Mambo yanayofanya watu wajue matokeo ya uchaguzi kabla ya uchaguzi kamili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yanayofanya watu wajue matokeo ya uchaguzi kabla ya uchaguzi kamili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 19, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi Unaofanyika Tanzania sio wa kwanza. Pia uchaguzi wa Tanzania ni sehemu ya chaguzi nyingi zilizofanyika duniani.
  Mtu wa kawaida anaweza kuchunguza mambo machache yafuatayo na akajua matokeo.
  1. Vijana ambao mara zote ni wengi kuliko watu wa umri mkubwa wanayemuunga mkono huwa anapata asilimia kubwa ya uhakika wa kushinda ( ilikuwa hivyo kwa Obama)

  2. Vyombo vya huru vya habari vinapomuunga mkono mgombea mara nyingi humpa mgombea asilimia kubwa ya kufanikiwa ushindi ( Ninazungumzia vyombo huru) Ilikuwa hivyo kwa Obama.

  3. Watu wanapokuwa wamechoka na kisha akatokea mmoja anayeonyesha kuweza kuleta mabadiliko inakuwa ni rahisi kwa yule aliyejipambanua wazi kama mwenye nia ya dhati ya mabadiliko kupata wingi wa kura. Watanzania wako zaidi ya kuchoka. ( Ilikuwa hivyo kwa OBAMA)
  4. Watu wanapokuwa na mwamko mkubwa wa kutaka kushiriki katika kuyaleta mabadiliko hayo basi yeyote anayeungwa mkono anakuwa na uhakika mkubwa wa kushinda kura.

  5. Mahudhurio ya mikutano ya kampeni yanapokuwa ni ya kuwa na shauku ya kuhudhuria na sio kubebwa au kulipwa. Panapoonekana ari ya kweli ya kumsikiliza mgombea basi yule anayesikilizwa na umati mkubwa unaoenda kwa ushawishi tu wa kumsikiliza mgombea, basi huyo anayesikilizwa

  6. Upande wa kupoteza nao huwa na dalili za wazi za kupoteza. Dalili mojawapo ni pale wanapotafuta njia mbovu hata za kuhatarisha umoja na usalama. Inapotokea njia hizo zikatumiwa na bado moto wa mabadiliko ukaendelea kuwaka basi ni vizuri upande wa kushindwa ukajiweka tayari KUKUBALI YAISHE.
  Ilikuwa hivyo kwa OBAMA. Walimuita Muislamu kwani wengi wa wamarekani sio waislamu na walikuwa na picha mbaya ya uislamu. Walimhusisha na Mchungaji aliyekuwa ametoa maneno makali ya kibaguzi na ya kuhatarisha usalama.
  Naunganisha na haya hapa chini kuonyesha kuwa CCM imejaribu yote hayo hapo lakini watu wamezidi kuunga mkono.


  NINAAMINI TENA KUWA HUU UCHAGUZI UTAKUWA WA KUSHANGAZA NAANZA KUAMINI MANENO YA WALE VIONGOZI WA DINI.
  1. KILA MTI WALIOUSHIKA CCM KWA NIA MBAYA UMETELEZA NA WAMEKUTA INA MIIBA
  A. Kumchafua Dr. Slaa kwa habari ya maisha binafsi kumempandisha chati mara dufu
  B. Kuzuia wagombea wasishiriki mdahalo kumewatangaza wapinzani na kumewafanya iwe kama CCM hawagombei mwaka huu wanasindikiza tu.
  C. Kule kujaribu kusambaza ujumbe wa simu kumegeuka kuwa hasara na majuto. Hasara ni nyingi.
  Kama upelelezi utaenda vizuri kutawaweka wengi mahali pabaya kwani sasa mwenyewe amepatikana. Mgombea urais ameanza kuhusishwa na ukaribu na watu hawa. Hata kampuni ya Vodacom wengine wameshajitoa kwa kujua kumbe inaweza kutumika kwa jinsi hizo. Mimi ni mteja wao wa postpaid wamenikosa na wamelikosa shirika ninalolisimamia - wenzangu hawapendi niendelee nao hata wao wanajitoa kwani wamethibitisha sio makini.) Kuna siku watajachochea makubwa zaidi.

  2. KILA SHOKA LILILOKAMATWA KUTAKA KUWAKATA WAPINZANI MIPINI IMENG'OOKA WAMEBAKI NA MIPINI NA WAPINZANI WAMEKAMATA SHOKA.

