Mameya wa Ilala na Kinondoni walaumu utungaji wa sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mameya wa Ilala na Kinondoni walaumu utungaji wa sheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watu, Feb 23, 2011.

 1. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Msikilize meya wa ilala redio one!

  Sheria zipindwe kisa busara ya kubembeleza kura lolo!
   
 2. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Jamani nilivyo mwelewa meya wa ilala his talking politics

  Mambo mengi tanzania hayaendi kwa sababu sheria hazifwatwi na hazifwatiwi kwa sababu za kisiasa na rushwa?

  Eg mtu akijenga bar/night club kwenye makazi ya watu huku akilipa kodi zote manispa na tra

  Mtu kama meya wa ilala atato kibala kwa kuwa huyo mtu anaingizia kipato manispa??

  Ndio hilo tu
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  By WATU:_Jamani nilivyo mwelewa meya wa ilala his talking politics

  Mambo mengi tanzania hayaendi kwa sababu sheria hazifwatwi na hazifwatiwi kwa sababu za kisiasa na rushwa?

  Eg mtu akijenga bar/night club kwenye makazi ya watu huku akilipa kodi zote manispa na tra

  Mtu kama meya wa ilala atato kibala kwa kuwa huyo mtu anaingizia kipato manispa??

  Ndio hilo tu

  Kwanza sote tumesikiliza mahojiano hayo, Meya huyo Kijana kwa jina Silaa kathibitisha kweli kuwa vijana wanaweza kuongoza, vile vile ameweza kuthibirihsha kuwa Mhe John Magufuli kakurupuka katika kufanya maamuzi hayo. Nasema hivyo kwa sababu Mhe John Magufuli ametoa madai kuwa mabango yamatangazo yaliwekwa katika hifadhi za barabar yanasababisha "obstruction" kwa watumiaji barabara na kusababisha ajali.

  Sasa nauliza kati ya Mabango ya Matangazo na magari yanayoharibika na kutelekezwa barabarani nmijini na vijijini ni kipi hatari zaidi kwa watumiaji wa barabara na wananchi?

  Sheria hiyo hiyo anayodai kuwa inampatia madaraka kuagiza kuondolewa kwa mabango, yaani Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009 katika Ibara ya 9 (1-10) inaipa TANROAD mamlaka ya kuondosha magari yaliyoharibika ama kutelekezwa barabarani kwa zaidi ya masaa 6 kwa maeneo ya mijini na masaa 24 katika maeneo ya vijijini.

  Lakini kutokana na TANROAD kushindwa kutekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa Kanuni zake yenyewe, idadi ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani hususan zile zinazosababishwa na magari yaliyoharibika na kutelekezwa barabarani zinazidi kuongezeka kila mwaka hapa nchini.

  Kwanini TANROAD haitumii fedha TANROAD za mfuko wa barabara ambao kila mwananachi huchangia anaponunua mafuta ya magari kununua magari ya breakdown yenye uwezo wa kuvuta magari makubwa na madogo yaliyoharibika barabarani kwa kila mkoa?

  Hivi kati ya makampuni yaliyoweka mabango ya matangazo kwa kuingia mikataba na halmshauri za Miji na wilaya na wenye magari makubwa na madogo yanayofanyiwa matengenzo barabarani kinyume cha Kanuni za sheria ya barabara ibara ya 9.3 na 4 na ambao amara kwa mara huwaga mafuta ya aina mbali mbali. Kati ya hawa wawili ni yupi anayecheza sheria za barabara Magufuli alizoapa kuzilinda zisichezewe?Mbona hatuoni jitihada zozote za kuzuia hali hiyo kutoka kwa Mhe John Magufuli na TANROAD?.
  Ndugu zangu sheria sio straight jucket kama wengi wetu tunavyofikiri, ni lazima busara itumike katika kutekeleza sheria kwa kuwa nature ya sheria nyingi za kimataifa na hususan za nchi maskini kama Tanzania zinaji contradict. Hivyo sheria haziwezi kuchukuliwa kama "Menu" katika hoteli ambapo mlaji huchagua kutumia chakula apendacho na kuacha asichopenda. Kwani haiwezekani kiongoizi mwandamizi wa hadhi yake akaamua kuzingatia zile sheria zinzolinda maskahi ya sekta yake na kudharau na kupuuza sheria zinzotoa haki kwa wadau, taasisi na wananchi kwa ujumla.

