Mambo yanayosababisha gari kutumia mafuta mengi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Mafuta ni kimiminika muhimu kuliko vitu vyote katika gari. Ili gari liweze kufanya shughuli zake zilizokusudiwa ni lazima liwe na mafuta. Uwepo wa mafuta hulifanya gari kutekeleza majukumu yake kama vile kuiwezesha mifumo mbalimbali ya gari kufanya kazi kwa ufasaha na kulifanya gari kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Kwa kawaida kila gari hutumia kiwango fulani cha mafuta kwa kilomita moja, kulingana na ukubwa wa injini na umri wa gari lenyewe. Ikiwa gari linatumia mafuta zaidi ya kiwango ilichotakiwa kutumia kwa umbali fulani, basi yawezekana kuna tatizo linalosababisha kuongezeka kwa kiwango cha mafuta kitumiwacho.

Mkurugenzi Mkuu wa Evolution Garage, Evodius Alex anaeleza ni vitu gani ambavyo husababisha gari kutumia mafuta mengi.

Kuchoka kwa Plug

Ni muhimu kubadilisha plugs kwa wakati hasa zikianza kuonyesha hitilafu, mfano gari kutetemeka kwa mbali na hata wakati mwingine zikitumika kwa miezi 6 mpaka mwaka mmoja au zaidi ya kilomita 15000. Plugs huhusika katika uchomaji wa mafuta hivyo uchakavu au kuchoka kwa vifaa hivi huchangia kwa kiasi kikubwa ulaji wa mafuta kwa kiwango kikubwa katika gari.

Matatizo ya umeme katika gari.

Kama gari lina tatizo la umeme, mfano linazimika kila mara, au sensor mbovu au linaonyesha check engine katika dashboard na haujaangalia matatizo haya husababisha gari kula mafuta mengi zaidi. Hii ina maanisha kwamba gari haliko vizuri kaatika mfumo wake wa umeme na hivyo husababisha kutumia mafuta zaidi ukizingatia umeme ni sawa na damu katika mwili wa binadamu. Ni muhimu kuwaona wataalamu wa magari wapime na Diagnosis mashine kujua tatizo lake ili kuepuka ulaji wa mafuta zaidi.

Aidha kama gari lina tatizo la mechanics katika injini, mfano linapandisha joto kila mara ni muhimu kushughulikia tatizo hilo mapema. Ni muhimu pia kujua kiwango cha juu cha joto la gari yako ili utambue kwa haraka joto likizidi kuliko kawaida. Joto likizidi husababisha gari kutumia mafuta mengi zaidi kutokana na kukosa nguvu halisi ya injini. Kuna vitu vingine vya kuangalia kama vile Piston, kiwango cha maji ya Radiator (coolant), ufanyaji kazi wa feni na Thermostat (cooling system).

Kiwango cha RPM anachotumia dereva

RPM ni mzunguko wa injini kwa kipimo cha dakika (Revolution Per Minute). Endapo dereva atakuwa na tabia ya kupenda kukanyaga mafuta zaidi, hii nayo husababisha gari kutumia mafuta mengi hasa magari ya manual. Ni muhimu kuzingatia mafuta unayokanyaga. Matumizi makubwa ya RPM yanaweza kuongeza hadi 3% zaidi ya kawaida. Aidha ni muhimu pia kurekebisha level ya RPM yako hasa unapowasha gari. Magari mengi, RPM zipo katika range ya (0-1) na si zaidi ya hapo pindi tu unapoliwasha. Ukiona mshale wako wa RPM uko juu ya moja na kuendelea wakati gari halitembei, ujue gari linatumia mafuta zaidi ya kawaida.

Matumizi ya Overdrive (OD) kwenye Magari Automatic

Image result for overdrive button

Hii nayo husababisha ulaji wa mafuta, ni kweli ukiweka overdrive gari inakuwa nzito na inavuta sana. Unashauriwa kutumia katika safari ndefu, wakati unataka kuovertake au gari inaposinzia kwenye mlima. Kwenye tope au mchanga tumia D2 au Low-L na baada ya hapo rudisha katika Drive ya kawaida-D. katika maeneo ya mjini usitumie OD kwani itaongeza ulaji wa mafuta sana, yaani inatakiwa kuwa ON, dashboard light itakuwa OFF. OD ON inamaanisha kuweka gia za juu haraka na kupunguza kutumia gia kubwa (za chini) katika matumizi ya kawaida na OD OFF ni kupangua gia, inamaanisha kutoka gia ya juu ili uvute kasi na moja kwa moja utaongeza spidi ya injini (RPM) na kasi na pia itakula mafuta zaidi.

Kufahamu Uwezo wa gari yako, ukubwa na umri wa injini

Unatakiwa kuifahamu gari yako kwa kina kuhusu matumizi ya mafuta, ukubwa wa injini, Mileage na vitu vingine. Hii itakusaidia kuepuka matumizi makubwa ya mafuta katika gari lako.

Pia ni muhimu kufahamu umri wa injini yako pamoja na kufanyia engine overhaul au kubadili mnyororo wake kila baada ya kilomita 100,000, ili kuepuka matumizi makubwa ya mafuta. Kwa kawaida injini inapoanza kuchoka kutokana na kutumika kwa muda mrefu huwa ina tabia ya ulaji wa mafuta.

Kufanya matengenezo kwa wakati

Hiki ni kitu muhimu katika kupunguza ulaji wa mafuta wa kiwango cha juu katika gari yako. Unashauriwa kufanyia matengenezo gari lako kwa kubadilisha mafuta na filters kwa wakati. Kuendesha gari zaidi ya kiwango kilichopangwa kulingana na oil unayotumia inaweza kusababisha ulaji wa mafuta. Ni muhimu pia kutumia oil nzuri na sahihi kwa gari yako. Kuna oil za kilomita nyingi kama vile km 5000 na zaidi. na pia ni muhimu kufahamu vilainishi (Lubricants) sahihi vya gari lako.

Ili kufahamu dereva wako anaendesha katika utulivu na ustadi wa namna gani, unashauriwa kupima kiwango cha mwendokasi (Cruise control) cha dereva husika, hii itakusaidia kufahamu hasa matumizi mazuri ya mafuta. Kwa madereva wa magari makubwa ni muhimu kuendesha gari katika wastani wa spidi ya 25% ya spidi ya jumla ya gari (speedometer readings).

Chanzo: Mwananchi
 
Hapa"

Matumizi ya Overdrive (OD) kwenye Magari Automatic

Image result for overdrive button

Hii nayo husababisha ulaji wa mafuta, ni kweli ukiweka overdrive gari inakuwa nzito na inavuta sana. Unashauriwa kutumia katika safari ndefu, wakati unataka kuovertake au gari inaposinzia kwenye mlima. Kwenye tope au mchanga tumia D2 au Low-L na baada ya hapo rudisha katika Drive ya kawaida-D. katika maeneo ya mjini usitumie OD kwani itaongeza ulaji wa mafuta sana, yaani inatakiwa kuwa ON, dashboard light itakuwa OFF. OD ON inamaanisha kuweka gia za juu haraka na kupunguza kutumia gia kubwa (za chini) katika matumizi ya kawaida na OD OFF ni kupangua gia, inamaanisha kutoka gia ya juu ili uvute kasi na moja kwa moja utaongeza spidi ya injini (RPM) na kasi na pia itakula mafuta zaidi


Nadhan hapo juu panahitaji maelezo mapya maana bado hayaja kaa sawa kuhusu hiyo O/D
 
Na kuhusu Nozzle kuchoka inaweza kua sababu ya gari kutumia mafuta mengi?
 
Asante sana mwalimu....

Mimi naomba kufahamu mambo machache kuhusu gari kuchoka na kuwa kisababisho cha excessive fuel consumption....

å Gari ikiwa na umri gani injini yake itakuwa imechoka na hivyo kutumia mafuta ya kiwango cha juu kuliko kawaida yake?

å Umri wa gari tunaupimaje? Je, tunaangalia mwendo iliyokwisha kutembea (Mileage) au umri wa gari tangu kutengenezwa kwake?

å Kama kigezo ni umbali (Mileage) iliyokwisha kutembea gari; Then, ni km/mile ngapi ndiyo naweza kuhesabu kuwa injini hii imechoka?

å Kama kuchoka kigezo chake umri wa gari/engine;

Ni umri gani basi kitaalamu wa injini ya gari unaihesabu gari husika imekwisha kuchoka haifai?
 
Back
Top Bottom