  A. Kule kuwatishia wafanyakazi kwa ukali na kuwahakikishia kuwa haitawezekana kusikiliza kilio chao na kisha kukataa kura zao. Imekuwa kazi kuziomba tena kura hizo za wafanyakazi.
  Nadhani hawakukumbuka kuwa wafanyakazi ni Waalimu, Polisi, Mahakimu, Wasimamizi wa uchaguzi, Mashushushu, madaktari, wauguzi, na taaluma nyingi. Na kwa bahati mbaya badala ya kuwaomba radhi bado ni kama kauli hiyo imetaka ionekana kuwa ni sawa.

  B. Kule kuwapitisha na kuwakampenia watuhumiwa wa ufisadi kwa woga wa kupoteza majimbo yao kwa upinzani kumeongeza hasira za watu na kuongeza umuhimu wa kuleta mabadiliko ya haraka.

  Kwa sababu za kushangaza na kwa kurudia rudia wagonjwa wa Ukimwi wameendelea kuitwa ni kiherehere chao.

  3. MATAMKO YA KUSHANGAZA NA KUSHINDWA KUKANUSHA KAULI TATA.
  A. Mgombea urais wa CCM kutokukanusha ulinzi wa majini juu ya mgombea wa uraisi kwa ccm , kumewaudhi sana wacha Mungu na kuwakatisha tamaa hata wana CCM wacha Mungu. Kwa sasa kituko chochote kinahusishwa na aidha ushirikina au ushauri wa kishirikina.

  B. Kung'ang'ania kuwaita wenye ugonjwa wa ukimwi ni kiherehere chao kumewafanya wengi kuona wamenyanyapaliwa au kuna saikolojia inatumika.

  C. Kusema wanaopata mimba mashuleni ni kiherehere chao kumeleta uchungu kwa watu wengi waliotarajia maneno ya faraja na ya matumaini.

  HII SIO KUTAKA KWA VIONGOZI MUNGU HUWA WAKATI WA MWISHO WA KITU UKIFIKA HATA UKILAZIMISHA UTALETA HASARA MBAYA ZAIDI.
  Wale waliomlaumu Katibu mkuu na kusema anasambaratisha chama sio kweli. Ni wakati wa kusambaratika tu umefika hata angekuwepo nani huwezi kuzuia. Nawahimiza walioko madarakani waruhusu Mungu apitishe upepo wake. HAUZUILIKI. WENYE HEKIMA WASIUPINGE UPEPO UTAWAVUNJA. JIUNGE NAO.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Na kura wanazotaka kuiba nazo zinazidi kunogesha ngoma ya uchaguzi.
   
 3. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Life is process... huu ndo wakati wa watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini kuelekea kwenye mafuriko ya maendeleo... Chagua CHADEMA CHAGUA SLAA...
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kwa nini ushindi usiwe wazi?
   
 5. manchester

  manchester Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ...Ndio Mtaka haki uliyoyasema yote ni ya kweli kabisa na yana sesne katika mtu mwenye akili timamu na mwenye kuitakia mema Nchi yake na vizazi vijavyo (Baba zetu, Bibi Zetu,Babu Zetu,Mama Zetu, Wajomba Zetu, shangazi zetu na watoto wetu pia) yana Mantiki kubwa yanani KUBWA SANAAAAAA Kaka yangu....Kwa kweli uki- uliza ya kuwa mara yangu mwisho kuhudhuria kampeni za chaguzi sa kisiasa kwa mara ya mwisho kuhudhuria sina hata kumbukumbu hiyo kama nilishawahi kufanya hivyo.... Yote hiyo si kwa sababu nilikuwa nimekata tamaa ila leo niulize Kampeni ya mtetezi wa kweli wa Kizai hiki na kijasho ambaye ana uwezo wa kusimama na kuleta wa kuleta mabadiliko ya Nchi ni lini sitashindwa kukuambia hata kama utanikurupusha usingizini sitashindwa kufanya hivyo....Mweye haki kwa Taarifa yako tuu Kuanzia tarehe 28-30 October...Nakuambia hata kama nikufukuzwa kazi acha iwe hivyo ila Sipo tayari kukosa Kampeni hizi na kilele cha kampeni Tarehe 30 Octoba nikiwa mbele kabisa kumsikiliza Raisi wa Mabadiliko pale Kawe katika viwanja vya TANGANGANYIKA PARKERS BWANA!!!!!!!!!! UKO HAPO???
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Jk na CCM ni vyema wakajiandaa kukubali matakwa ya wapigakura na yakaishiia salama. Tusingependa Moreno Ocampo na majemedari wake wa ICC wakamweka JK na maswahiba wake mkononi kwa kuchezea kamari nguvu ya wananchi..............
   
Loading...