'Mamia' wampokea Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Mamia' wampokea Kikwete

Discussion in 'Celebrities Forum' started by NakuliliaTanzania, Oct 8, 2007.

 1. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi nilidhani wangekuwa maelfu, halafu kumbe ni wanachama wa CCM..so ningedhani ingekuwa mamia ya wana CCM....au ndo kujaribu kufunika ishu?


  Habari za Kitaifa

  Mamia wampokea Kikwete

  Mwandishi Wetu

  HabariLeo; Monday,October 08, 2007 @00:04

  MAMIA ya watu jana walifurika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea Rais Jakaya Kikwete aliyerejea nchini baada ya ziara ndefu ya Marekani.

  Watu hao akiwamo Waziri Mkuu Edward Lowassa, mawaziri kadhaa na wanachama wa CCM waliokuwa wamevalia mavazi ya njano na kijani walifurika uwanjani tangu saa saba mchana, wakimsubiri Rais Kikwete aliyewasili baada ya saa moja.

  Umati huo wa watu ulikuwa ukiburudishwa na nyimbo maarufu za John Komba wa TOT huku wakiwa wameshika mabango ya kumkaribisha nyumbani rais.

  Mengi ya mabango yalisomeka ‘Karibu nyumbani Rais Kikwete.’

  Baada ya kuwasili, Rais Kikwete alitoka nje ya eneo la kupumzika wageni mashuhuri (VIP) na kwenda nje kuwasalimia wananchi hao waliokuwa wamefurika ambao nao walimshangilia kwa makofi na vigelegele kabla ya kuondoka kuelekea Ikulu kwa ajili ya mapumziko.

  Ziara hiyo ya rais ya wiki tatu nchini Marekani imeelezwa kuwa na mafanikio kutokana na kuiwezesha Tanzania kupatiwa kiasi kikubwa cha fedha kuliko kilichowahi kutolewa kwa nchi yoyote chini ya Mpango wa Millennium Challenge Corporation(MCC).

  Mtendaji Mkuu wa MCC, Balozi Johyn Damilovich alimueleza rais uamuzi wa bodi ya shirika hilo kuidhinisha fedha za kugharamia miradi mikubwa ya uwekezaji nchini. Fedha hizo siyo mkopo.

  MCC imeidhinisha dola za Kimarekani milioni 699 (Sh bilioni 881), kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko kilichowahi kutolewa kwa nchi yoyote duniani na MCC. Miongoni mwa miradi itakayonufaika na fedha hizo ni ile ya ujenzi wa miundombinu.

  Taarifa iliyotolewa na Ikulu juzi ilisema kuwa Marekani iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwamo eneo la kijeshi.

  Katika eneo la uwekezaji kampuni kadhaa zimeonyesha nia ya kujenga viwanja vya mbolea nchini na miradi mingine. Miongoni mwa makampuni hayo ni JP Morgan, Merrill Lynch, Tegris na Gilbraltar Properties.

  Wakati wa ziara yake nchini humo aliyoianza Septemba 15, Rais Kikwete alizindua matangazo ya vivutio vya utalii wa Tanzania katika televisheni ya kimataifa ya CNN huku kampuni kadhaa zikionyesha kukubali kuwekeza nchini katika sekta ya utalii ikiwamo kampuni maarufu ya mahoteli ya Global Hyatt Corporation ambayo imekubali kuja nchini kuangalia maeneo ya kujenga mahoteli.

  Rais pia alizindua maandalizi ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa 33 wa Utalii Afrika uliopangwa kufanyika Mei mwakani mjini Arusha.
  http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=4431
   
 2. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #2
  Oct 8, 2007
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  huyu mwandishi hajui protocal au ndio wanamtandao wamebadili..mnajua aliyeongoza mapokezi ni makamu wa rais shein...mbona wanamfanya kama hayupo??? alafu wale walioenda pale walikusanywa na mabasi na kupewa buku tano kila mmoja kama chai....wengine wasaniii wa mjini wanahojiwa wanajifanya wamesafiri toka tanga maalum kumlaki muhashimiwa....
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Nafikiri huyu mwandishi anajipendekeza kwa EL kwani aliyempokea JK ni Shein, kwa vile shein sio mwanamtandao basi hakuonekana. Kuna ajenda ya siri ya kumpigia Ndanda Kosovo debe la 2015 na huu ni mpango mahsusi wa mafisadi, ni lazima tusimame kidete kupambana nao
   
 4. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  OOh poor Shein nadhani historia itamhukumu kuwa 'hakushiriki nao' ndo maana huyu mwandishi wetu hakumwona, na kama unavosema hakujali protokali...
   
 5. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hadi jumatatu mchana kwa saa za uingereza na marekani na tanzania, oneni watu wakavyomponda Muungwana kwa kuwa kapokewa na watu wengi ! hapo ndipo utakapojua watengenezaji propaganda !
   
 6. K

  Kasana JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2007
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 413
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  karibu nyumbani JK, taifa linasubiri 'response' yako.
   
 7. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nina shaa kama hayo mabango waliyokuwa nayo kuna lililokuwa likisomeka hivyo.....
   
