Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Pengine wapo watu hawaelewi maana ya teuzi za mawaziri na namna zinavyoweza kubadilisha mambo.
Ngoja niwaeleze...
Mawaziri ni influencers na watekelezaji wa sera. Sera ndizo zinazoendesha mambo mengi kama sio yote kwenye sekta mbalimbali. Hakuna linaloenda bila ya sera, hivyo sera zikiwa nzuri basi mambo yanakuwa mazuri, zikiwa mbaya ni majanga.
Kijana Innocent Bashungwa amepewa dhamana ya kuongoza wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo. Sekta ya habari, sanaa na michezo imeajiri na inaendelea kuajiri vijana wengi wa kileo. Huyu kwa wenzangu na mie tunaokutana koridoz tunamjua ni kijana wa aina gani. Kwa ufupi tu ni msomi na mjanja.
Pia anajua anachotakiwa kufanya na yuko serious kwenye kupata matokeo. Hana mitazamo ya "kizee" na sio "mshamba" wala "limbukeni". Kwenye haya mabalaa ya kanuni za maudhui na unyanyasaji wa wanahabari atatufaa sana. Huko kwenye sanaa na michezo amuachie Ulega. Ndio mambo yake.
Kaka yetu Faustine Ndugulile kapewa wizara mpya na nyeti - TEHAMA. Wizara hii haikuwepo japo imehitajika kwa muda mrefu sasa. Alivyo msomi, principled na kijana wa vijana hasa huku mitandaoni, naweza hata kumuwekea dhamana kuwa atatubeba sana tu. Bahati nzuri sio mtu wa kupokea pokea maagizo kutoka juu.
Na mpaka Magufuli anawateua hawa "vichwa ngumu" maana yake kuna mambo anataka kuona yanaenda bila kujipendekeza kwake.
Kikubwa cha kuombea ni hawa vijana, watoto wa mjini, watengeneze couple ya kiutendaji. Sina shaka wakifanya hivyo mambo yataenda tu.