Mambo yenye kufikirisha juu ya Hatma ya Taifa letu TANZANIA...Nakubali kuna tatizo kwenye elimu yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yenye kufikirisha juu ya Hatma ya Taifa letu TANZANIA...Nakubali kuna tatizo kwenye elimu yetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 25, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 25, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Leo sikupanga kuandika jambo lolote sehemu yeyote kwani kwa kawaida leo ni siku yangu ya kujiongezea maarifa kwa maana ni siku yangu ya kuingia Maktaba kujisomea, lakini nimekuta mjadala unaendelea katika sehemu ambayo ninanunua magazeti kila asubuhi, kundi la watu wanajadili kuhusu TAFITI.

  Kilichonifanya niandike ni muelekeo wa mjadala huo unaohusu tafiti zilizotoa matokeo yake hivi karibuni..Kila mmoja anajua TWAWEZA wametoa matokeo ya tafiti yao na kuonyesha kuwa MAGUFULI atashinda kwa asilimia 65 na LOWASSA 25%, na kisha Taasisi ya Kimataifa Synovate nayo imetoa matokeo ya tafiti yake na kuonyesha Magufuli atashinda kwa asilimia 62 na Lowassa 26%. Matokeo haya yameleta ukakasi mkubwa kwa Upinzani hasa CHADEMA maana watu kama Zitto ambao ni wapinzani wasomi na wanafanya siasa za mahesabu wamekubali..

  [​IMG]
  Nimeshangazwa na Kundi la Watu ambao wanaonekana kuwa wameenda shule lakini abaa-manthura hakuna kitu kichwani ambao walikuwa wanapinga matokeo ya tafiti hizo kwa kutumia "Eti wanaouita UTAFITI wa Kkoo" na mmoja anatokwa povu anasema nina Digrii lakini sikubali matokeo ya Twaweza ila wale jamaa wa kariakoo wako sahihi kwa sababu wamefanya utafiti kwenye ground kabisa." sikutaka hata kuchangia nikanunua magazeti yangu na kuondoka eneo hilo kwa masikitiko makubwa.

  Nikajiuliza hivi hawa watu wanajua maana ya Utafiti..? wanajua maana ya MTAFITI..? na ikiwa mtu mwenye digrii tena anayeishi Dar es salaam bado hajajua maana ya Utafiti na nani mtafiti, hali ya Taifa hili ikoje kwa waliokosa elimu na wanaoishi vijijini..? Sikutegemea kuwa anaweza kuwepo Mtu mwenye akili Timamu tena aliyeenda shule ambae ataamini Utafiti wa Kkoo unaosema LOWASSA atashinda kwa 98% na kupinga tena "serious" kabisa tafiti za TWAWEZA na SYNOVATE..nasikia hata kwenye baadhi ya maofisi mjadala huu uko katika sura hii pia.

  Elimu yetu BADO HAIJATUKOMBOA...katika Serikali ijayo na kwa kuwa nitakuwa Bungeni, nitapeleka muswada binafsi ama nitaomba kupitia Chama Serikali ilete Muswada "Maalum" Bungeni wa kujadili ELIMU na HATMA ya Taifa, tufanye Overall reform and rebranding..bado elimu yetu inazalisha MAMBUMBUMBU kupindukia...
   
 2. jd41

  jd41 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2015
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 2,608
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  ...kwa hiyo kwako chochote atachosema Zitto unakikubali..,kwangu chochote atachosema Zitto nakipinga,sababu najua nyie ndio wafadhili wake toka enzi za Adam na Hawa..!
  lila na fila...
  #hazitengamani!
   
 3. g

  goodluck5 JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 8, 2014
  Messages: 2,776
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Huna hoja, we endelea kujipendekeza pengine utapewa na ukuu wa mkoa...who knows!
   
