Mambo ya Walawi 18:22: Usilale na mwanaume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,651
18,021
Katika sura yote ya 18 ya kitabu cha mambo ya Walawi kwenye Biblia, Mungu amekataza mambo machafu yahusianayo na ngono ikiwemo kuoana na ndugu wa karibu, ikiwemo pia kulala na wanyama.

Uzi huu ni kumbushio maalumu juu ya unajisi utokanao na ushoga. Uchafu wa mambo hayo HUINAJISI NCHI, hata nchi hiyo hutapika wenyeji wake na kuwatoa. Mambo ya walawi 18:25 "Na hiyo nchi imekuwa najisi kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa".

Watanzania Mungu ametupa nchi nzuri sana yenye utajiri mwingi mno wa mali asili, tujiepushe na kuinajisi isije ikatutapika (tukabaki maskini kwenye nchi iliyo tajiri). Tutubu na Mungu atusamehe, maana kwenye hii nchi matendo machafu ya ushoga yapo, japo hasa upande wa mwambao wa bahari kutokana na athari ya Waarabu.

Tusiyaonee aibu bali tuyakemee kwa nguvu zote na tuwafundishe watoto wetu wasijiingize kwenye uovu huu. Vinginevyo watoto wetu watadhani ni mambo ya kawaida kama ilivyo kwa nchi za Magharibi!
 
Hakuna kitu kibaya kama kuinajisi nchi kwa kutenda maovu yaliyokithiri. Nchi ikikutapika hakuna anayeweza kukusaidia!! Ukiilima ardhi haitatoa mazao yake!!

Ukifanya biashara unaishia kufilisika au kudhulumiwa! Ukiajiriwa unaishia kufukuzwa kazi!! Hata ukiwa na ndugu wengi utaishia kugombana nao na mtachukiana mno! Nchi ikikutapika imekutapika!!! Watanzania wenzangu tujiepushe kuitia nchi yetu unajisi kwa uchafu wa ushoga!!
 
Agano la kale hilo halina impact zaidi ya history tu
Mungu ni yeye yule jana na leo na hata milele!! Uovu hauna agano la kale au agano jipya, tofauti ni jinsi ya kushughulika nao. Kwenye agano la kale uovu ulikuwa unaondolewa kwa sadaka ya kuteketezwa kupitia makuhani. Kwenye agano jipya uovu unaondolewa kwa kumwamini Yesu aliyemwaga damu yake msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.
 
Kwa wale wanaoweza, ni vizuri kuiombea sana nchi yetu iokolewe na uchafu huu wa ushoga. Kuna uzi humu unaoonyesha kiwango cha ushoga nchini kwetu kimeongezeka sana. Watu wanashuhudia jinsi wanavyovamiwa na kusumbuliwa na mashoga na wasagaji. Uzi huo unaitwa:

Wanawake au wanaume waliowahi kutongozwa na wasagaji/Mashoga watoe ushuhuda humu.​

Wengi wametoa ushuhuda wa kusikitisha sana na baadhi wanajisifia hadharani kufanya uchafu huo.
 
Wazazi pia tuwafuatilie sana watoto wetu, na kuongea nao. Kuna watu waharibifu huwanajisi watoto wadogo kinyume na maumbile na kuwatishia wasiseme.
 
Viongozi wa dini pia wawer mstari wa mbele kukemea na kuwafundisha watoto kuwasemea watu ambao watajaribu kuwaharibu.
 
Sasa hivi katika Ile posting nyingine anauliza kwa nini watu wa Kilimanjaro ni corrupt?(Kama kweli ni corrupt takwimu tu ndio zinaweza kusema).
Nilikuwa Marangu kwenye Guest House nasubiri kwenda kupanda Mlima. Nilikuwa nasikiliza redio( yangu) chumbani. Ilikuwa hii redio stesheni ya Kimarekani inahubiri Injili,nadhani yule aliyekuwa anaongea alikuwa Ni Padre. Alikuwa anaongea,akainukuu hiyo verse hapo juu,akaendelea kwa kusema,"Unaona basi? Kama ukilala naue ksma unavyofanya na mwanamke ndio makosa. Lakini ukimtafuna mwanaume kwa njia nyingine,hakuna kosa" Akawa anaendelea kuongea,"Fikiria ule mstari kabla ya hapo imeandikwa nini,( huo mstari kabla sijui umeandikwa nini)halafu ndio utaielewa hii verse vizuri zaidi. Hakuna kosa kumtafuna mwanaume,lakini usimlaze kitandani kama unavyofanya mwanamke. "
Haya ndiyo mahubiri niliyoyasikia pale from this very,very calm priest. Ain't that something?
 
Nilikuwa nasikiliza redio Kilmanjaro, ( nilikuwa Marangu,nikienda kupanda Mlima)ilikuwa mwaka 2000 ,ilikuwa redio ya Injili ya Kimarekani. Padre mmoja( nadhani alikuwa Padre,+unaweza vipi kujua ni Padre kama unasikiliza redio). Huyu Padre akainukuu hiyo verse,akasema,"Angalia, imeandikwa usilale naye kama mwanamke. Ukimtafuna vingine inaruhusiwa." Akasema,"Tazama ilivyoandikwa mstari uliopita( Sijui imeandikwa nini kwenye mstari uliopita). Lakini huyu Padre Marekani akasema,"Tazama ilivyoandikwa katika mstari uliopita na utaona dhahiri shahiri kwamba kinachokatazwa pale ni kulala Naye tu kama unavyolala na mwanamke."
Kama nilivyosema hii ilikuwa mwaka 200. Siku hizi huyu Padre mjanja nadhani ameshazuiwa kufanya mahubiri yake.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuinajisi nchi kwa kutenda maovu yaliyokithiri. Nchi ikikutapika hakuna anayeweza kukusaidia!! Ukiilima ardhi haitatoa mazao yake!!

Ukifanya biashara unaishia kufilisika au kudhulumiwa! Ukiajiriwa unaishia kufukuzwa kazi!! Hata ukiwa na ndugu wengi utaishia kugombana nao na mtachukiana mno! Nchi ikikutapika imekutapika!!! Watanzania wenzangu tujiepushe kuitia nchi yetu unajisi kwa uchafu wa ushoga!!
Ushoga na usagaji kweli ni mambo mabaya na yastahili kukemewa kwa kila namna.

Lakini hiyo nadharia yako ya KIROHO haina ukweli, nchi zilizo halalisha huo uchafu hizo shida hawana hata moja wanaishi vizuri raha mustarehe.

Sisi huku tunaojitahidi walau kukemea, maisha yetu unayaona yalivyo.
 
Agano la kale hilo halina impact zaidi ya history tu
Agano Jipya* ( Gay , Lesbian na Ufiraji wa Mke)

Warumi 1 : 26 - 32 "

" Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile. Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke, wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu. Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya "
 
Duh.!

Tunako amini mambo ya ushoga na usagaji ndiko yameshamiri hatiwazidi kwa utajiri na kufaidi matunda ya nchi yao.

Huku kwetu tunako kemea kwa nguvu mambo haya. Wanachi wake wanaongoza kwa kutokua na furaha, umaskini na kutofaidi matunda ya nchi yao.


Si saport ushoga na usagaji ila ushoga na usagaji sio chanzo Cha umaskini wa nchi yetu.
 
Mungu ni yeye yule jana na leo na hata milele!! Uovu hauna agano la kale au agano jipya, tofauti ni jinsi ya kushughulika nao. Kwenye agano la kale uovu ulikuwa unaondolewa kwa sadaka ya kuteketezwa kupitia makuhani. Kwenye agano jipya uovu unaondolewa kwa kumwamini Yesu aliyemwaga damu yake msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.
Hakika
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom