Mambosasa: Watu wengi wamejeruhiwa kutokana na kukanyagwa na kukosa hewa wakati wa kuaga Mwili wa Rais Magufuli

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baadhi ya wananchi walioshiriki shughuli ya kumuaga Rais John Magufuli wamejeruhiwa baada ya kukanyagwa na wenzao.

Mambosasa ameeleza hayo leo Jumapili Machi 21, 2021 alipoulizwa na Mwananchi Digital kuhusu taarifa za kuwepo kwa watu waliojeruhiwa na kukimbizwa hospitali katika shughuli hiyo iliyofanyika Uwanja wa Uhuru na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu.

Kutokana na wingi huo, shughuli ya kuaga ilisitishwa saa 9 alasiri na mwili wa kiongozi huyo ukiwa katika gari maalum ulizungushwa mara tano uwanjani hapo ili maelfu ya wananchi wapate fursa ya kuaga baada ya kuomba kutokana na kuelezwa kuwa wote hawataweza kupita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa Magufuli.

Katika maelezo yake Mambosasa amesema idadi kamili ya watu waliojeruhiwa katika shughuli hiyo hana lakini ni wengi.

“Binafsi sina idadi lakini ni watu wengi ambao walikanyagana na kukosa hewa. Walikuwa wanaanguka na kubebwa,” amesema Mambosasa.
 
Kipenzi cha watu enzi za uhai wake ilikuwa ukipatikana Umati kwny Mikutano yake Mawakala wakawa wanasingizia wamenunuliwa

Huyu Mwamba ndio tulidanganywa hakubaliki kaiba kura

Magu anaumbua watu hata baada ya uhai wake

Huyu Mwamba hata Kambarage anasubiri, alikuwa ndio Roosevelt wa Taifa letu
 
Walijitakia kwenda kukanyagana hadi kupoteza maisha. Nawashangaa sana na ujinga huu mkubwa hivi bado maambukizi corona wengi wao hata bila hawana Nasubiri matokeo ya ujinga wa Watanzania walio wengi kweli ujinga umeabakia nchi 2 tu Africa Tanzania na Zimbabwe.
 
Kipenzi cha watu enzi za uhai wake ilikuwa ukipatikana Umati kwny Mikutano yake Mawakala wakawa wanasingizia wamenunuliwa

Huyu Mwamba ndio tulidanganywa hakubaliki kaiba kura

Magu anaumbua watu hata baada ya uhai wake

Huyu Mwamba hata Kambarage anasubiri, alikuwa ndio Roosevelt wa Taifa letu
Haya sawa umesikika. Hata kambarage anasubiri! Vijana wa lumumba mna hatari
 
Mambosasa wengine wameshaona mpaka ripoti zenu mlizoandikiana huko polisi, bora uwe muwazi tu.
 
Back
Top Bottom