Babe la mji
JF-Expert Member
- Dec 14, 2019
- 982
- 2,051
- Bei ya mafuta ya petrol kupanda hadi kuvunja rekodi ya tangu tupate uhuru, leo hii kwa Dar ni sh 2510 kwa lita.
- Mgao wa umeme
- Mgao wa maji
- Kipanda kwa vifaa vya ujenzi
- Gharama za maisha Kupanda maladufu eg, sabuni, mafuta ya kula nk
- Maisha magumu
- Mgogoro wa kisiasa hasa swala la Mbowe na Rais kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia mikitano ya kisiasa wakati ipo kwa mujibu wa katiba
- Swala la katiba mpya
- Gesi Kipanda bei
Pia kunatakiwa kuwe na maridhiano ya kitaifa ili tuwe na umoja kama Taifa moja. Kuendelea kulumbana na kutunishiana misuli sio Suluhu kwa umoja wa nchi yetu.
Pia nawaomba viongozi wa dini zote kupitia taasisi zao kama vile Bakwata na TEC nk mmshauri Rais juu ya kukutana na vyama vyote vya kisiasa ili tupate majawabu ya mkwamo wa kisiasa uliopo nchini.
Tanzania ni ya Watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama hivo basi kama tunaipenda nchi yetu basi tunatakiwa kuwa wamoja bila kibaguana hasa kufata katiba. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA