Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Leo sikupanga kuandika jambo lolote sehemu yeyote kwani kwa kawaida leo ni siku yangu ya kujiongezea maarifa kwa maana ni siku yangu ya kuingia Maktaba kujisomea, lakini nimekuta mjadala unaendelea katika sehemu ambayo ninanunua magazeti kila asubuhi, kundi la watu wanajadili kuhusu TAFITI.
Kilichonifanya niandike ni muelekeo wa mjadala huo unaohusu tafiti zilizotoa matokeo yake hivi karibuni..Kila mmoja anajua TWAWEZA wametoa matokeo ya tafiti yao na kuonyesha kuwa MAGUFULI atashinda kwa asilimia 65 na LOWASSA 25%, na kisha Taasisi ya Kimataifa Synovate nayo imetoa matokeo ya tafiti yake na kuonyesha Magufuli atashinda kwa asilimia 62 na Lowassa 26%. Matokeo haya yameleta ukakasi mkubwa kwa Upinzani hasa CHADEMA maana watu kama Zitto ambao ni wapinzani wasomi na wanafanya siasa za mahesabu wamekubali..
Nimeshangazwa na Kundi la Watu ambao wanaonekana kuwa wameenda shule lakini abaa-manthura hakuna kitu kichwani ambao walikuwa wanapinga matokeo ya tafiti hizo kwa kutumia "Eti wanaouita UTAFITI wa Kkoo" na mmoja anatokwa povu anasema nina Digrii lakini sikubali matokeo ya Twaweza ila wale jamaa wa kariakoo wako sahihi kwa sababu wamefanya utafiti kwenye ground kabisa." sikutaka hata kuchangia nikanunua magazeti yangu na kuondoka eneo hilo kwa masikitiko makubwa.
Nikajiuliza hivi hawa watu wanajua maana ya Utafiti..? wanajua maana ya MTAFITI..? na ikiwa mtu mwenye digrii tena anayeishi Dar es salaam bado hajajua maana ya Utafiti na nani mtafiti, hali ya Taifa hili ikoje kwa waliokosa elimu na wanaoishi vijijini..? Sikutegemea kuwa anaweza kuwepo Mtu mwenye akili Timamu tena aliyeenda shule ambae ataamini Utafiti wa Kkoo unaosema LOWASSA atashinda kwa 98% na kupinga tena "serious" kabisa tafiti za TWAWEZA na SYNOVATE..nasikia hata kwenye baadhi ya maofisi mjadala huu uko katika sura hii pia.
Elimu yetu BADO HAIJATUKOMBOA...katika Serikali ijayo na kwa kuwa nitakuwa Bungeni, nitapeleka muswada binafsi ama nitaomba kupitia Chama Serikali ilete Muswada "Maalum" Bungeni wa kujadili ELIMU na HATMA ya Taifa, tufanye Overall reform and rebranding..bado elimu yetu inazalisha MAMBUMBUMBU kupindukia...