Mambo yanayotuunganisha watanzania ni yepi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yanayotuunganisha watanzania ni yepi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shibalanga, Jun 3, 2011.

 1. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu, naomba tusaidiane kwa pamoja kutambua mambo ambayo sisi kama watanzania bila kujali itikadi za siasa, dini, Rangi, kabila,kanda na jinsia; mwisho wa siku yanaturudisha pamoja kama wananchi wazalendo wa nchi hii.

  Binafsi, nimekuwa nikijiuliza sana swali hili nakosa jibu, na hii ni kutokana kushuhudia minyukano ya kisiasa, kidini, kiuchumi na kitabaka ambayo hali hii imepelekea sasa kila kukicha ni malalamiko,maandamano,tuhuma, mauaji, vitisho, ubabe; Kiasi kwamba inataka kuonekana kana kwamba Tanzania si pahala pazuri pa kuishi.

  Ndugu zangu, najua humu kuna watu makini sana waliobobea katika nyanja mbalimbali na kutokana na umuhimu huo mlio nao hebu kwa pamoja tutambue ni mambo gani ambayo mwisho wa siku sitakuwa na haja ya kutambua huyu ni wa CUF, CHADEMA,CCM, MWISLAM, MKRISTO, MPAGANI, KIJANA, MZEE, MTOTO, PROFESA,MKULIMA N.K lakini tunakuwa kitu kimoja?
  Nisaidieni tafadhali.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kinachotuunganisha ni umbeya na kupenda ngono
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kISWAHILI WAKATI FULANI SASA KINAPOTEA! UTAIFA UMEPOTEA (Chenge anataka DOWAN walipwe) sioni kilicho baki cha kutuunganisha watz
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kupiga domo

  ubishi

  na kulalamika na hivi platform kama JF tunayo ndio zaidi!
   
 5. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Yapo mengi cha msingi ni kujiuliza kutuunganisha katika lipi?
  Kuna wakati watu wa itikadi na vyama tofauti tunaunganishwa na mpira.
  Kuna wakati watu wa timu tofauti tunaunganishwa na dini.
  Kuna wakati watu wa dini tofauti tunaunganishwa na siasa.
  Hayo hapo juu pia ukiamua kuyageuza unavyotaka bado yataleta maana ileile.
  Pia ukiyatazama kwa upande wa pili yanayotuunganisha na huyu ndiyo yanayotutenganisha na yule.
   
 6. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Cha kutuunganisha ni "Utanzania", na kiswahili ndo fahari yetu. Tutatofautiana katika mambo mengi sana, ila mwisho wa siku sote tutabaki kuwa ni watanzania na tutaimba kwa pamoja wimbo wetu wa taifa la Tanzania katika lugha yetu ya kiswahili.
   
 7. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kilichotuunganisha ni aina fulani ya system ya maisha ya kila siku aliyoanzisha mwalimu,maisha fulani ya ujamaa!
  Hiyo ladha ilianza kupotea wakati wa Mkapa, awamu hii ya nne ndo kabisaaaaaa!!!
  Nguvu za giza nyingi imetawala live.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  kitchenpart
  ubatizo
  harusi
  graduation
  maneno mengi
  ujuaji
   
 9. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  njaa ndo inatuunganisha
  uchaguzi pia hasa wakati wa kampeni
  lakini simba na yanga vinatukusanya na kututenganisha
   
 10. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  bia imeniunganisha na wat kibao lakini
   
 11. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Asanteni! kama hayo mliyoyasema ndo yanatuunganisha sawa, nyie si ndo wataalam bwana niliowahitaji!
   
Loading...