Uchaguzi 2020 Mambo yamegeuka: CCM inafanya kampeni kama ndio inatafuta kushika dola kwa mara ya kwanza; dhana ya Bashiru kutumia dola kushinda uchaguzi yafeli

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,485
2,330
CCM walijiamisha kuwa wameua upinzani kwa manunuzi ya waunga juhudi, walifikiri kwa kufanya hivyo wananchi watachukia vyama vya upinzani.

CCM walijiaminisha kuwa kampeni zitakuwa mteremko kwa kuonyesha madaraja na ndege, kumbe kuna kitu zaidi ya ndege wananchi wanakihitaji.

CCM walijiamisha kuzuia mikutano ya wapinzani na vikao vyao vya ndani kutaua upinzani na 2020 mambo yatakuwa mteremko.

CCM walijiaminisha katika dhana ya Bashiru kutumia dola kupata dola. Wakajua 2020 bonge la mteremko.

Kwanini nasema waliamini hivi? Matendo na kauli za viongozi wa serikali na CCM zilituonyesha mapema, kwa miaka hii mitano walikuwa wanaenenda kama 2020 hakutakuwa na uchaguzi na kama upo hakuna cha kuwazuia. Wasijue wananchi tumekata tamaa na maisha, tuko radhi kuchagua mawe kuliko watu. TL sio maarufu kihivyo ila tatizo wananchi tumechoka.

Ukiangalia kampeni za wagombea wa CCM ni kama ndio wanatafuta kukamata serikali kwa mara ya kwanza na CHADEMA ndio wanapigania kuongeza 5 mingine.

CCM wasipobadili strategy hawatoboi kwenye sanduku la kura. Hakuna rangi wataacha kuona mwaka huu. TL kwa bara na Maalim kwa zanzibar hawa ni wapinzani kweli na wasioogopa chochote, hii combinenga ya safari hii ni hatari wasifikirie kuiba kura kabisa option hii haipo kabisa.
 
Hiki Ni kipindi Cha Kampeni kwahiyo lazima Kila chama lazima kioneshe ushindani hasa hivi vyama vikuu vitatu.

Halafu nature ya mgombea wa Urais CCM ni mtu wa kutumia nguvu na anapenda mishe mishe za majukwaani Kama hizo.

Ikumbukwe hata uchaguzi wa 2015 mgombea huyo wa CCM ndo aliongoza kutumia hp za mwili nyingi kuliko mgombea wa chama chochote kile, kwa kuzungukia majimbo yote Tanzania isipokuwa mawili tu(Ukerewe na ukara) plus kupiga push up majukwaani.

Hivyo Basi hata kwasasa CCM inaonekana Kama inatumia nguvu sababu na tabia asilia aliyo nayo mgombea wao.
 
Rais anasema aling'ang'anizwa alikuwa anabeep ikang'ang'ania huko huko.

Baada ya kufika Ikulu akajipanga kwa lengo kuu moja tu kwa miaka mitano.
KUUFUTA UPINZANI.
.Akawanyima uhuru wa kisiasa kwa kuisigina katiba aliyoapa kuzuia mikutano ya siasa kwa miaka 5.
.Akawabambikizia wapinzani kesi na vifungo kila kona ya nchi.
.Akajaribu kuwapoteza baadhi waliokuwa wanampinga.
.Akafikia hatua ya kuwavunja viungo baadhi ya wanasiasa,mbowe mdee lissu.
.Vitisho na kuteka baadhi ya wapinzani.
.Amenunua wabunge na madiwani kila kona kwa kudai eti wameunga juhudi.

ALIJITAHIDI KUUA UPINZANI LAKINI AMESHINDWA HAKUJUA UPINZANI UPO MIOYONI MWA WATU

UPINZANI SIO CHAMA UPINZANI NI ROHO.
 
CCM walijiamisha kuwa wameua upinzani kwa manunuzi ya waunga juhudi, walifikiri kwa kufanya hivyo wananchi watachukia vyama vya upinzani.

CCM walijiaminisha kuwa kampeni zitakuwa mteremko kwa kuonyesha madaraja na ndege, kumbe kuna kitu zaidi ya ndege wananchi wanakihitaji.

CCM walijiamisha kuzuia mikutano ya wapinzani na vikao vyao vya ndani kutaua upinzani na 2020 mambo yatakuwa mteremko.

CCM walijiaminisha katika dhana ya Bashiru kutumia dola kupata dola. Wakajua 2020 bonge la mteremko.

Kwanini nasema waliamini hivi? Matendo na kauli za viongozi wa serikali na CCM zilituonyesha mapema, kwa miaka hii mitano walikuwa wanaenenda kama 2020 hakutakuwa na uchaguzi na kama upo hakuna cha kuwazuia. Wasijue wananchi tumekata tamaa na maisha, tuko radhi kuchagua mawe kuliko watu. TL sio maarufu kihivyo ila tatizo wananchi tumechoka.

Ukiangalia kampeni za wagombea wa CCM ni kama ndio wanatafuta kukamata serikali kwa mara ya kwanza na CHADEMA ndio wanapigania kuongeza 5 mingine.

CCM wasipobadili strategy hawatoboi kwenye sanduku la kura. Hakuna rangi wataacha kuona mwaka huu. TL kwa bara na Maalim kwa zanzibar hawa ni wapinzani kweli na wasioogopa chochote, hii combinenga ya safari hii ni hatari wasifikirie kuiba kura kabisa option hii haipo kabisa.
Nimesomaaa kwetu sisi tulip Neutral . Hakuna HOJA yenye Mantiki Umeandika.
Zaidi ushabiki usio wa kisayansi.

Nilitegemea useme ni namna gani wanafanya kitu ambacho hakikutegemewa na ilitegemewa wafanye kwa namna gani.

Uko sawa na yule wa ccm aliyeandika CHADEMA YATHIBITIWA MBEYA halafu akatoa HOJA mfu zisizo na Mantiki

Tulieni Muandike vitu vya maana mnawapotosha watu wenu.
Wapeni taarifa za kweli ili wazifanyie kazi sio fake
 
Bashiru alikaririwa akisema uchaguzi wa 2020 ccm haina haja ya kutumia wasanii kwenye mikutano ya mgombea wao weeee!!wamepiga U-turn ya haja.
 
Back
Top Bottom