 4. Davion Delmonte Jr.

  Davion Delmonte Jr. JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2015
  Joined: Oct 27, 2013
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,022
  Trophy Points: 280
  Yaani mnadharau tafiti za kariakoo. Hizo tafiti zenu mnaziita za kisomi mbona bado zinafanya nchi inakuwa masikini. Tatizo la nyie mnaodhani ni wasomi hapa Tanzania mna tabia ya kujiona kwamba mna haki ya kuongea chochote hata kama ni non-sense.
   
 5. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,466
  Likes Received: 6,773
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe mwenyewe ni mfano wa hadaa katika elimu yetu

  Yaani you are a case study ya mfumo wetu wa elimu mbovu uliosababishwa na serikali ya CCM
   
 6. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa mtu ambaye unajua kwa 100% hawezi pata 2% za kura zote unafikiri ataacha kukubali matokeo! Zitto na chama chake ni kibaraka wa CCM, kwa hiyo kama tafiti zinakipendelea chama cha majambazi (ccm) hana zitto anazikubali kwa sababu yeye ni ccm. Synovate na Twaweza ni matwi ya ccm hakuna asiyejua. Bado kidogo na REDET watakuja na yao maufuli 58%na Lowasa 40% Ila OCT 25 porojo zote zitawaishaa
   
 7. a

  aiai654 JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2015
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,861
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Hao synovate asilimia 41 waliwahoji wakulima, kuna ajabu ipi kwa kuhoji watu wa kariakoo
   
 8. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2015
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 11,505
  Likes Received: 12,585
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa wewe ndio watu waliosababisha tukadharau wasomi. Hivi unaposema tuheshimu mambo yaliyofanywa na wasomi unatufanya sisi ni wajinga wa kiasi hicho. Mikataba yote hii mibovu inayotufanya kila siku tulie imeingiwa na hao watu unaowadharau wa kariakoo? Kwa hiyo wewe baadhi ya wasomi ambao huna shaka nao ni Zitto!!? Ukiona hivyo ujue kwamba hapa tulipofikia tumeona mambo mengi yakuongopea wananchi yakifanywa kwa kigezo cha usomi, zamani tulikuwa tukisikia mtu ni msomi tulikuwa tunampa mpaka akili zetu atushikie. Leo hii mashirika na taasisi nyingi zinazoendeshwa na wasomi ziko taabani kwani hakuna wasomi bali watu waliohudhuria vyuo vikuu. Baada ya sisi wananchi wa wa kawaida kuwastukia nyie mnaojifanya wasomi tumeamua kufanya kivyetu na hakika sasa tunaoana mambo yananyooka. Jaribu kuangalia shughuli nyingi zinazofanywa na watu wachapa kazi fananisha na za wasomi jinsi utakavyoona tofauti kubwa. Ama nikupe mfano mrahisi, leo msomi na asiye msomi wape biashara wafanye halafu njoo ndani ya mwaka utakuta ile ya asiye msomi ndio imefanya kwa ufanisi kuliko inayoongozwa na msomi.

  Kwani nyie mnaojifanya wasomi zaidi ya kuzunguka na bahasha kwenda kuomba kazi za kuajiriwa ni kipi kikubwa mnachofanya? Sana sana mkipata kazi ndio mnaoishia kuiba hela za wananchi wavuja jasho kwa kutengeneza receipt fake ili kujipatia hela kwa njia ya uwizi. Kwa mfano wewe mwenyewe zaidi ya kujipendekeza ili upate madaraka ni mradi gani wenye tija umewahi kusimamia na ukatoa matokeo chanya? Jipime kwa dhamira yako kama kuna chochote tangible unaweza kutuonyesha zaidi ya kujipendekeza ukae ofisini.
   
 9. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,584
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mimi ni wewe ningeishauri serikali iwape elimu ya kutosha vijana wale wa Kariakoo hasa kwenye nyanja za TAFITI.Wameonyesha wanauelewa wa hali ya juu kuliko JM pamoja na TWAWEZA.

  Wamejua hakika nini maana ya TAFITI,wanakosa vitu vichache sana ili wawe wanatafiti bora.Ingekuwa nchi za wenzetu vijana hawa wangepewa elimu zaidi kuwaendeleza kwenye hilo na siyo kuwakamata na kwenda kuwafungulia kesi kama walivyofanya polisi wetu.

