Mameneja 29 TANESCO wasimamishwa kazi kwa hujuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mameneja 29 TANESCO wasimamishwa kazi kwa hujuma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HUNIJUI, Oct 20, 2012.

 1. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mameneja 29 Tanesco wameshimamishwa kazi baada ya kuhusishwa kuhujumu utendaji wa shirika hilo kwa kuunganisha umeme kinyume cha utaratibu, wizi wa mafuta ya transfoma na nyaya za umeme.

  Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alisema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati yao ya kutoa huduma bora kwa wananchi na operesheni inayoendelea nchini kote ya kuwasaka watu wanaojiunganishia umeme kinyemela.

  "Tanesco ya sasa siyo ile ya zamani. Tunajisafisha na tayari wapo waliochukuliwa hatua na wengine kusimamishwa," alisema lakini akakataa kutaja majina ya vigogo waliosimamishwa.

  Alisema waliosimamishwa kazi ni wenye vyeo vya umeneja na maofisa. Akizungumzia hali ya umeme nchini, Badra alisema hakutakuwa na mgawo wa umeme kwa sababu sasa hivi Tanesco haitegemei zaidi umeme wa maji, isipokuwa wanatumia umeme wa mafuta na gesi.

  "Hakuna mgawo na hatutarajii kuwa na mgawo. Sasa hivi tunatumia umeme wa mafuta na gesi," alisisitiza.

  Kuhusu kukatika kwa umeme katika baadhi ya mikoa, alisema hiyo inatokana na sababu za kupanga wenyewe ili kuruhusu kufanya marekebisho katika njia za umeme au wakati mwingine inatokana na sababu tofauti kama vile mvua za radi, upepo, kukatika kwa miti kunakosababisha kuharibu mfumo wa usambazaji umeme au hata gridi ya taifa kupata matatizo ya kiufundi.

  Katika hatua nyingine, Badra alisema Tanzania inafanya mazungumzo na serikali ya Ethiopia ili kuangalia uwezekano wa kununua umeme kutoka nchi hiyo. "Njia kuu za kusafirisha umeme zitakapounganishwa na kukamilika, nchi yetu itaweza kununua umeme unaozalishwa kwa njia ya maji na unaouzwa kwa bei nafuu moja kwa moja kutoka nchi kama Ethiopia," alisema na kuongeza:

  "Ethiopia wanazalisha nishati ya umeme megawati 10,000 na kubakiwa na ziada ya megawati 8,000."

  Alikuwa akizungumzia mkutano wa mawaziri wa nishati wa nchi za Afrika Mashariki na Kati kuhusu mtandao wa usambazaji wa nishati hiyo unaojulikana kama Eastern Africa Power Pool (EAPP) unaozihusisha nchi 11 za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djibout, Ethiopia, Libya, Jamhuri ya Sudan na Misri.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  porojo hizi.
  hakutaja majina?
   
 3. StayReal

  StayReal JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 519
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  She talks too much this lady Badra!
   
 4. StayReal

  StayReal JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 519
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ndio kawaida yetu mkuu hata usishangae,I wont to be surprised to learn its just a lie!
   
 5. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Wananunua umeme Ethiopia? What a shameful nation full of resources but rich of boguses!
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mameneja 29 sio mchezo
  Tanesco ina mameneja wangapi?
  maybe les than 35 sasa ukisimamisha 29 siio kitu rahisi
  halafu wasitajwe majina?
   
 7. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mameneja 29 ni wachache sana maana mikoa ya kiTANESCO ni 29 yote ina mameneja, wilaya kiTANESCO ziko 72 zote zina mameneja, HQ wako kama 49 shirika lina staff zaidi ya 5,000 mameneja waandamizi wako kama 10,
  So its possible
   
 8. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,312
  Likes Received: 2,973
  Trophy Points: 280
  Kwani hujui anataka viti maalum?
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  yes but mostly hapa tunazungumzia wenye authority za kufanya hizo crime
  hapo unapata wa mikoa na wilaya zaidi...
  hao wa head office sidhani...
   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  moja kati ya mashirika pumbafu kabisa, kila siku kupandisha bei ya umeme kwa faida ya ufisadi wao.

