Mambosasa, Viongozi wanaojiuzulu baada ya kuharibu au mambo kuwa hovyo ni wabinafsi na woga

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,604
2,000
Kumezuka tabia ya ajabu ya kuiga utamaduni wa matifa ya watu huko kwa wenzetu. Kulazimisha mambo yanapoharibika eti "wajiuzulu" kujiuzulu ni kujidhuru tu hamna haja ya kufanya hivyo kwa sisi binadamu.

Tumesikia finland,tumesikia tunisia.na wengi wamekuwa wakizungumza hayo kila mara kwa viongozi wetu.kujiuzulu ni ishara ya ubinafsi na ukosefu wa fadhila kwa aliyekuchagua.

Wewe hufikirii yeye katika mamilioni ya watu kaona unafaa kupata kula yake katika uongozi, kawaza kawazua,kafikiria kachekecha kapata jibu kuwa wewe ndo unafaa.halafu unakuja kusema unajiuzulu?

Huoni kuwa unaweza umiza hisia zake?huoni kuwa utakuwa umempotezesha muda wake?mimi sishauri mambosasa ajiuzulu hata kidogo.akijiuzulu familia yake itaishije?

Suala la mo dewji lipo lilivyo kungekuwa na uwezekano wa kujulikana kila kitu kungejulikana.lakini kwa kuwa ipo hivyo ilivyo nadhani tuyaache hayo. Na mheshimiwa rais najua linamtesa sana suala hili.

Kama ambavyo namwona halali akiwaza suala la waliomshambulia lissu,waliompoteza ben saa nane na yule mwandishi wa habari wa kibiti.

Hawa walitendewa unyama na watu waovu wenye nia mbaya ya kuipaka serikali yetu tulivu damu na ninaamini siku mh akipata muda atasema neno.

Ila nasisitiza tuacheni roho mbaya za korosho za kushinikiza watu wajiuzulu.hizo ni roho za wakosaji.nyie mnadhani ni rahisi tu kusema najiuzulu?

Halaf akijuzulu aidhuru na familia yake?hawa mawaziri ni image yetu sisi huku tuliowapatia KULA. Unapomwangalia kangi lugola jiangalie na wewe...unapomwangalia mbunge juma nkamia angalia na watu wake jimboni.

Unapomwangalia kibajaji ana akisi watu anaowaongoza waliompa kula.unapomwangalia mkuu wa mkoa angalia ya aliyemweka hapo alipo toka awali.

Tuacheni roho mbaya.mambosasa usijiuzulu,kangi lugola fanya kazi uliyopewa, kigwangala endelea na ulevi wako wa madaraka. Sisi tupo nyuma yako...usitie shaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom