Mambo yasiyo ya kawaida yanastahili kushughuliwa kwa mikakati isiyo ya kawaida! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yasiyo ya kawaida yanastahili kushughuliwa kwa mikakati isiyo ya kawaida!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Dec 18, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kusema kweli hawa mafisadi wana bahati kwamba Tikerra sio rais wa Tanzania, kwanza sitakuwa, kwasababu hata huo upenyo wenyewe wa kufika huko nitaupata wapi maskini. Na kusema kweli kabisa, maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu, hata kama upenyo huo ningeupata, nisingekubali kabisa kuingoza Tanzania.

  Mmmm! Inatisha wenzangu. Lakini nisemalo ni lipi, nasema hiviii, mambo yanayotokea sasa Tanzania sio ya kawaida. Nikisema mambo yanayotokea Tanzania, nina maana pamoja na ufisadi, tena ufisadi wa kutisha. Sasa ufisadi huu sio wa kawaida kabisa, sasa mantiki ya kuushughulikia kwa kutumia mbinu za kawaida hasa ni nini?

  Nakumbuka Mchonga alitumia mbinu sizizo za kawaida, kamata weka ndani, ukitoka viboko ukamsimulie mkeo. Mantiki yake ilikuwa hii: kwamba mambo yasiyo ya kawaida yanahitaji kushughulikiwa kwa mbinu zisizo za kawaida. Hivi kinachoshindikana leo ni nini?

  Unashukiwa wewe ni fisadi unakamatwa unawekwa ndani usivuruge uchunguzi. Halafu usalama wa taifa pamoja na wataalam wengine wanatumika kutengeneza "balance sheet" ya mapata yako halali Vs. rasilimali zako. Ikionekana rasilimali zako zimezidi kipato chako halali unahukumiwa moja kwa moja. Kwangu mimi huu ni ushahidi tosha kwamba wewe ni fisadi.

  Kwakweli bado mpaka sasa haingii akilini mwangu kwanini majitu haya ambayo yamesababishia taifa letu hasara kubwa kiasi hicho bado tunayawapa heshima kiasi hicho. Jamani, mbona yenyewe hayakutuheshimu? Kikwete yakamate yote, funga, halafu yakitoka piga viboko yakawaambie wake zao!
   
Loading...