 8. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Lakini Kaka Kada Embu tuwe wakweli kidogo Muungwana!Hivi kwa nini Jk anapokewa kwa makeke namna hiyo?Kuna nini kinataka kuelezwa hapa?Au safari yake hii ya Marekani imekuwa na Mafanikio kuliko alizowahi kufanya huko mwanzoni?.Au wananchi wamefurahi kwamba amerudi salama kwa sababu Medical check up huko Ufaransa iliwapa wasiwasi labda Jk ana tatizo kubwa?.Na wala sio kweli kwamba watu wapo hapa kumshambulia Muungwana!TUTAMPONGEZA atakapomuondoa Kaka Karamagi katika Cabinet!
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Oct 8, 2007
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  kada acha upenzi..hata wengine ccm lakini ukweli lazima usemwe ...jk kapoteza umaarufu..source za waliokuwa uwanjani zinasema hakuwa na ile kicheko chake cha kawaida ...ana mawazo mengi..na hata katika haliisiyo ya kawaida aliwakwepa waandishiambao siku zote ni marafiki zake...ni wa kumuonea huruma for sure..

  tofauti na ule umati unaomlaki kila mara wa jana ulikuwa wa kulazimisha....watu walisombwa na mabasi na nauli juu..na wala hawakuwa wengi ...wapo wachache walioenda kwa moyo na walikereka sana na kitendo cha wengi walopelekwa pale kuvaa magwanda...capt komba alifanya kazi kubwa sana ya kuiimba ili kuendelea kuvutia watu pale uwanjani...it was no as usual....hata jk atakuwa amegundua kuwa ule umati haukuwa wa rohoni kama wakati mwingine...
   
 10. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2007
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  KM (kuwadi wa mafisadi) sijakuelewa hata kidogo unachoongea.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mawaziri wote hao wameacha kazi zao, familia zao, ndugu zao, majimbo yao ili tu kwenda kumpokea Muungwana airport?

  Tanzania bado tumelala sana. Hayo masaa tunayopoteza airpot si tungetumia kwenye uzalishaji? kwenye kutatua shida za watu? Kwenye kuhimiza mambo ya maendeleo?

  Nashangaa kila siku watu wako VIP lounge, eti hata wabunge ni VIP. Hivi mtu kama Zitto akitelemkia kule kwa wananchi wengine kutatokea nini?

  Hivi hawa CCM, CHADEMA, TLP, CUF, wanapingana nini? Naona mambo yao yote yanafanana. Kila mmoja anajifanya ni VIP, kila mmoja kakimbilia shangingi badala ya hizo pesa kununua vitabu vya shule, kila mmoja kwenye kura ya kupandisha mishahara yao, anasema ndio.

  Sisi kweli tumelala, tunacheza mdundiko wao bila kujua ulikoanzia wala utakako ishia.
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Baba KABWELA UNO " Wenye wivu wajinyonge"
   
 13. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli yaani.....tatizo la bongo ni kuwa kila mtu anataka ufalme,huyo kikwete mwenyewe kwanini asiseme kwamba hataki li-umati kuja kumpokea???wanapenda sana hayo mambo ya umungu mtu.......
   
 14. M

  Mshamba wa Kijijini Member

  #14
  Oct 8, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waacheni tu kiama kimefika walipe wasilipe wembe ni ule ule wanaondoka ngoja maandamano yaanze mtaona.

  ila msiwe waoga kuonyesha haya maoni yenu kwa maandamano waoga sana CCM wala msihofu.
   
 15. M

  Mshamba wa Kijijini Member

  #15
  Oct 8, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hata mchawi anao wachawi wenzake waache marehemu wana jikokota karamagi si naye alikuwepo?

  wezi wanapokea wezi wenzao.hata huyo Lowassa mwizi nitawapa stori zake ngoja nipange mambo vema.
   
 16. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tupe story mshamba wa kj,tunakuaminia.
   
 17. B

  BroJay4 JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2007
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtanzania,
  Ndio maana tukaitwa maskini,
  maskini huwa ni mtu jeuri sana,anapenda sifa sana,haiingii akilini
  viongozi wote wanahamia airport eti kumpokea rais,what a hell,hivi akienda mkuu wa mkoa peke yake kutaharibika nini?Watu weusi sijui
  hii laana itaondoka lini?Jifunzeni kwa nchi za magharibi hamna upuuzi kama huu,Bush na Brown ni sawa na Tibaigana tu huku majuu.
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sioni sababu ya kuwa kila rais akisafiri akapokewe na lukuki ya watu. .....ila hii ya safari hii ccm wamefanya kwa makusudi kuonyesha kuwa rais hajapoteza umaarufu wake kama watu wanavyopiga kelele kwa kiingereza wanasema ni image control! na hii image control sio kwa sisi watanzania, maana hatubabaishwi na tarumbeta la john komba, bali n kwa vyombo vya nje visivyojua propaganda ya tz
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Oct 8, 2007
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  mimi naona haya mapokezi ni kama kupoteza muda vile. Time is money jamani.

  kwa wenzetu mlioko majuu hivi George Bush na Gordon Brown na wenyewe hupokewa na umati wa mawaziri na wananchi kama JK?
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  safari zake nyingi tu Muungwana amekuwa akipokewa na watu kede kede, hii sio mara ya kwanza mheshimiwa !
   
Loading...