  Refer kwa kijana aliyeweza kuiba mamilion Bank ya Sweden na kuzipeleka kwenye account ya baba yake.ALipokamatwa wala serikali haikumpeleka gerezani sababu walijua nini atafanya huko,atawafundisha wengine na wizi ungekuwa mkubwa.

  Walimwajiri,wakaendelea kumsomesha mpaka alipomaliza elimu yake,na kuwa mfanyakazi kamili wa bank.

  Pole,hawa wasio naelimu wanauelewa mkubwa kuliko tunavyofikiri.Tusidhani sababu hajafika chuo kikuu basi ni mburura tu.Ndiyo maana wafanya biashara wazuri ni wale wasio na uwezo wa darasani.Pole mdogo wangu.
   
 10. Chimps

  Chimps JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2015
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 80
  Endeleeni na tafiti zenu feki,
  Lowassa ndo Prezida,
   
 11. SUPER PREDATOR

  SUPER PREDATOR JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2015
  Joined: Apr 29, 2014
  Messages: 2,091
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Juliana shonza bana, sijui yukoje?
   
 12. U

  Undu JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2015
  Joined: May 18, 2013
  Messages: 1,829
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Democrasia africa mashariki ipo Kenya tu basi
   
 13. The Businessman

  The Businessman JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 7,237
  Likes Received: 6,879
  Trophy Points: 280
  Kipaumbele Kikubwa Elimu.
   
 14. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2015
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,945
  Likes Received: 1,694
  Trophy Points: 280
  ...kwa hiyo wewe akiongea zitto ndo wamwona mkweli na msomi???....kwa vile asemacho kinawapa favour nyie basi yeye msomi na mkweli???....alipokuwa zitto anawazodoa na wizi wa hela za escrow mlimwona mwongo na mzandiki.....leo anatetea tafiti inayowapa favour...kawa msomi!...This is idiotic thinking at its best....woote hao twaweza, synovet na hata zitto wanawatumikia nyie ccm....nani asiyejua??...Ni wapi uliona mwanasiasa anayejiita wa upinzani akiwaponda wapinzani wenzake??..nyie wote kitu kimoja na njia moja...
   
 15. MAGALEMWA

  MAGALEMWA JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2015
  Joined: Jul 8, 2015
  Messages: 4,144
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Fyonza wewe na Zitto ni matokeo ya elimu duni inayotolewa na CCM.

  Ungekuwa unaaminika ningekupa namna tafiti tafiti hizi zinavyotumika kuchakachua matokeo halisi. Ukweli unaokiri wa tatizo kwenye elimu ni matokeo ya kugushi kunakofanywa na watawala wote wa CCM kuengua wasomi wa kudumisha ubora na tija, misingi na maadili ya elimu.

  Mimi kama mwalimu niliyeanza kuufundisha 1972 baada ya kumaliza shahada yangu ya Sayansi na Elimu nimeshudia jitihada za CCM kudhoofisha elimu na maadili yake kwa ajili ya kuruhusu watawala wa mifukoni wanaosimikwa na dola kuanzia 1977.

  Tatizo la Elimu limekuwa na mafanikio makubwa pia. Wananchi wakawaida wamekuwa jasiri kuhoji wanachoambiwa kwa sababu hawaridhishwi na hhawayaelewi na hawataelewa maelezo na sera/ahadi zisizotekeleza.

  Wewe na Zitto mlijikita kusaliti CHADEMA kwa elimu mbofu mbofu mliyonayo. Matokeo ya usaliti wenu umeongezea watu kuhoji na kujiunga na CHADEMA. Kumbe hata Dr. Slaa mlikuwa naye kwenye sera za chupi? Naye kaondoka. Ujumbe hata mkipeana PHD za chupi inapokuja kwenye utendaji hamtafua dauu na aina ya elimu iliyoasisiswa na CCM. Watu wataendelea kuwahoji na kuwakataa.

