serikali ya Marekani kubadili mitazamo na fikra zake kuihusu nchi hiyo badala ya kutumia vitisho na mabavu. Tae Song amesisitiza kwamba Washington inatakiwa kuchukua uamuzi muhimu kuhusiana na kuondoa vikwazo vyake dhidi ya Pyongyang kabla ya kuanza upya mazungumzo ya pande mbili. Song amezidi kufafanua kuwa, utumiwaji wa lugha za kibabe unaofanywa na Marekani ni kosa kubwa na kusisitiza kuwa hatua ya Washington ya kutwaa meli ya Korea Kaskazini, ni kikwazo kingine kikubwa katika kuboreshwa uhusiano wa pande mbili.
My take:Najikuta nacheka tu maana vikwazo vya USA vimeanza kufeli duniani yaani nchi nyingi zimeshaanza kuipuuza marekani