Mambo yenye kufikirisha juu ya Hatma ya Taifa letu TANZANIA...Nakubali kuna tatizo kwenye elimu yetu | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yenye kufikirisha juu ya Hatma ya Taifa letu TANZANIA...Nakubali kuna tatizo kwenye elimu yetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 25, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 25, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Leo sikupanga kuandika jambo lolote sehemu yeyote kwani kwa kawaida leo ni siku yangu ya kujiongezea maarifa kwa maana ni siku yangu ya kuingia Maktaba kujisomea, lakini nimekuta mjadala unaendelea katika sehemu ambayo ninanunua magazeti kila asubuhi, kundi la watu wanajadili kuhusu TAFITI.

  Kilichonifanya niandike ni muelekeo wa mjadala huo unaohusu tafiti zilizotoa matokeo yake hivi karibuni..Kila mmoja anajua TWAWEZA wametoa matokeo ya tafiti yao na kuonyesha kuwa MAGUFULI atashinda kwa asilimia 65 na LOWASSA 25%, na kisha Taasisi ya Kimataifa Synovate nayo imetoa matokeo ya tafiti yake na kuonyesha Magufuli atashinda kwa asilimia 62 na Lowassa 26%. Matokeo haya yameleta ukakasi mkubwa kwa Upinzani hasa CHADEMA maana watu kama Zitto ambao ni wapinzani wasomi na wanafanya siasa za mahesabu wamekubali..

  [​IMG]
  Nimeshangazwa na Kundi la Watu ambao wanaonekana kuwa wameenda shule lakini abaa-manthura hakuna kitu kichwani ambao walikuwa wanapinga matokeo ya tafiti hizo kwa kutumia "Eti wanaouita UTAFITI wa Kkoo" na mmoja anatokwa povu anasema nina Digrii lakini sikubali matokeo ya Twaweza ila wale jamaa wa kariakoo wako sahihi kwa sababu wamefanya utafiti kwenye ground kabisa." sikutaka hata kuchangia nikanunua magazeti yangu na kuondoka eneo hilo kwa masikitiko makubwa.

  Nikajiuliza hivi hawa watu wanajua maana ya Utafiti..? wanajua maana ya MTAFITI..? na ikiwa mtu mwenye digrii tena anayeishi Dar es salaam bado hajajua maana ya Utafiti na nani mtafiti, hali ya Taifa hili ikoje kwa waliokosa elimu na wanaoishi vijijini..? Sikutegemea kuwa anaweza kuwepo Mtu mwenye akili Timamu tena aliyeenda shule ambae ataamini Utafiti wa Kkoo unaosema LOWASSA atashinda kwa 98% na kupinga tena "serious" kabisa tafiti za TWAWEZA na SYNOVATE..nasikia hata kwenye baadhi ya maofisi mjadala huu uko katika sura hii pia.

  Elimu yetu BADO HAIJATUKOMBOA...katika Serikali ijayo na kwa kuwa nitakuwa Bungeni, nitapeleka muswada binafsi ama nitaomba kupitia Chama Serikali ilete Muswada "Maalum" Bungeni wa kujadili ELIMU na HATMA ya Taifa, tufanye Overall reform and rebranding..bado elimu yetu inazalisha MAMBUMBUMBU kupindukia...
   
 2. m

  madenge8 JF-Expert Member

  #21
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 19, 2015
  Messages: 441
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  mkuu huyu Juliana tulikua nae mbozi magharibi kwa silinde mwaka 2010,hela tuliyoandaliwa ya chakula na posho kidogo huyu dada na mwenzake mkaka alikua anasoma RUAHA walituibia........leo hapa anajifanya msomi na yeye.............km huyu ataingia bungeni basi ni kwa kigezo cha kuuza mwili na sio utendaj
   
 3. r

  ray jay JF-Expert Member

  #22
  Sep 25, 2015
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 974
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  Bavicha hamna jema..leo July amewapa kick ya Elimu kwanza bado mnamshughulikia..mmetisha.
   
 4. M

  MZALENDO NO.1 JF-Expert Member

  #23
  Sep 25, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 279
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wewe UTAKUWA MBUGE KUPITIA CHAMA KIPI? WEWE NAHISI NI WALE WALE, SO MVUTA KAMBA HUVUTIA UPANDE WAKE! WEWE BORA UNGEENDA KUPEKUA HAYO MAKALABRASHA YAKO BADALA YA KUJA HUKU KUANDIKA VITU AMBAVYO HATA HAVIELEWEKI
   
 5. s

  security guard JF-Expert Member

  #24
  Sep 25, 2015
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  Wewe unaishi Dunia gani...yaani Haujui Juliana yuko Chama gani..sasa tukusaidiaje..?
   
 6. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #25
  Sep 25, 2015
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Eti ni siku ya kujisomea maktaba,.. huna hata aibuna elimu yako ya kujitungia stori za pwagu na pwaguzi!!!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #26
  Oct 8, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,764
  Trophy Points: 280
  Kiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.

  Karibu Boss, Mheshimiwa saba, Bi Juliana Shonza.

  Paskali.
   
 8. Myahudi Jr II

  Myahudi Jr II JF-Expert Member

  #27
  May 2, 2018
  Joined: Jan 7, 2016
  Messages: 3,001
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Kumbe haka kabibi kapo humu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...