  Kwa mtizamo wangi na nikizingatia jinsi Mhe John Magufuli alivyogawa nyumba za Serikali kwa upendeleo akiwapendelea watu wasiostahili waliokuwa na uhusinao naye wa karibu na jinsi alivyogiza nyumba aliyonunua yeye ishushwe bei, nahisi kuwa baada ya kugundua kuwa industry ya mabango ya matangazo ni moja ya multi billion industry baada ua kukua sana kipindi alipokuwa hayupo katika wizatrra hiyo, anachofanya ni kutafuta njia za kusolicit rushwa through cohesion.
   
 4. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kilaza ni Watu(aliyeandika thread hii).Wewe Watu hapa sio facebook jaribu andika thread ya kueleweka.
   
 5. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Jana katika kipindi cha hoja yangu, kilichokuwa kilichowakutanisha mameya wa manispaa za ilala mhe jerry silaa, na kinodnoni mhe mwenda na mwanashaeria oscar kikonyo kilichokuwa kikijadili sakata la mhe waziri wa miundo mbinu mhe john magufuli kuagiza kuondo mlewa kwa mabango ya matangazo katika hifadhi za barabara yaliyowekwa baada ya kuingia mikataba na manispaa za jiji la dar es salaam. Wote kwa pamoja walilaumu mfumo wa utungaji wa sheria wa tanzania ambao unatoa fursa kwa taasisi inayotunga sheria kuingiza mambo inavyotaka yawe pekee badala ya kushirikisha wadau waote na kuzingatia hali halisi.

  Walikuwa wakiraehea sheria ya barabara namba 13 ya 2007 ambayo katika siku za hiviu karibuni mhe john magufuli amekuwa akijigamba kuwa aliaapa kuiheshimu na kuhakikisha haichezewi.

  Kitu wote walichosahau kusema kuwa mfumo wa utungaji wetu wa sheria ambao tuliurithi kutoka kwa wakoloni sambamba na katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania hutoa madaraka kwa mawaziri husika kutunga kanuni za sheria husika mara baada ya sheria husika kupitishwa na bunge(annex 1 caption ya sheria hiyo). Hivi sasa anachofanya nacho kazi mhe john magufuli ni kanuni za sheria hiyo zilizopitishwa kupitia tangazo la serikali namba 21 la tar 23 januari 2009 (annex 2 kanuni husika). Hivyo kanuni hizi ni maoni ya wizara yake tu, hakuna mwakilishi wa wananchi (mbunge) hata mmoja aliyehusika katika utungwaji wake

  huu ni utaratibu mbovu kabisa. Ndio maana cahdema inataka kuandikwa upya kwa katiba yetu ili kuondao mapungufu kama haya ambapo viongozi kutoka chama kimoja waziri wa serikali kuu na mameya na wakurugenzi wa manispaa wanalumbana hadharani.

  Pamoja na mapungufu haya mhe john magufuli ana lake jambo katika mabango hayao kwa kuwa alitakiwa kuanza na the most vpressing need, and the most pressing ni magari makubwa na madogo amabayo huharibika na kufanyiwa matengenezao barabarani kinyume na ibara ya 9 (3-4) ya kanuni hizi na amabyo hutelekezwa barabarani kwa masaa na siku kadhaa na kusababisha ajali zinzosababisha vifo k.m katk daraja la kibamba kila wiki lazima itokee ajali au barabara kuzibwa kabisa kutokana na magari kutelekezwa barabarani kwa masaa na hata siku kadhaa. Ibara hii inatoa madaraka kwa tanaroad kuyaondoa magari haya na kuyahifadhi na kumataka mmiliki kulipi gharama husika.

  Mbona hilo halifanyiki?
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nilisahau kupload attachamnets, ndio hizo kama ifuatavyo, caption ya sheria hiyo inayoonysha waziri kupatiw amadaraka ya kutunga kanuni kama ananex 1

  na
  kanuni zenyewe ananex 2

  na nakala ya tangazo la serikali la tar 23 januari 2009 kanuni hizo zilipopitishwa, kwani mhe john magufuli hataki kuzitambua kanuni hizi kwa kuwa wziri aliyemtangulia alipunguza eneo la hifadhi ya barabara kati ya ubungo hadi kiruvia
   

  Attached Files:

Loading...