  Kwa taarifa yako kabla ya CCM 1977 elimu Africa Mashariki ilikuwa moja na performance ya Tanzania ilikuwa bora. Kwa elimu ya wakati huo 1972 Tanzania ilikuwa inaongoza elimu na uchumi wa Africa Mashariki

  Hakuna sababu ya kuungama; dawa ni CCM IONDOKE MADARAKANI labda watairudisha TANU
   
 16. J U G A N I A

  J U G A N I A JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2015
  Joined: May 30, 2015
  Messages: 584
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  Tunaowaita wasomi ni wale walioenda shule lakini kichwani hawajaelimika..
  Wangeelimika tungekuwa mbali sana kimaendeleo maana wizara nyingi zinaongozwa na ma-doctor, na ma-prof.
   
 17. MAGALEMWA

  MAGALEMWA JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2015
  Joined: Jul 8, 2015
  Messages: 4,144
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Fyonza wewe na Zitto ni matokeo ya elimu duni inayotolewa na CCM.

  Ungekuwa unaaminika ningekupa namna tafiti tafiti hizi zinavyotumika kuchakachua matokeo halisi. Ukweli unaokiri wa tatizo kwenye elimu ni matokeo ya kugushi kunakofanywa na watawala wote wa CCM kuengua wasomi na kudumisha misingi na maadili ya elimu.

  Mimi kama mwalimu niliyeanza ufundisha 1972 baada ya kumaliza shahada yangu ya Sayansi na Elimu nimeshudia jitihada za CCM kudhoofisha elimu na maadili yake kwa ajili ya kuruhusu watawala wa mifukoni wanaosimikwa na dola.

  Tatizo la Elimu limekuwa na mafanikio makubwa pia. Wananchi wakawaida wamekuwa jasiri kuhoji wanachoambiwa kwa sababu hawaridhishwi na maelezo na sera/ahadi zisizotekeleza.

  Wewe na Zitto mlijikita kusaliti CHADEMA kwa elimu mbofu mbofu uliyonayo matokeo ya usaliti wenu umeongezea watu kuhoji na kujiunga na CHADEMA. Kumbe hata Dr. Slaa mlikuwa naye kwenye sera za chupi? Naye kaondoka. Ujumbe hata mkipeana PHD za chupi inapokuja kwenye utendaji hamtafua damu na aina ya elimu iliyoasisiswa na CCM.

  Kwa taarifa yako kabla ya CCM 1977 elimu Africa Mashariki ilikuwa moja na performance ya Tanzania ilikuwa bora. Kwa elimu ya wakati huo 1972 Tanzania ilikuwa inaongoza uchumi wa Africa Mashariki

  Hakuna sababu ya kuungama dawa ni CCM IONDOKE MADARAKANI labda watairudisha TANU
   
 18. gnassingbe

  gnassingbe JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2015
  Joined: Jun 14, 2015
  Messages: 3,948
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Mchumia tumbo huyo achana nae hiyo elimu anayoinanga na kusema atakwenda bungeni kuirebrand ni matokeo ya utawala wa chama gani.Aisee hizi njaa zitatuua kumbe kuishabikia CCM lengo ni maslahi binafsi ya kwenda bungeni nitamshangaa sana atakayempeleka bungeni huyu.
   
 19. a

  aaamuk JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2015
  Joined: Jan 26, 2015
  Messages: 714
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mleta uzi nakusikitikia hoja yako umeileta kwa watu wenye uelewa mpana. ..kama unasoma kwa rula utajua lengo lako halitatimia
   
 20. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2015
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 27,714
  Likes Received: 47,120
  Trophy Points: 280
  Communication skills yako nayo inaonyesha nawe elimu yako ni mbovu tena sana tu!!

  Angalia ulivyo poor katika "punctuation" kwenye bandiko lako alafu unadharau wenzako!!


  Hata kuweka "comma" kunakostahili hujui alafu unajifanya umeenda shule kiasi cha kudharau wengine?!

  Wote tuna uwalakini ila kwasababu wewe unajifanya mjuaji,ndio maana nimeyasema haya.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...