  Wanakwiba mchana kweupe hata aibu hawana na kutuibia zaidi na zaidi visenti vyetu vichache kwa kupandisha bei.

  eti kununua ethipia nani sisi watanzania? aibu na ujinga mwingine ufisadiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 11. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ujinga gani wa kununua umeme ethopia?
  Kwani wao wanazalishaje sisi tushindwe?
  Hawa tanesco ni vimeo wala hawana jipya.
   
 12. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  very poor english.
   
 13. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ngereja hoyeeeeeee?

  V
  SENGEREMA
   
 14. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ebu weka list ya majina yao
   
 15. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Nami nilitaka kumuuliza majina ya hao mameneja yako wapi?
   
 16. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Are they senior manager, I mean head of departments wale wenye parking zao kabisa zimewekwa vibao head office? Au mameneja uchwara...
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Aliyelazimisha mkataba na richmond mpaka leo hajafungwa wadanganyika wanajiunganishia umeme kwa sababu ya urasimu wa tenesco ndo wanabughudhiwa ee Mungu ni lini utaleta gharika I'll mateso tugawanee???
   
 18. hodogo

  hodogo JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 239
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanesco ni shirika kubwa na lina mameneja zaidi ya 100! Hebu hesabu Tanzania Bara ina Mikoa mingapi?

  Kila mkoa una wilaya ngapi za kiserikali na kuna wilaya za kitanesco! Mfano wilaya zote za Dar na baadhi katika miji mikubwa, kitanesco ni Mikoa! na ina wilaya zake si chini ya 2! Kila Mkoa, kila wilaya, na kila kanda, ukiacha mamenja wa kumwaga makao makuu katika sekta mbalimbali!

  Nataka kusemaje, HILO LA BADRA LINAWEZEKANA!
   
 19. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  The Boss, sio uongo, haya ni ya kweli, Waziri wa Nishati alikuwepo pia katika mkutano huo...Baada ya hapo wakaenda kujipongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa mlo wa jioni hotel ya Mlima Meru. Juzi ilikuwa ni Kagasheki (Waziri wa Maliasili na Utalii) kumkaba koo bosi wa TANAPA na kutaka kumpiga chini. Kisa ni mbwa walionunuliwa hapa SA kwa ajili ya kuwafuatilia majangili. Mbwa hao wamefika tu na kabla ya kuanza kazi zao, tayari majangili yalikuwa na taarifa ya kufuatiliwa nyendo zao na kuhusu uwepo wa mbwa hao maalum wenye uwezo mkubwa wa kugundua majangili walipo na bila ya kuwashtua na baadaye huleta taarifa za wapi majangili walipo ili wafuatiliwe...hapo ngoma ilikuwa nzito...Juzi hiyo hiyo Wizara ya Nishati na Madini ikaanza safisha safisha. Jana ndio ilikuwa hitimisho la zoezi zima.

  Vyanzo hivi vya habari: Waandishi wa habari, kama una namba zao wapigie kwani habari zote unaweza zipata zikiwa bado za moto. Pili ni uwepo wako eneo la tukio, tatu ni mtandaoni. Nne ni kama una ukaribu wa kutosha na hao"wakubwa" bila kuwataja majina yao wala kutoa namba zao za simu kwa ajili ya mawasiliano. ZINGATIA SANA.
   
 20. m

  mokti Member

  #20
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ethiopia wanauwezo wa kuzalisha 10,000MW. Tanzania inauwezo wa kuzalisha 1200MW na tunajidai kwamba tunaendeleza nchi. aidha, Ethiopia wakumbana na majanga mengi yakiwemo njaa kali, vita na kadhalika. Ni aibu iliyoje kwa Tanzania.
   
Loading...