VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Siasani chezea vyote, si uzee. Uzee husheheni taarifa, maarifa; busara zisizo na hasara; ujuzi muhimu kama mchuzi na staha kama star. Uzee huonsha ukomavu na ubobevu wenye ushupavu. Uzee huelekeza kusema pa kusema na kunyamaza pa kunyamaza. Uzee hupunguza na kuepuka roporopo na upopo.
Wale 'wachochezi wa kuchonga' ndani ya CCM wameanza kuchoka na kuchokwa. Wanaongozwa na yule aitwaye Cyprian Musiba anayejibanza kwenye Uanaharakati Huru. Amini nawaambieni, Musiba ameanza kuchoka. Anapigia simu na kuwatumia ujumbe makada wazoefu chamani akiwaomba uungwaji mkono.
Hata baadhi ya Wabunge na Wanachama wengineo 'walioingizwa mkenge' na kujazwa wenge na Musiba nao wamechoka kama mwisho wa mwaka. Wanateswa na busara ya uzee ya kukaa kimya. Wanajilaumu kuropoka mapema bila kuhema na wala kutazama adhima ya roporopo yao kwa makini. Wamejikuta wameumbuka.
Niliwaambia, Wazee wa chama tutajipanga na kupangika kama maji na bila kumwagika. Tulianza na gia-ya-kimyakimya. Kukaa kimya ni kupuuza na kuumiza. Mipango inaendelea kusukwa kuelekea kusambaratisha wanafiki wasio marafiki kwa Rais na Mwenyekiti wetu. Wanaojichora kwa ukora wa kumtetea na kumpigania.
Wazee tumeanza kwa kunyamaza, chama kitatikisika tukianza kuijibu 'CCM mpya'. Tusiendelee kuchokozwa kwa mustakabali wa chama!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kasulu, Kigoma)